Tumia mbinu chache tu, na matunda utayaona!
1) Ishi mbali kabisa na familia. Yaani ishi Mkoa wa mbali kidogo kutoka kwa hao ndugu zako. Na uhakikishe wanakubatiza jina jipya la SINA HELA! Yaani wakikupigia simu kwa ajili ya kukupiga mzinga, jibu lako liwe fupi tu; mimi SINA HELA! Watakusema weeeh! Baadaye watazoea.
2) Hakikisha huwaambii mipango yako ya maendeleo/wasifahamu mali unazo miliki/ ulizonunua. Yaani kwao iwe suprise tu, siku wakija kwenye matukio.
3) Jitahidi uwe na nidhamu ya fedha. Yaani tumia 1/3 ya kipato chako. Na ili ufanikiwe katika hili; ingia benki, vuta mkopo chefu chefu! Fanyia malengo. Kinacho bakia, ndiyo upambane nacho mpaka akili ikukae sawa.