Mliofanikiwa kwenye Network Marketing tunawaomba mtoe Ushuhuda hapa

Mliofanikiwa kwenye Network Marketing tunawaomba mtoe Ushuhuda hapa

Katika hizi biashara za networking naona 98% tunajua kua ni utapeli, labda niseme ivi kuna baadhi ya companies ndio haziko vizuri , ni sawa tu na biashara nyingine ambayo mtu anaweza anzisha na mwisho ikaenda ndivyo sivyo na kudondokea pua au ikaenda vyema akatusua. Binafsi naweza kushuhudia company moja tu ninayoifahamu, yenyewe bidhaa yake ni tofauti kidogo na zingine zooote. Kuna watu zaidi ya kumi kwa harakaharaka wengine wakiwa na vyeo maalumu selikarini wapo ktk company hiyo na wanapata pesa nzuri kama vile angewekeza ktk biashara nyingine na ikastawi tu.

Kinachokuja kuvuruga na kuona ni utapeli katika baadhi ya aina hii ya biashara ni pale baadhi ya companies kusema utatajirika haraka, kusema ukweli hakuna muujiza uo labda iwe kwa kagere,

Hivyo mimi naona ni biashara kama zilivyo biashara zingine za kawaida kama tigopesa mpesa nk

Kikubwa ni strategies zako tu katika kuiendesha


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kila network marketing ni ya uwongo coz mm kunamtu namfahamu yupo forever living alikuwa hana gar wala hela ila now anagari na nyumba ila yupo kwenye Hiyo busness 10yrs now coz ts all about finding a customers wanunue ile product ulipwe percentage yako inaingia bank mm nikikuwa nina mindset kama zetu ila mm nimeona kwa macho yangu watu waliofanikiwa kupitia hiyo forver living ukiwa mvivu miez miwil mingi unafell unaona ningumu unaishia njian ila ukikaza kwel mwsho wa siku lazma unfanikiwe coz hakuna mtu anaeshika hela zako na pia ukishindwa hela yako inarud kwakupewa wateja wanunue hizo product utakazopewa
sio kweli upewe wateja akati wateja ni deal mnawagombania kwa gharama upewe umekuwa nani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuh maskini RIP😂😂😂kajitafutia gonjwa la moyo bure

Alafu ndo kwanza wanandoa wapya...!nilimuask ushawah isikia sehem akasema hapana ...ndo ameisikia...eti oh kuna dk wa operation kaacha kazi ndan ya miez minne amejenga ghorofa..ati alikua anabadili magari wasap ndo mumewe kumuask ndo kumpa siri hyo .the following month mume kaacha kazi hahahaha
 
Duh ofisi ya q net?.Yaani hii kitu ni kama ina mtia uchizi mtu maana hawaambiliki kabisaa
Ni jana tu jirani yangu anniambia toka huko migodini njoo tufungue ofisi yetu tuanze kutajirika[emoji4][emoji4]..nikamwambia anza tu..watu wa qnet hao!kauza gari kaingia qnet[emoji1787][emoji119][emoji119]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi network marketing labda niende kutafuta mademu. Maana kuna mademu wazuri kweli ila naona akili hazipo kichwani.

Saiv wapo kama wawili hivi nachat nao. Nasubiri niwale kimasihara ili na me nikatoe ushuhuda kule kwenye uzi wetu pendwa.
Wakuu,
Mwishoni mwa mwaka jana Mdogo wangu (Mwanafunzi wa chuo Kikuu Ardhi) alinitumia ujumbe Uliosomeka " Bruv! Nimepata platform ya kupiga pesa, Sure am telling you bruv am gonna be a great millionaire in just few coming days". Nikamuuliza, "Vipi umepata dili la kuwa Contena?(kwa maana ya Msafirishaji wa madawa ya kulevya)" .......Akanijibu "Bruv i just need you to lend me 560k Tshs nimepata nafasi ya kuwa milionea kwa kutengeneza pesa na Kampuni moja ya Kifilipino inaitwa Alliance In Motion Global after one year hata wewe nitakuwa nakupumulia kisogoni". I was shocked kivipi laki tano na sitini izae mamiloni ndani ya mwaka mmoja!! Nilimuuliza dogo iwapo amefanya utafiti wa kutosha juu ya hiyo anayooita "platform" na kunijibu kuwa ameshafanya na anawajua watu wengi waliotusua kupitia hiyo Alliance.

Binafsi nampenda sana mdogo wangu, Sikutaka afikirie kuwa namnyima nafasi ya kutekeleza,adhma yake (Japo nilikuwa na wasiwasi) niliamua Kumtumia Sh. Laki 7 ili akifanya hayo mambo yake abaki na balance ya kutumia kwa muda (ili tusisumbuane tena).....Now ni mwezi wa 6 huu unaelekea wa 7 tangu ajiunge sioni mabadiliko yoyote, mara ananiambia "Bruv, Haya mambo hayataki haraka pesa ipo inakuja". Mara, "oh! natengeneza Pair ya watu wangu ili nianze kulipwa".....Kuanzia hapo nikajua tu kuwa mdogo wangu alipotea njia kwa kufuata mkumbo na kukubali kuingizwa mkenge coz mpaka sasa hazipiti wiki mbili bila kuniomba pesa za,matumizi.

Siku moja tena ya Mwezi February kuna dada alinifuata ofisini akataka tuongee ili anishirikishe busness yao alijitambulisha kwa A.k.A ya Cherry...nilimpomkubalia akaniambia kuwa anafanya kazi na kampuni ya QNET na kuna mtu alim'direct kwangu (alisita kumtaja) ndipo akaanza kutoa "Likitabu" lake lina picha za simu, saa, mikufu nk. Kwa ufupi tu ni kwamba alinieleza kuwa kwa kiasi cha kuanzia dola 2000 kwa maana ya Shilingi milioni tano pekee naweza kununua bidhaa moja kama vile saa au mkufu na nikishirikisha wenzangu wengine nitaanza kulipwa pesa...Niliposikia hivyo nilimwangalia yule dada nikamwambia kwa ufupi ".Sista nipo busy sana kwa sasa na pia siwezi kufanya hiyo biashara yako am so sorry".aliondoka akiwa na mfadhaiko usoni mimi sikujali coz Niligundua kuwa hawana tofauti na wale Alliance waliomtapeli mdogo wangu miezi kadhaa iliyopita.

Nyie watu Wa Hayo makampuni tajwa hapo Juu na ninyi mliofanikiwa kupitia haya makampuni (kama mpo humu) hebu jitokezeni mtujuze mlitumia njia gani..otherwise i declare you kama Matapeli mliofumbiwa macho na Serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
No, mimi nna ujuzi wa vifaa vya electronics kuna sehemu nli igusa makusudi ika anza kusumbua wakanipa nika rekebishe nika kaa nayo almost one month baadae nika waambia haiwezi kupona wanunue tu nyingine nika iuza laki 7 nikapoza majeraha yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee, atleast ulipunguza hasara mkuu[emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaah mwenyewe nilipelekwa na sister angu ulivyoambiwa ww na mimi niliambiwa hivo hivo mzee.bahati nzuri sikuwa na pesa tu ningetoa wanamaneno matamu mazuri ya ushawishi .
Hii thread inataiwa ipestiwe kwenye magroup ya whatsapp ili watu ambao bado hawajajiunga, waweze kujua kile kinachoendelea huko mtaani.

Kwani binafsi nnakumbuka, kuwa nliambiwa nisiwaambie watu hadi pale ntakapo kuwa nshajiunga.

Kilicho niacha bumbuwazi, pale mmoja wa presenter aliponambia kuwa, hii sio biashara ya kila mtu. Ni kwa ajili ya watu wachache ambao, ndio maana aliyenialika aliamua kunipendelea ili na mimi niweze kufanikiwa kama yeye, ndio maana akaamua kunialika, hivyo nisiichezee hiyo bahati, pia natakiwa kumheshimu sana business partner aliyenialika kwani amenionyesha ulipo utajiri uliokusudiwa kwangu mara baada ya kuzaliwa. Nisiiache hiyo bahati inipite.

Akanambia,
Hii biashara ingekuwa ni kwa ajili ya kila mtu,
Basi hapo nje pangekuwa hapatoshi kwa mafuriko ya watu
Wanaotaka/gombania kujiunga. Ila wameifanya special isiwe kwa kila mtu
Ili utakapofanikiwa na wengine wakakuona mtaani, waweze kukuuliza wao wenyewe, na wala sio wewe tena kwenda kuwatangazia biashara.

Binafsi tena kimoyo moyo,
Nkawa najisemesha, hayo mafuriko ya watu anayozungumzia kuwa
Hapo nje pangekuwepo na rundo la watu wanaotaka kujiunga kama hii biashara ingekuwa ni fursa kwa kila mtu, nkajiuliza

“Kwa usawa huu wa Magu, ni nani ambaye yuko tayari kwenda ku risk 5m yake kwenye Deci”
kwanza upatikanaji wake tu ulivyo mbilinge.

Huwezi amini,
Ukiwa QNET au AIM GLOBAL, unashawishiwa hadi kuuza
Nyumba,kiwanja,gari au chochote cha thamani
Ulichonacho huku wakiku laghai kuwa ndani ya miezi3, hela yako inakuwa imerudi na kutengeneza rundo la utajiri.

Jamani,
No easy money.
Tujitume, tufanye kazi.

NB; biashara ya PONZI SCHEME kama ni mpya na ndo kwanza imeingia nchini, jaribu ku risk, kwani wale wa mwanzo, uwezekano wa kupiga hela ni mkubwa kama mtaweza kuitangaza vizuri biashara yenu.

Kuna moja iliwahi kunitoa,
Ilipo ingia, nkagundua kuwa ndio kwanza tuko watu 15 tu kwa TZ,
nkapiga mpunga 56m,
Wakati nlichokuwa nmeinvest ilikuwa ni 1.8m
Hutoweza ku feel utajiri kwani hela yenyewe inakuwa inaingia
Gradually. Na wewe huku ukiwa na mahitaji ya kila siku.
 
Aisee ckiwahi kuwaelewa hawa watu! Me nilifatwa na watu kibaoo...ooh korino wewe unapenda biashara so this kitu itakupa mafanikio!
Napenda biashara ndio ila c biashara yakuanza kumconvice MTU anunue bidhaa kwa hela ndefu....mwisho wa siku hanunui huku mdomo umechoka kwa kuongea na taya kuuma! Aku cwezagi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mstaafu mbibi wameshampiga million 4 za kuuza kiwanja chake.
Hapa wanamvizia apate pesa ndefu zaidi maana ana tarajia kupokea si chini ya 40m wanataka kumpiga.
Huyu bibi hata unieleweshe vipi haelewi a naamini mahela yatamiminika kwa akaunt yake.
Goodmorning Business partner[emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nmepitia comments zote sas nmepata jibu fasaha kwa jamaa ang alonialika qnet. ..maana simu zimekua too much had nahis kumshusha viwango
 
Back
Top Bottom