Mlionunua Magari kwa kuagiza kutoka Japan tafadhali njooni hapa

Kwa upande wangu nawatumia sana Kimomwe Motors Limited. Wanakushauri, unapata nafasi kubwa ya kuchagua gari nzuri sababu wana deal na kampuni nyingi za huko nje. Pia itakusaidia kupata gari kwa bei nafuu, dhamana ya pesa yote wanabeba wao na gari ikipata tatizo bandarini au kwenye meli wanawajibika bila kukuzungusha....wenyewe wana masemo wao kwamba β€œtunampa huduma bora mteja ili atuwezeshe kukua zaidi kwa kuleta wengine na wengine”

Ukifika kwenye ofisi zao utachagua nao gari kwa pamoja, watakufanyia hesabu ya jumla ili ujue bajeti kamili na ndio hiyo itakua kwenye mkataba. Utaonyeshwa CIF kwa uwazi, Ushuru wa TRA, na gharama za Bandari na Clearing. Wao wanapata discount kutoka kwenye kampuni hiyo ya nje watakapochukulia gari yako ambayo ndio wanaiweka kama fedha ya kukubebea dhamana chombo chako mpaka wakukabidhi. Ukipata dharula ya kutotimiza kiasi cha kodi mara nyingi wanakulipia.

Zaidi wapigie kwenye 0746267740 au nenda ofisi zao za Dar es Salaam na Mbeya
 
πŸ™†πŸ½β€β™‚οΈπŸ™†πŸ½β€β™‚οΈπŸ™†πŸ½β€β™‚οΈ
 
Be Forward gari zao mbofumbofu.
Kampuni za kuaminika kupata quality car ni:
Autorec na Japanesevehicles.
Vipi TradeCarView?
 
Sina experience nao. Lakini ukimkuta Clearing Agent mzoefu, atasema kama wapo vizuri. Lakini Autorec ndiyo bora.
 
Sina experience nao. Lakini ukimkuta Clearing Agent mzoefu, atasema kama wapo vizuri. Lakini Autorec ndiyo bora.
Ni kweli hata mimi nimesikia sifa zao ila upungufu wao ni kuwa hawana magari mengi ya kuchagua. Hao TradeCarView wana magari mengi sana, kila brand na kila model.
 
Hao wote na wenzao kina kct na wengine ndio wezi na wazee wa janja janja...wazee wa kudanganya hadi kilomita

Una hoja ya kitoto sana ndugu. Unawezaje kusema ni wezi bila maelezo ya kutosha. Binafsi nimewatumia Kimomwe Motors sana, ingekua ni wezi wasingeweza kusomga mbele kwa kasi ambayo wako nayo.

Hapo kwenye kilomita ndio panaonesha ulivyo sifuri kichwani mwako. Mfano Huyo kimomwe anawezaje kudanganya kilomita ambazo ziko wazi kwa huyo muuzaji wa Japan. Hizi kampuni zimeanzishwa ili kumpunguzia adha mwananchi mwenye majukumu mengi na wakati huo huo kumpunguzia risk maana wanakufanyia process zote.
 
Mzee nahisi una ka mgao kako... Angalia gari zinazopostiwa na hao wadau wako halafu nenda kwenye website zinazouza hizo gari ndio utajua kama hoja za kitoto au ww kamishen ndio zinakutoa akili
 
Ni kweli hata mimi nimesikia sifa zao ila upungufu wao ni kuwa hawana magari mengi ya kuchagua. Hao TradeCarView wana magari mengi sana, kila brand na kila model.
Ila sijui ni madalali wa mtandaoni, maana gari zao naona wanatoa kwenye web kama be foward, enhance yani mchanganyiko na bei zao huwa juu kiasi kulinganisha na kule walipoitia hiyo gari... Fuatilia utaona gari zao ni zile zile zilizopo kwenye web nyingne
 
Si vibaya Synthesizer kama utatoa uzoefu wako kwa faida yetu, swali lake limebase sana kwenye mazoea yetu watanzania walio wengi kuwa magari tunaagiza kutoka Japan. Unaweza kuwafungua macho watu wengi ili tuondokane na mazoea. Tafadhali mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…