Mliojenga shikeni Maua yenu!

Mliojenga shikeni Maua yenu!

Wazee Mimi nimejichanganya nimejenga nyumba Kali nimeezeka bati Kali nimeweka grill nikachimba shimo la choo nikalifunika Hela zimeisha hapa Nina kende tu na inatakiwa nihamie.
Hizo kende ziuze upate pesa ya kumalizia 😂😂😂
 
Waga nikikuta fb,fundi njaa njaa anapiga picha nzurii anakwambia mpaka kuisha 7m nacheka tu,Mimi mwaka Jana nikasema nijenge chumba kimoja Mara nikasema acha nijenge chumba self na sebure,nilianza na Moto 😆😆 hapo Yani Sina bajeti Wala nin,nikafika lenta nikapumzika mwezi nipapiga bati,tokea hapo nipo hoi balaa,unakuta najifariji nampigia fundi nipimie madirisha hapo niletee site alafu kimyaa,juzi Napo nikamwambia embu nipigie hesabu ya shimo la choo na lafu floor kaenda site kapima kanipa hesabu nimeandika nimeweka pembeni,Yani fulu kujifariji Ila mwaka ujao nitapambana nihamie
Kila la kheri.
 
Asante sana. Binafsi nimepokea maua kwa moyo mkunjufu sana. Unaweza ukakadiriwa nyumba hadi kukamilika itakugharimu Tsh 60m, lakini siku ya mwisho ikasimamia Tsh 80m.

Mwanzoni nilikuwa naandika gharama zote ninazotumia. Kila nikinunua kitu, naandika. Baadae nikaona ni ujinga huu kuandika andika. Maana unakuta kuna matumizi mengine unayasahau. Muda wote unakuwa kama karani. Nikajisemea moyoni, kwa kuwa ninausimamia ujenzi mimi mwenyewe hakuna haja ya kuandika. Halafu je, kwani nikiandika..nitarejeshewa pesa zangu?

Sent from my Infinix X6816 using JamiiForums mobile app
Ukiandika itakusaidia kujua thamani halisi ya nyumba yako. Hata ukitaka kuiuza utaiuza kwa bei ambayo itakupa faida
 
Pesa ya emergency lazima na wanashauri pia ukipata mtu makini kuna nyumba ya kawaida na gorofa ... Kweny gorofa unaweza kuweka pesa ya emergency hata zaidi ya mil 30 kwa wale waonfanya ujenzi wa moja kwa moja ili kumaliza.

Mara nyingi inaweza isitumike kabisa.
Ghorofa asikwambie mtu, ujenzi wake ni shughuli pevu. Tena ukipata Msimamizi wa Ujenzi Mjanja mjanja ndio balaa zaidi.
 
KQUOTE="Jane Lowassa, post: 48169015, member: 365567"]
Gharama zisizotajwa: kuchekecha mchanga, kubeba cement, maji ya kumwagilia, kujaza kifusi, mara mirunda ya kusimamia, sijui kuweka milango na madirisha
[/QUOTE]
Kufyeka nyasi😅😅
 
Marhaba ukitaka kujua shuuli ya nyumba pale unapoanza kuongea kiingereza kupandisha boma eti tofal mchanga na cement sio issue sana shuuli unapoanza kuzunvumza kiingereza blandaring rental finishing wirering plumbing plaster floor tiles na n.k
 
Asante sana. Binafsi nimepokea maua kwa moyo mkunjufu sana. Unaweza ukakadiriwa nyumba hadi kukamilika itakugharimu Tsh 60m, lakini siku ya mwisho ikasimamia Tsh 80m.

Mwanzoni nilikuwa naandika gharama zote ninazotumia. Kila nikinunua kitu, naandika. Baadae nikaona ni ujinga huu kuandika andika. Maana unakuta kuna matumizi mengine unayasahau. Muda wote unakuwa kama karani. Nikajisemea moyoni, kwa kuwa ninausimamia ujenzi mimi mwenyewe hakuna haja ya kuandika. Halafu je, kwani nikiandika..nitarejeshewa pesa zangu?

Sent from my Infinix X6816 using JamiiForums mobile app
Tetetetete mi nakumbuka kipindi najenga nilikua naingia kazini mchana kuanzia asuhi nipo saiti wife analeta mboga Mimi na mafundi wangu tunasonga ugali crate za bia hazipungui mbili kula dadeki. Mpaka naenda kujiandaa kuondoka kazini nipo chwee kama ndo Mimi saidia fundi. Kisa wasini pige tu

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Hizo vitu zingine ukweli ndio zinaletaga maumivu ya shingo.

Nikaambiwa mbao za lenta kukodi,jukwaaa zote zinakodshwa kwa siku na mbao tutakaa nazo wiki mbili.

Piga hesabu pale ikaja Laki 3 na 20 hapo na kupunguziwa bei juu.

Hii hela imeniuma na itaendelea kuniuma na nimesema sitoanza ujenzi popote pale kama sijanunua hizo Mbao hata kama zitabaki ila haziozi.

Kukodisha Laki 3 kweli nikaamini wachina wametuzidi sana maarifa katika Ujenzi.

nilikua naona wanachukua marine board mpyaaaa inakatwa katwa wanaitumia hawakodshi cha mtu.. Sasa ndio nimeelewa.
 
Marhaba ukitaka kujua shuuli ya nyumba pale unapoanza kuongea kiingereza kupandisha boma eti tofal mchanga na cement sio issue sana shuuli unapoanza kuzunvumza kiingereza blandaring rental finishing wirering plumbing plaster floor tiles na n.k
mkuu una fundi wa blandaring unaemjua wa bei kitonga room zipo 3
 
Ujenzi makadrio wanaweza kuwa sawa ila ukiambiwa nyumba inaisha kwa 10m ukiwa na 10m peke ake Nyumba haiiishi ng'o.

ukiambiwa nyumba inaisha kwa 20m ukiwa na 20m peke ake hutoboi.

Labda ununue nyumba hapo sawa ila sio ujenge,ujenzi hauna makadirio tunapotezana tu
 
Mie naheshimu sanaa mwenye nyumba yake hata chumba kimoja , shughuli ya ujenzi kwa mtu mwenye kipato cha kuunga unga sio ndogo aiseee
hakuna kipato kikubwa wala kidogo komaaa
 
Back
Top Bottom