Mliofanikiwa kwenye Network Marketing tunawaomba mtoe Ushuhuda hapa

Hahaaa hii maza alijiunga kupitia vikundi vyao vya vicoba nikamtahadharisha hakuelewa, sijui iliishia wapi ila kile kikundi kilishatawanyika
phyto science? Siyo watu wazuri walipita na mils 18 za mwana
nga
 
Oriflame kiingilio ni 10,000

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakumbuka Oriflame walifunga ofisi hapa Tanzania..... Hizi products kwani bado zipo sokoni???
 
Nakumbuka Oriflame walifunga ofisi hapa Tanzania..... Hizi products kwani bado zipo sokoni???
Ofisi walifunga hapa Tanzania,kwa east Africa ofisi zimebaki Nairobi tu na watu wengi ambao bado wanaendelea na biashara products wanachukua kutokea Nairobi.
 
Mm ni muhanga wa Alliance in Motion Global walikua na project yao wanaita Economy Driver mwaka 2021 nilipokua nipo mwaka wa 2 chuon UDOM nilijiunga kwa mtaji wa 360K niliendaga ofisini kwao Majengo sokoni nilishawishiwa na hao watu wa hyo kampuni mm nilipelekea ofisini na rafik angu niliekua nasoma nae ila kiukweli nilifanikiwa tu kuwa na watu wawili na kuambulia 72K nilimuunganisha mdada mmoja naye anaumia namna alivyopoteza pesa yake Alliance jamaa ukiwa unajiunga wanakwambia kama huna mtaji anza na kujaza fomu ya kujiunga kwa 30K then hapo unashika nafasi watu watakaojiunga watakua chini yako na ww utapata team ukikamilisha mtaji wale waliojaza fomu watakua ni team yako na utaanza kupata pesa lakn ukijiunga wanakuambia fanya kazi ya kutafuta watu hao watu ulioahidiwa huwaoni alaf hawa jamaa wanakuaga waongo wanasema walijiunga na hyo biashara wakiwa wanachuo alaf kila mmoja anasema alikosa mkopo kipind anasoma chuo wakajiunga na biashara ikawasaidia nakumbuka ile siku kuna binti alijiunga pale pale akasema ametoa ada aliyopewa ili ajiunge na biashara ya Alliance Jamaa waongo sana hizo products zenyewe kuuza haziuziki mm najutia kujiunga na huo upatu na style zao za makofi one million two million three million
 
Pole mkuu
 
Mjini watu hawatumii nguvu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…