mwaka 2002 serikali ilwanyima mikopo wanafunzi 603 waliochaguliwa udsm. Wale wanafunzi waliripoti chuoni na kuungana kudai haki ya kukopeshwa. Baada ya shinikizo kubwa wanafunzi wote walikopeshwa/dhaminiwa na serikali. Asiwadanganye mtu. Si kweli kuwa serikali haina pesa bali haijui vipaumbele. Kama inaweza kuawapeleka maelfu jeshini na kuwahudumia kwa kila kitu bila mkopo itakuwaje leo iseme haina pesa? Kama inaweza kutenga mamilioni kwa ajili ya kukimbiza na kuzima mwenge, itakuwaje isiwe na pesa za kukopesha wanafunzi? Ni lini mlisikia rais ameahirisha ziara zake za kuizunguka dunia kwasababu serikali haina pesa? Ni lini mlisikia wabunge wamekosa posho zao kwakuwa serikali haina pesa?mmeambiwa waziri mkuu analipwa milioni 26 na rais milioni 32 kila mwezi. Ni lini mlisikia serikali imeshindwa kuwalipa? Ukweli ni kuwa serikali ina pesa za kukopesha wanafunzi wote waliodahiliwa lakini inaelekeza pesa kwenye mambo yasiyo na msingi. Uanganeni mdai haki zenu kwani hizo ni pesa wanazokamuliwa masikini wa nchi hii. Kama pesa hakuna, waliwapeleka jeshini kufanya nini? Muda mliokaa jeshini si mngekuwa mmewasaidia wazazi kutafuta pesa za kujigharimia? Sasa hivi wamewaita wengine tena jeshini, hizo pesa zintoka wapi?! Solidarity for ever?