Ngoja na Mimi nitoe experience yangu niliwahi kujiunga na oriflame baada ya kumaliza chuo ,nilichagua kujiunga na oriflame kwa sababu Kwanza kiingilio kilikua kidogo(37000/= hapa unapata na baadhi ya products unachagua mwenyewe) Halafu pia aina ya products zao ilinivutia Sana... kwenye kufanya biashara ni wewe utaamua bidhaa gani uanze nazo...unaweza unachagua bidhaa moja tu ndo ukadeal nayo mfano skincare set, au perfume tu,au feminine hygiene, au makeup kits..then kuanzia hapo ndio unaanza kutengeneza wateja wako,uzuri wa hii mtu akishatumia product Halafu imemsaidia Basi unamuambia tu unaweza kujiunga na wewe ununue at a more affordable price tayari unaongeza mtu kwenye network yako.
Cha kuzingatia Kama unauzaje skin Care products please make sure your skin can vouch for you..la sivyo Anza na product nyingine.niliacha baada ya kuanza kufanya kazi ya kile nilichosomea ila mpaka Leo natumia baadhi ya product za oriflame.