Mliobahatika kupata kazi bila hata interview mtupe siri

Mimi mama aliniambia nenda pale kwa baba ako (uyu baba sijawahi muona kiukweli kabisa tangu nazaliwa) na kihualisia sio baba yangu basi nimefika pale nikaambiwa wewe ndio kikoozi, nikamuambia ndio akasema kumbe joyce ana mtoto mkubwa ivi, akaniambia karibu chai, nikanywa chai, nikaonyeshwa kiti changu na computer yangu ya ofisini. Nikapewa na laki 3 na nusu ya maandalizi ya kazi.

Hvyo, ila uyu boss wangu uwa nina wasiwasi uwa anamtafuna bi mkubwa wangu.
 
😁😁😁😁😁
 
Hii dunia you use what you have to get what you want. Kuna mhenga alisema,,"ukitaka kula......"
 
Walikuonea sana yaani boss atafune bi mdashi harafu akupe 1.25πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
acha tu ndugu, maana akuniuliza ata kama nitafanya nao kazi wanilipe sh ngapi yeye kesho yake akanipa tu mkataba nisaini, ndio ivyo nikasaibi ile milioni moja na laki mbili na nusu kwa shingo upande sana
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Yani wewe
 
Mwaka 2009 steadman (mikocheni) nilituma sana cv nikawa siitwi hata kwa interview nikaongea na mlinzi kwamba siku wakiita watu training aniambie, siku moja nikapigiwa simu na mlinzi njoo ghafla mikocheni hapa watu wameitwa training nikavaa fresh kabisa maana maana kupendeza kunaleta confidence.

Nikatimba training ikafika lunch time ikaja karatasi unaandika jina lako una sign buku tatu ya lunch mtiti ulianzia hapo kumbe wadau waliita watu mia tu na mimi nikawa wa mia na moja nikasema ukisikia mtu anafedheheΔ·a mbele ya pisi kali nyingi ndio leo nilikua nimekaa karibu na dirisha floor ya kwanza nikasema wakianza tu kupitia majina nakua spider man mlinzi getin kishakua rafik yangu halaf hampend muajili wake kukimbia haikua ngumu kabisa , mara paap jamaa wakasema hainakwere tuendelee tu training kumbe bhana kaz yenyewe ni ngumu balaa wanaanzaga mia wanakimbia mpaka wanabaki 10.

Ajira nyingi ndio ziko hivyo kujuana ,wengine ngekewa wengine kufosi miksa milungura.

Baada ya kupata degree yangu nimeona kuajiliwa ni ubatili mtupu nimejiingiza kwenye ujasiliamali na mtaji wa kinyonge changamoto zake ni nyingi ila kwa vile ndio kitu napenda wala sioni shida ila ndugu zangu ndio wananionea huruma balaa
 
Connection tu boss,,,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…