Mliokuwepo wakati 'bana ba cameroon' inatoka naomba uzoefu wenu!

Mliokuwepo wakati 'bana ba cameroon' inatoka naomba uzoefu wenu!

Ndo hivyo!
Sijazaliwa kipindi hicho, lakini haki ya nani huu wimbo huwa sichoki kuusikiliza. Waheshimiwa mliokuwepo kipindi unatoka naomba mnipatie picha tu la vibe Lake lilikuaje maana hiki kibao si cha mchezomchezo!
Sam mwangwana, huo wimbo nina historia nao ndefu sana, kuna Lp ipo home, ina nyimbo tatu, bana bacameron, zimbwabwe na maria tebo
 
Naukumbuka sana nilizoea kusikia mzee wangu akiinjoy nao zamani zile nami nikaupendea pale, imebidi niudownload tena
 
Ndo hivyo!
Sijazaliwa kipindi hicho, lakini haki ya nani huu wimbo huwa sichoki kuusikiliza. Waheshimiwa mliokuwepo kipindi unatoka naomba mnipatie picha tu la vibe Lake lilikuaje maana hiki kibao si cha mchezomchezo!

Hebu attach hilo songi tuliaikilize kwanza
 
Kuna siku moja nikiwa o-level mwanzoni mwa miaka ya 2000 niko home mida kama saa 5 asubuhi, redio one iko ON huku Julius Nyaisanga akiendesha kipindi cha zilipendwa. Nikaona ngoja nibadili station ila nabadili bi mkubwa akaniamuru acha hapohapo usibadili. Nikagundua anasikiliza nyimbo za ujanani mwake. Wimbo uliokuwa ukipigwa ni Nyakokonya wa Les Mangelepa. Ule wimbo ukipigwa leo vijana hawawezi kuelewa kabisa ila kwa enzi za wazazi wetu ndo ilikuwa hit song. 😄
 
Kuna mwamba anaitwa MB Doggy. Huyu jamaa alitoa nyimbo hit na zote zikatamba. Kwa kweli nakumbuka sana his era na kipindi kile mziki ukaporomoka baada ya kuja diamond era. Big up sana MB Doggy. .

Hii kwa ajili ya kizazi kipya😀
 
Ndo hivyo!
Sijazaliwa kipindi hicho, lakini haki ya nani huu wimbo huwa sichoki kuusikiliza. Waheshimiwa mliokuwepo kipindi unatoka naomba mnipatie picha tu la vibe Lake lilikuaje maana hiki kibao si cha mchezomchezo!
Huu wimbo ni hatari tupu...

Kuna wakati nikivurugwa naweza usikiliza week nzima mfululizo.... Unabamba Asubuhi, mchana, alasiri jioni, usiku mpakaa alfajiri.

Napenda kuuacha ujirudie usiku, na nitakuwa nausikiliza ndotoni usiku mzima.

Naweza weka playlist nyimbo 50 zikacheza zote nisizitengenezee ndoto, ila ukipigwa huo lazima niutengenezee ndoto na ukiisha naamka.

The best!
 
Kuna siku moja nikiwa o-level mwanzoni mwa miaka ya 2000 niko home mida kama saa 5 asubuhi, redio one iko ON huku Julius Nyaisanga akiendesha kipindi cha zilipendwa. Nikaona ngoja nibadili station ila nabadili bi mkubwa akaniamuru acha hapohapo usibadili. Nikagundua anasikiliza nyimbo za ujanani mwake. Wimbo uliokuwa ukipigwa ni Nyakokonya wa Les Mangelepa. Ule wimbo ukipigwa leo vijana hawawezi kuelewa kabisa ila kwa enzi za wazazi wetu ndo ilikuwa hit song. 😄
Soki nakufi bandeko..nzela na ngai ya bomoi..
Les mangelepa wanasema ,siku nikifa ndugu zangu njia yangu itakuw na nafuu,ndoa za ujanani zina tabu
 
Ila nyimbo ya Sam Mangwana ambayo nasikiliza tanguy utoto ni Kabibi. Hii nyimbo niliikariri kabisa. Mpaka leo hii ninayo na jana tu nimetoka kuisikiliza. Big up to Mangwana.
Huyu jamaa anazungumza kiswahili,lingala,french nadhani na kereno, ndio maana akawa na uwezo wa kuimba hata hiyo kabibi,pure talent
 
kila wimbo uliotajwa hapa nimeenda kuushusha you tube
 
Back
Top Bottom