Mliofanikiwa kwenye Network Marketing tunawaomba mtoe Ushuhuda hapa

Kuna mshkaji niliwahi fanya nae kazi sehem flani kabla sijaacha pale na kuhamia kwingine, sasa akawa ananisumbua na mameseji mara kuna opportunity sijui e-Commerce nataka tufanye itatutoa kimaisha, ukimuuliza ni nini hasa mnafanya? Hasemi ye anataka tuonane anieleze vizuri hiyo fursa, ukiangalia Status zake za Whatsapp asubuhi mpaka jioni ni Motivational Quotes tu za Financial freedom na zinazodharau waajiriwa, Mara mapicha ya Safari n.k, siku naonana nae nikamkuta na jamaa flani sura yake anaonekana hana furaha halafu kachoka, wote wamenyonga tai nikajua tu hawa ndio yaleyale ya network marketing ila nikajifanya sijui kitu, yule jamaa mwingine ndio kaanza kunipa somo na likitabu lao issue za QNet, nimewasikiliza bila kuwa-interupt for 2hrs, walivomaliza wakasema tutapanga session ya pili nikasema poa, nilivoondoka kesho yake nikamwambia yule mshkaji siwezi kufanya hiyo biashara yenu wala usihangaike kunitafuta tena, nimeblock na namba zake nadhani na urafiki mdogo uliokuepo umeisha rasmi. Nafikiri aliona mimi ni easy target.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo swali ni non-starter..

Hata kama waliofanikiwa wapo sio kwamba na wewe utafanikiwa.., Kwa muundo wake wa kupata commission kwa recruitment basi ni hakika wapo waliofanikiwa kwenye tiers za juu hadi kufikia kukurecruit wewe ni kwamba kuna mtu kapata pesa..

Network marketing faida yake kubwa ni contacts and through those contacts wajanja wanauza bidhaa zao pia sio za kampuni tu.., yaani seminars, vitabu n.k., ila kama unataka uingie ili utajirike kwa urahisi might not be that easy..
 
Siku moja nilihudhuria semina yao wale Aim Global jamaa mmoja akajinasibu kumiliki magari na pesa Cash nyingi kama milioni 109 tulivyomaliza Semina zao nikaenda kwa Mama ntilie kupata lunch wale Mama ntilie wa Barabarani chakula cha 1500 nikashangaa namkuta jamaa mwenye milioni 109 tunakula nae Chakula cha 1500 nikasema Hiiiiiiiiiii
 
Kawaida hawakubali kuongea hii ishu kwenye simu.

SangaweJr
 
Ngoja na Mimi nitoe experience yangu niliwahi kujiunga na oriflame baada ya kumaliza chuo ,nilichagua kujiunga na oriflame kwa sababu Kwanza kiingilio kilikua kidogo(37000/= hapa unapata na baadhi ya products unachagua mwenyewe) Halafu pia aina ya products zao ilinivutia Sana... kwenye kufanya biashara ni wewe utaamua bidhaa gani uanze nazo...unaweza unachagua bidhaa moja tu ndo ukadeal nayo mfano skincare set, au perfume tu,au feminine hygiene, au makeup kits..then kuanzia hapo ndio unaanza kutengeneza wateja wako,uzuri wa hii mtu akishatumia product Halafu imemsaidia Basi unamuambia tu unaweza kujiunga na wewe ununue at a more affordable price tayari unaongeza mtu kwenye network yako.
Cha kuzingatia Kama unauzaje skin Care products please make sure your skin can vouch for you..la sivyo Anza na product nyingine.niliacha baada ya kuanza kufanya kazi ya kile nilichosomea ila mpaka Leo natumia baadhi ya product za oriflame.
 
Vp ulikuwa unaingiziwa pesa kwa account yako??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni jana tu jirani yangu anniambia toka huko migodini njoo tufungue ofisi yetu tuanze kutajirika😊😊..nikamwambia anza tu..watu wa qnet hao!kauza gari kaingia qnet🤣🙌🙌
Duuh maskini RIP😂😂😂kajitafutia gonjwa la moyo bure
 
Oriflame kiingilio ni 10,000
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana majigambo sana kuna jamaa mmoja alikua ana tufanyia presentation anasema kma ana afford kuvaa saa ya million 5 je akinunua gari itakua ya million ngapi? nikabaki nacheka tu hao viumbe ni kama kuna kitu hua wanapewa maana sio kwa imani hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwashakoo tena? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] funguka mkuu mbinu uliyotumia kuwatapeli mm mwenyew niijaribu

Sent using Jamii Forums mobile app
yule yule dem alikuwa kimbelembele kuniset alinipigia sim tukuta dar free market kuna mgahawa expensive unaitwa terence.akawa ananiletea pigo zake za kujiona expensive nimetumia vyake kama lunch ya 35.then nikamdrive mpaka ofisini kwao kesho yake nikampiga soundi aniongeezee laki tano maana nauza gari nije kulipia..akaja mpaka nyumba nilio panga tukawa tunauzia gari kimagumashi na dadaangu akatoa pesa akijua wanajiongeza mkenge.jioni yake tukahama coz nilikuwa nimepanga kuhama mda tu. Ile miatano yake nikaitumia kuhama na nikanunua flat
 

Umenifanya nicheke ila tu sipo katika mlengo wako


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…