Mliokutana na mauzauza katika ujenzi wa nyumba, naomba msaada wa hatua mlizochukua

Ndugu yangu mleta uzi

Usipoteze muda wako wala pesa zako kwa kwenda sijui kwa wazee wa hilo eneo wala kwenda kwa waganga.

Usimtegee binadamu hata kidogo ndg yangu watakuongezea matatizo na wataishia kukugombanisha na majirani utawachukia watu kwa sababu ya maneno watakayokwambia. Maana utaanza kuambiwa mara fulani mchawi

Ishi peace na majirani zako

Ukiona chochote kwenye nyumba yako cha kishirikina kichome moto

Mtegemee Mungu tu

Watafanya mauzauza yao yote baadaye watachoka
 
Ok noted luckyline
 
Asante
 
Tanzania kuna vituko sana unaweza kununua kiwanja eneo fulani halafu utasikia watu/mtu anakwambia hili eneo kuna watu wanawafanya wenzao wawe wazito kujenga

Wanaweza hata kuanza kukuonyesha viwanja vingine ukaambiwa huyu mwaka wa kumi huu hata kusafisha eneo lake hakumbuki

Utasikia huyu naye kaleta tofali hizi mwaka wa tatu hata chumba kimemshinda

🤣🤣🤣
 
Mkuu ushawahi kufanya hivyo?
 
Vip hao mbwa usiku uliwaachia nje
Ni lazima kuwaachia, kwenye mji wangu ukiingia bila kufuata protocol kuanzia saa 4 usiku mpaka saa 12 hakuna rangi utaacha ona. Hata hao walozi watafanya mambo yao nje ya gate la himaya yangu na sio ndani.
 
Okoka ili Yesu awe Bwana na Mwokozi wako. Hayo yote yatakwisha
 
Wanakutisha tu hao wapuuzi,chukua CHUMVI ya mawe nyingi kiasi ifunge kwenye nguo nyeusi izike kwenye kona zote na katikati ya eneo,kabla ujaanza kujenga,CHUMVI hiyo utaisomea zaburi ya 91 Mara 9,kabla ya kuweka.
 
Tangia nianze kujenga hadi namaliza sijawai kukutana na upuuzi wa aina yeyote ,niliwaambia mafundi hapa hata wafukie kichwa cha mtu nitajenga hadi mwisho ,ukiona nimesimama basi ujue sina pesa ya kujenga lakini nikiwa nayo wachawi hata wafukie ngombe mzima nitajenga.
 
Ujenzi umechukua muda mrefu mpaka wachawi wameshahamia ivyo wanakutishia.

Dogo wako naye ameshaingia tamaa ukimbie umwachie mji.

Ulivyopata hiyo hela unajua mwenyewe, kama kuna maruweruwe upatikanaji wake uza tu ujipange upya
 
Hapo hamna kitu, ni mapicha picha tu hayo. Tafuta na wewe style yako ya mapicha picha ufanye hapo kwenye eneo lako la ujenzi uone kama kuna jirani yoyote atarudi tena hapo kufanya mauzauza. Tafuta mmbwa koko mmoja mweusi, mpulizie rangi nyekundu upande mmoja, mvalishe shanga nyingi sana alafu mfungie chini ya mti hapo kwenye kiwanja kwa wiki moja alafu baada ya hapo mfungulie azurure hapo mtaani. Hapo utakua umemaliza kazi.
 
Usishangae sana wala usiumize kichwa, ipo siku utakuta hata kondom, mizoga ya mbwa n.k.. hii ni kwa sababu hujahamia bado ni pagale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…