Mliokasirishwa kuhusu Rais Samia kutoa msaada Uturuki hii sio awamu ya Magufuli

Uturuki wengi ni muslim zingatia!! Kuna nchi wao majanga ni kilasiku pia chakula,mavazi na makazi ni mtihani na wazee wanateseka mmmno lkn hawasaidiwi!!! Poor studip little leaders...
 
Kwa logic yako basi maskini hawatakiwi kutoa sadaka kwa Mungu bali kila siku wanatakiwa wapewe wao tu! Si ndio?

Acha roho ya kishetani hiyo, roho ya kwanini,roho ya unyimi, roho ya umimi...! Hili ni suala la kiubinadamu, kusaidia wahanga wa maafa mbalimbali! Kitendo cha maskini kumpa hata shilingi elfu kumi tajiri aliyepata maafa kinaonesha ni jinsi gani ana moyo safi, moyo wa kiubinadamu, moyo wa kusaidia wengine regardless of their financial status. Unapotoa ndipo unapoongezewa!!!
 
Kuna maskini unaemjua wewe anatoa sadaka; halafu yeye mwenyewe akalala njaa.
 
Kwahiyo tanzania hizo bilioni 2 ilizotoa kuwapa waturuki ndio zimefanya tulale na njaa?? Lini umelala na njaa toka hizo bilioni 2 zilipotolewa?

Ni watu mnaoishi kwenye dunia yenu na kwenye njoozi nzito kuamka amtaki kila kitu kiko sawa; wakati paa lishaanza kuwaka moto.

Huyo ‘Hakan Yavuz’ ndio main troubleshooter wa WB kwenye madeni. Akitia mguu kwenye nchi chances are kuna forensic investigation ya kufa mtu kwenye mapato, economic indicators, sambamba na DeMPA evaluation.

Kwa lugha nyingine akifika huyo bwana wanadhani nchi ina high defaulting chances kwenye kulipa madeni yake.

Sasa kama hali ipo hivyo serikalini na mnaendelea kujipa moyo mpo vizuri kama Ukraine na kichapo cha Russia; wakati sasa hivi imegeuka testing ground ya silaha zake.

Kwa mantiki hiyo sitegemei uone logic ya concerns zangu kwa sababu right or wrong depends on individual moral stance.

Mwenye shibe, awezi jua struggle za mwenye njaa (wewe upo kwenye shibe) so sioni ukielewa how absurd it is kuisaidia nchi tajiri miezi miwili baada ya maafa na kipindi ambacho wako stable tayari. Wakati wewe una wananchi wana wagonjwa ata gharama za matibabu hawawezi.

You people are just very shallow and live in your own little bubbles
 
Nani kakwambia kuwa katika hii miezi miwili wapo stable? Nakufananisha na mtoto pindi anapopewa zawadi na baba yake kisha baadae baba yake huyohuyo akaamua amuombe mwanawe ampe kidogo katika kile alichomgawia then mtoto anakataa kutoa katakata.


Huu ndio mfano wa moyp wako jinsi ulivyo...yaani ukimkuta mtu mwenye vogue amepata ajali barabarani huwezi kusimama kumsaidia kwasababu tu wewe kila siku unatembea kwa miguu. Hao waturuki wanaisaidia sana Tanzania...tembea vijijini uone jinsi gani wamejitolea kuwachimbia visima watanzania ili kutatua adha ya maji.
 
Una majibu mepesi sana.

Dhana ni binadamu wote wanastahili kuheshimiwa sawa.

Uhalisia ni kwamba binadamu wote hawana uwezo sawa.

Sasa ili utimize duties zako (kwa muktadha wa post uliyo quote mwanzo) kuna vitu vya kuzingatia.

Una wajibu wa kutoa sadaka nyumba ya ibada, lakini usifanye hivyo kwa kujilaza wewe njaa au wanaokutegemea. Kwa hivyo kwenye priority ya kipato your basic needs are first; mengine yanafuata.

Sasa unawezaje toa hela ya familia kwa waturuki ambao kwanza wanamudu hayo maafa yao, washavuka hatua za hatari (disasters zina stages of intervention na washatoka kwenye critical stage), na sasa hivi maisha kwao yanaendelea.

Iwapo binadamu wote wanatakiwa kuheshimiwa sawa (heshima maana yake ni kuwa na afya kwa definition za WHO; ni jukumu lako ina tafsiri vipi afya).

Wenye hela yao leo wana hali mbaya za afya kushinda hao waturuki waliopata maafa, kupeleka hela sehemu ambayo ipo imara zaidi; wakati kwako kuna shida hizo na zaidi ni dharau kwa watu wenye shida.

Kwetu kumekucha 👋
 
Hebu ngoja kwanza mkuu, we hadi sasa umenielewa vp?
Nimeelewa kwamba wanaotumia mitandao (Zaidi ya million 10) hawapo MTAANI.

Ila huko MTAANI ndio Kuna watu halisi.

Sasa sijui hao million 10 ikiwemo Mimi tunaishi sayari ipi!!
 
Nimeelewa kwamba wanaotumia mitandao (Zaidi ya million 10) hawapo MTAANI.

Ila huko MTAANI ndio Kuna watu halisi.

Sasa sijui hao million 10 ikiwemo Mimi tunaishi sayari ipi!!
Hukunielewa, nilichosema ni kwamba asilimia kubwa mambo ya mitandaoni hayatoi picha halisi ya huko mitaani na ndio maana kuna vitu vinafanyika mitandaoni tu ila huko mtaani huvikuti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…