Mlionunua Magari kwa kuagiza kutoka Japan tafadhali njooni hapa

Mlionunua Magari kwa kuagiza kutoka Japan tafadhali njooni hapa

Mkuu kwani wewe unachotaka kujulishwa ni namna ya kuagiza gari toka nje na kuli-clear bandarini, au kuagiza gari toka Japan na kuli-clear?

Kwa namna ya swali lako, mimi niliagiza gari toka Singapore kwa bei poa na kuli-clear kiulaini kabisa, lakini kwa kuwa unataka wale walioagiza toka Japan basi siwezi kukusaidia
 
1.Chagua gari mtandaoni
2.Beforward.jp
Watakuletea invoice
3.Peleka benki yoyote ya biashara,mie natumia Diamond trust,utalipa na ya kutuma kwa pesa za kitanzania
4.Benki watakupa confirmation kwamba pesa imeshaingizwa kwenye akaunti ya muuza gari
5.Itume hiyo confirmation kwa email kwa muuza gari
6.Muuza gari atakuletea confitmation kwamba amepokea pesa yako,na siku fulani atapandisha gari melini
7.Baada ya kupandisha gari melini utaletewa sampuli ya shipping documents ili uweze kuhakiki majina na anuani
8.Ukishahakiki utamruhusu atume shipping documets,aidha zije kwako moja kwa moja au zifikie kwenye ofisi yao
9.Ukishapokea shipping documents,utampa wakala wa forodha aanze mchakato wa kulitoa gari,unaweza lipia kodi kabla gari halijafika,ili likifika tu ulitoe ndani ya saa 24

NB maelezo hayo ni kutokana na uzoefu niliopata kwa Beforward
 
Mkuu kwani wewe unachotaka kujulishwa ni namna ya kuagiza gari toka nje na kuli-clear bandarini, au kuagiza gari toka Japan na kuli-clear?

Kwa namna ya swali lako, mimi niliagiza gari toka Singapore kwa bei poa na kuli-clear kiulaini kabisa, lakini kwa kuwa unataka wale walioagiza toka Japan basi siwezi kukusaidia
Singapore kuna gar kali sana
 
Habari za jioni ndugu zangu,

Naomba uzoefu kwa nyie mliojaliwa kupata magari kwa kuyaagiza toka Japani hasa yale ya mtumba mlifanyaje fanyaje mpaka mzigo ukawafikia? Pale Bandarini mzigo ulitokaje?

Naomba wenye uzoefu na haya mambo mnijuze tafadhari.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tumia wakala kama Befoward, itakupunguzia usumbufu
1. Unakuwa na akaunti kwenye mtandao wa Befoward
2. Unachagua gari ulilopenda
3. Unawasiliana na staff wa Befoward akuangalizie "mechanical report" na kukushauri mfano magari mengi yana mwonekano mzuri lakini yana oil linkage au dashboard ina ufa; hawa watakushauri.
4. Watakupa akaunti ukalipie plus kama u$ 100 bank charges za wao kutuma hiyo pesa yako.
5. Kama uko mkoani, utalipa kiasi fulani gari utaletewa mpaka ofisini kwa Befoward.
6. Gari ikifika au ikikaribia kufika watafuatilia hesabu za kodi na bima; kwa upande wa kodi utalipa moja kwa moja TRA
7. Bima italipwa kabla ya gari kutoka bandarini.

Hivyo ndivyo nilivyofanya. Ushauri ni muhimu kuna magari mengi yana muonekano mzuri wewe ukililipia bila kupitia ofisi ya wakala utanunua kitu kibovu ila wao "internally" wana "mechanical report" ya kila gari lililo sokoni. Kuna ushauri mwingine mfano kwenye ukubwa wa injini kama unanunu PRADO kuna cc 4600 na kuna la cc 3000 wao watakushauri ununue la cc 3000 ili ukitaka kuliuza liuzike tofauti na cc 4600
 
Wewe ni mmoja wa hao wezi. Kutuma hela ni dollar 59 bank wewe unasema 100

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi siyo mwizi ila nimewahi kuwa mteja wa Befoward. Kutuma pesa kweli ni US$ 59; nani anatuma? Huyo anayetuma hana gharama? Huo mtandao wa internet haulipiwi? Kupitia ofisi ya Befoward nilipata "Discount" sijui kama ukaigiza peke yako ipo; Befoward walinifanyia "clearance" sasa mtu aliyeko Mwanza aanze usumbufu wa kutafuta Clearing agent Dar wakati yuko Mwanza nao ni mkwamo fulani.

Kuhitimisha kila panapokuwepo mtu wa kati kuna gharama itaongezeka kwa huduma atakayokupa NO FREE LUNCH.
 
Back
Top Bottom