Mliofanikiwa kimaisha kwa kutumia kanuni ya 'Ubahili' mliwezaje, mbona mie nashindwa kabisa?

Usimuweke ndugu yako kusimamia biashara yako hautaweza kumcontorl na utagombana naye undugu utakufa bure ndugu ni WA kuweka mbali na Mali zako na vitega uchumi vyako labda kama uyo ndugu naye ni mchakarikaji Ila kama ni goigoi kaa mbali naye utalia na hutakiwa na la kumfanya
 
Shida haziishi Mkuu,

Mm ndo maana nilifurahi kuhamishiwa mkoani kikazi, Kituo changu cha kazi ni mkoa ambao Sina hata ndugu. Kama ni shida za ndugu na jamaa zote huwa najulishwa kwenye simu.

Zenye uzito huwa nasaidia, zisizo na uzito huwa nazipuuza.

Huwezi kumsaidia kila mtu, shida haziishi. Nilitumia miaka miwili tangu kuajiliwa kusaidia watu wa karibu. Kwasasa nasaidia ndugu wa damu na close friends tu. Tena kizuri ni waelewa wanajua Hali ni mgumu hata nikiwaambia Sina wanaelewa.

Kufanga kazi mbali na mkoa ambao ndugu na jamaa zako wanaishi ni nafuu zaidi kwa watu wenye mioyo ya huruma Kama ww.
 
Mkuu nimekupata vema. Hapo inabidi usipende hata kujiunga kwenye magroup ya WhatsApp ya Familia/Ukoo. Maana ukiwa huko ni kama upo tu home bado. Kila wiki itakuja taarifa ya michango/matatizo. Na inakuwa haiishi. Noma sana Mkuu.
 
Mara nyingi wema wako hukuponza, ukienda kwa mzungu bila taarifa hata kama anakula wewe utaendelea kusoma gazeti mpaka amalize kula. Hata kama ukitoa taarifa kama budget yake hairuhusu anakunambia usiende. Huo ndio ubahili wenyewe, ukiufuata vizuri utakuta una akiba nzuri kwa mwezi. Ila usiache kulipa fadhila kwa waliokusaidia, kwa kadiri ya uwezo wako na mahesabu makali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utajiri au mafanikio hayqji kwa kuwa bahiri mkuu,ni Nia na kuamua pasipo kugeuka nyuma au kujiulizauliza .uamie haswa.fanya kazi kwa juhudi na usisahau kutumia akili kwa kila Jambo,uthubutu ni muhimu pasipo hofu Wala woga. kanuni ndo hiyo
 
Jaribu kujiweka kwenye hiyo orodha ya kuwasaidia wengine, kila mwezi jilipe kiasi fulani, ambacho hukigusi mwezi hadi mwezi na itakapofika baada ya mwaka, angalia umekusanya kiasi gani na kinaweza kununua au kuwekeza kwenye nini.
Kwa Tz matatizo na umasikini hauishi, usipokuwa muangalifu utakuja juta baadae.
 
Hapo kwene kulipa fadhila mkuu ndio shughuli haswa. Maana sie watoto wa maskini unakuta tumesaidiwa na utitiri wa watu. Sasa hapo kila mmoja mpaka umlipe fadhila ndio unajikuta kila mwezi unatatua shida za ukoo. Japo ni jambo la msingi sana kama unavyosema. Ila kama umezaliwa ushuani wala unakuwa hufahamiki na wana ukoo kiviile, maana wanakuwa wanakusikia tu juu juu. Shida akina sie wa vumbini, unakuta umesaidiwa na kila mtu yaani. Hapo familia zao wanakutegemea pia ulipe hiyo fadhila.
 
Zingatia yafuatayo: (Naongea kwa uzoefu na majuto, Trust me I know)

1. Kuwa na Malengo yako binafsi na yaandike mahali yaani uwe na malengo ya kwamba unataka kutimiza nini ndani ya miezi 6 au Mwaka. (Hakikisha hakuna mtu yeyote anajua hili even your wife)

2. Marufuku mtu yeyote kujua kipato chako(kwenye hili tumia 'nguvu' ya ziada kuficha)

3. Wazazi waliokuzaa wape kipaumbele nambari moja katika kuwasaidia. (No limits on this)

4. Misaada ya aina yeyote kwa wengine tofauti na wazazi I mean hata ndugu wa kuzaliwa hakikisha ni lazima na iwe 'Life Threatening' sio unamsaidia mtu fedha ya Vocha, really!!? Au eti braza nimeishiwa ninunulie Bia au King'amuzi kimeisha, Aisee mimi utasubiri sana.

5. Misaada mengine kama Malipo ya Ada, Fine au Manunuzi ya Dawa. Fanya kulipia wewe kisha watumie Risiti. Usimuamini mti yeyote kwenye Fedha ambayo ni jasho lako... Pesa ina ushetani wa ajabu sana.

6. Usipende wageni/ kumkaribisha kila mtu nyumbani kwako. Macho ya watu/ ndugu ya uchawi sana. In-fact kuwa makini na wageni wako na hasa ndugu wa karibu ukiweza muwe mnakutana nje na nyumbani. (Hili ni gumu lakini ni muhimu na lina faida kubwa sana)

7. Na 8. Ntaendelea...
 
kiswahili ni lugha ya taifa...khaaaa......
 
Asante sana Mkuu. Tunasubiri muendelezo.
 
Mke atatoa na kukuibia juu.
 
Kama ukikataa nafsi yako INAKUSUTA mimi nakushauri endelea tu kuwapa , inawezekana unapata kwa sababu unatoa
 
Kama ukikataa nafsi yako INAKUSUTA mimi nakushauri endelea tu kuwapa , inawezekana unapata kwa sababu unatoa
Changamoto yake ni kwa nitaendelea kuwa 'an average person with regards to finances'. Yaani Mkuu inaonesha watoaji wengi huishia kuwa maskini ama watu wa kawaida sana kiuchumi huko mbeleni. Ineonesha ili ujijenge kiuchumi formula namba moja dhibiti milango ya kutolea fedha. Unapodhibiti milango ya kutoa pesa ni pamoja na hii habari ya kutoa pesa kwa watu kwa lugha ya kusaidia. Ndio wajuvi wanavyodai hivyo. Hasa waliofanikiwa tayari.. Hapo sasa inabidi kuchagua kimoja. Either ukubali kuwa mtoaji kwa watu na uishie kuwa mtu wa kawaida ama ukubali kuitwa bahili na majina mengine mabaya kama vile mchoyo ili utoboe. Haya maisha mkuu kiufupi ni complex sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…