Mlioangukia pua kwenye kura za maoni mjifunze sio kukimbilia fomu tu kwa sababu una hela ya kuchukulia

Mlioangukia pua kwenye kura za maoni mjifunze sio kukimbilia fomu tu kwa sababu una hela ya kuchukulia

Kibosho1

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
2,621
Reaction score
4,293
Habari wana jamvi? 😁😁😁πŸ€ͺπŸ€ͺπŸ€ͺ😏😏

Nacheka kwa dharau sana hasa waliokurupuka kuchukua form na kuangukia pua kama paskal Mayala,Stive Nyerere,Gwajma n.k

Kwanini nawacheka? Ukiangalia wengi wamekurupuka kisa JPM anadaiwa kurudisha heshima chamani na ni mchapa kazi sana. Kutokana na wapinzani wengi kuunga mkono juhudi huenda ikawa rahisi kukubalika. Wengi wakaamini kwa sababu ni watetezi wa serikali huko mitandaoni,makanisani na sehemu zingine itakuwa rahisi kufikiriwa(sio kwa sera)

Watu wanashindwa kutofautisha umaarufu wao kwenye jamii na umaarufu wao kwa wajumbe wa CCM,hii ndio imefanya wengi kuanguka katika uchaguzi.

Anasema, Idriss Sultan "Juzi nimekaa nikafikiria, unakuta mtu anakimbizana na siasa miaka zaidi ya 10 na kawa mwanachama kindakindaki, hope yake awe kiongozi alafu anakuja msanii na followers wake ambaye amekuwa active kwenye chama wakati wa uchaguzi tu, kama mjumbe UTAKUBALI AKUPITE KWELI ???".

Hii ni kweli kabisa lazima mtu ukitafakari vizuri sana. Wewe unajikuta ni maarufu mitandaoni ni hodari wa makala au maarufu kwenye televisheni au radio unataka kutumia huo umaarufu kwenda kuchukua fomu kisa una uwezo wa kulipia hiyo laki 1 unasahau kuna wanachama wanazi kweli kweli wao uchaguzi mpaka uchaguzi ni harakati tu. Wewe harakati zako ni unapokaribia uchaguzi hujioni kama umetamani ubunge? Utakuwa na sera kweli?

Siku nyingine msirudie tena, endeleeni kuomba huenda mkakumbukwa siku Magufuli akiamka vizuri.
(Mchambuzi mdogo wa mambo ya kisiasa na kijamii)
 
Hao wametengenez CV ngoja uone watakavyokula teuzi.
 
Yani wengine walikuwa ni kupoteza muda tu,au kuwa maarufu
 
Hao wametengenez CV ngoja uone watakavyokula teuzi.

Wamebet kwa yaliyotokea 2016 matokeo yake mwaka huu kuna CV 10K+, na mkulu sasa hivi ameanza kurudi kwenye utaratibu wa Zamani ule wa vyeo ni kwa ajili ya promotion kwa watimishi wa umma. Wewe kada subiria uchaguzi ugombee.

CV 10,000+ unasoma ya nani unaacha ya nani.
 
Walifikiri ubunge kama kugombea utime keeper.Hawakujua kuna watu wamevuja jasho na damu.Wengine wamepoteza muda wao,familia zao,wapendwa wao,mali zao kwa hizo nafasi.

Sasa anatokea mtu huko na kaumaarufu kake kakupost picha inapata like elf kumi.Mawazo yanamtuma kuwa yeye ndo kipenzi cha watu Tanzania.

Nawapa pole sana mkate wa nchi ni mkubwa tuendelee na maisha mengine.Itabidi wamuulize Babu Tale imekuaje ametoboa .
 
Back
Top Bottom