Mliojenga shikeni Maua yenu!

Wazee Mimi nimejichanganya nimejenga nyumba Kali nimeezeka bati Kali nimeweka grill nikachimba shimo la choo nikalifunika Hela zimeisha hapa Nina kende tu na inatakiwa nihamie.
Hizo kende ziuze upate pesa ya kumalizia 😂😂😂
 
Kila la kheri.
 
Ukiandika itakusaidia kujua thamani halisi ya nyumba yako. Hata ukitaka kuiuza utaiuza kwa bei ambayo itakupa faida
 
Ghorofa asikwambie mtu, ujenzi wake ni shughuli pevu. Tena ukipata Msimamizi wa Ujenzi Mjanja mjanja ndio balaa zaidi.
 
KQUOTE="Jane Lowassa, post: 48169015, member: 365567"]
Gharama zisizotajwa: kuchekecha mchanga, kubeba cement, maji ya kumwagilia, kujaza kifusi, mara mirunda ya kusimamia, sijui kuweka milango na madirisha
[/QUOTE]
Kufyeka nyasi😅😅
 
Marhaba ukitaka kujua shuuli ya nyumba pale unapoanza kuongea kiingereza kupandisha boma eti tofal mchanga na cement sio issue sana shuuli unapoanza kuzunvumza kiingereza blandaring rental finishing wirering plumbing plaster floor tiles na n.k
 
Tetetetete mi nakumbuka kipindi najenga nilikua naingia kazini mchana kuanzia asuhi nipo saiti wife analeta mboga Mimi na mafundi wangu tunasonga ugali crate za bia hazipungui mbili kula dadeki. Mpaka naenda kujiandaa kuondoka kazini nipo chwee kama ndo Mimi saidia fundi. Kisa wasini pige tu

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Hizo vitu zingine ukweli ndio zinaletaga maumivu ya shingo.

Nikaambiwa mbao za lenta kukodi,jukwaaa zote zinakodshwa kwa siku na mbao tutakaa nazo wiki mbili.

Piga hesabu pale ikaja Laki 3 na 20 hapo na kupunguziwa bei juu.

Hii hela imeniuma na itaendelea kuniuma na nimesema sitoanza ujenzi popote pale kama sijanunua hizo Mbao hata kama zitabaki ila haziozi.

Kukodisha Laki 3 kweli nikaamini wachina wametuzidi sana maarifa katika Ujenzi.

nilikua naona wanachukua marine board mpyaaaa inakatwa katwa wanaitumia hawakodshi cha mtu.. Sasa ndio nimeelewa.
 
Marhaba ukitaka kujua shuuli ya nyumba pale unapoanza kuongea kiingereza kupandisha boma eti tofal mchanga na cement sio issue sana shuuli unapoanza kuzunvumza kiingereza blandaring rental finishing wirering plumbing plaster floor tiles na n.k
mkuu una fundi wa blandaring unaemjua wa bei kitonga room zipo 3
 
Ujenzi makadrio wanaweza kuwa sawa ila ukiambiwa nyumba inaisha kwa 10m ukiwa na 10m peke ake Nyumba haiiishi ng'o.

ukiambiwa nyumba inaisha kwa 20m ukiwa na 20m peke ake hutoboi.

Labda ununue nyumba hapo sawa ila sio ujenge,ujenzi hauna makadirio tunapotezana tu
 
Mie naheshimu sanaa mwenye nyumba yake hata chumba kimoja , shughuli ya ujenzi kwa mtu mwenye kipato cha kuunga unga sio ndogo aiseee
hakuna kipato kikubwa wala kidogo komaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…