Mliomtukana Mwigulu kuhusu tozo mna lipi la kusema?

Mliomtukana Mwigulu kuhusu tozo mna lipi la kusema?

Crimea

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
25,874
Reaction score
36,030
Namnukuu Rais Samia:

"Tozo za miamala tuliweka kwa nia njema, zitaendelea ila tutarekebisha baada ya kilio chenu"

NOTE: Kuna watu walikuwa wanamtukana Mwigulu kuhusu hizi tozo na kusema kuna kundi limemzunguka mama ili kumharibia. Na kama kawaida wajinga walikuwa wanapeleka hizo lawama kwa kile wanachoita sukuma gang.

Unakuta mtu anasema, Samia fukuza watu wa Magufuli, maana ndio wanaokuharibia, na hapa alikuwa analengwa Mwigulu na PM Majaliwasasa unajiuliza yeye Samia si katoka huko huko kwa Magufuli?

Sasa ka-clear kwamba hizo tozo waliweka na yeye akiwemo, haya bado mnaamini kuna kitu kinaitwa sukuma gang ina mharibia mama?

Yote kwa yote, mama anaupiga mwingi!
 
Hakuna kauli ya kiongozi isiyo na mchango wa Rais.

Dharau kwa wananchi na Binge dhaifu.

Rais eti kasikiliza kelele za wananchi,wanapoomba kura huwa hawatumii neno kelele.

KELELE NI NINI
Zina hoja au hazina hoja
Nani ameshinda kwa hoja
Nani hawezi kuongoza ikiwa unatumia kelele.
Tuna safari moja ngumu sana
 
"Tutapitia kuangalia kama kuna penye kasoro turekebishe"

Unajiuliza hawa viongozi wa hii nchi ina maana walikuwa wanatupima imani au?
 
Wewe ulitaka alaumiwe nani? Rais?

Bado lawama zitakuwa palepale kwa Mwigulu maana yeye ndio mshauri Mkuu wa Rais kwenye uchumi.

Hilo wazo lilianzia bungeni hivyo yeye kama Serikali alipaswa atoe sababu za kiuchumi kulikataa-akalipitisha hivyo hivyo pasipo hata kufikiria economic impact yake!

Badaye unampelekea Simba mwenye njaa nyama utadhani ataacha kula-obviously kwa baraza LA Mawaziri lililokosa ubunifu katika uongezeji mapoto lazima lishangilie.
 
Avata yako tosha tu inaonyesha wewe ni sukuma gang na kada mzuri wa ccm
 
"Sukuma gang wanamrubuni mama"🤣

Tuanze kuelewa yule sio 'mamamdogo' wenu ,ni Rais wa nchi,anzeni kumpa scrutiny anayostahili as the occupier of the office of the presidency
 
Hakuna kauli ya kiongozi isiyo na mchango wa Rais.
Dharau kwa wananchi na Binge dhaifu.
Rais eti kasikiliza kelele za wananchi,wanapoomba kura huwa hawatumii neno kelele.
KELELE NI NINI
Zina hoja au hazina hoja
Nani ameshinda kwa hoja
Nani hawezi kuongoza ikiwa unatumia kelele.
Tuna safari moja ngumu sana
JF tuanzishe kampeni ya kumng'oa mama na chama chake.
 
Kwa hiyo kauli ya kuhamia Burundi nayo ina BARAKA za Rais?
 
Tena kasema tulisikia kelele na akasema serikali ni sikivu maana yake watu wangekaa kimya hayo ndoo yaliyokuwa yameamuliwa hawajaangalia vipato vya watu! Kweli mama anaupiga mwingi dhana ya sukuma gang ni dhana ya kitahira kwa watu waliokosa maarifa wao kazi yao tu ni kutukana tu
 
Back
Top Bottom