Sio tu hujathibitisha Mungu yupo, hujui kuthibitisha ni nini na unaji contradict.
Uwepo wangu hauthibitishi Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo.
Uwepo wangu unathibitisha Mungu huyo hayupo.
Kwa sababu.
1. Mimi nakunya. Waste products ni characteristic ya imperfect system. Mungu huyo muweza yote, mwenye ujuzi wote na upendo wote kwa nini katengeneza watu imperfect wanakunya badala ya watu perfect wasiokunya wala ku waste energy?
2.Mimi naumwa, same thing, Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna magonjwa? Kama lishindwa, ni kweli ana uwezo wote? Kama hakushindwa, ni kweli ana upendo wote?
3. Kwa nini Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mambo kama umasikini, vita majanga ya asili,ujambazi etc yanawezekana? Alishindwa kuumba ulimwengu ambao mambo haya hayawezekani? Kama alishindwa, ana uwezo wote kweli? Kama hakushindwa ila kaamua tu kutuumbia ulimwengu wenye mabaya yote haya, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, je, ni kweli ana upendo wote?
4. Mungu ana uwezo wa kutengeneza jiwe kubwa na zito sana kiasi hata yeye mwenyewe hawezi kulibeba?
Kama anaweza kuumba hilo jiwe, basi hana uwezo wote kwa kuwa hawezi kulibeba hilo jiwe.
Kama hawezi kuumba hilo jiwe, basi hana uwezo wote kwa kuwa hawezi kuumba hilo jiwe.
Mungu wako yupo kweli au ni hadithi tu?
Thibitisha yupo kweli.