Mliooa na mnaopata mshahara wa Tshs. 300,000 au chini ya hapo mnawezaje kumudu familia?

Mliooa na mnaopata mshahara wa Tshs. 300,000 au chini ya hapo mnawezaje kumudu familia?

tusidanga nyane humu wengi wanao sema nipesa nyingi utakuta wanapata zaidi ya hiyo Pesa kiukweli kama unafamilia unapata iyo Pesa kichwa lazima kiume
 
Subiri waje wanaopataga hizo 300,000/= kwa.Ila pia wamejenga na wanatumia magari yao binafsi kuja ofisin na kila siku mafuta ya 15,000.pia mchana lunch yao si chini ya 10,000.Pia kila jioni wanasimamisha magari yao daily pale kipawa kununua samaki wabichi wa angalau 5,000-10,000 kwa ajili ya nyumbani usiku na matunda pale Goms ya 2,000 na zaidi.Pia pleadge zao za michango ya kila send off na harusi pia watoto wao pia wanasoma pale pale Tusiime,Heritage,Atlas ,canosa etc
hii ni miujiza mkuu[emoji23][emoji23] (watu wanatembelea miujiza)
 
Angalizo usioe kama ujajipanga ipasavyo tatizo vijana mukielezwa mapema munajifanya wajuaji...ungesubiri upate iyo kazi ya 300K kwanza usevu uwekeze sehemu hata 2..3 iongezeke kwa mwezi iwe hata 800K ndio uoe.

NB: maisha yanapangwa kabla ya kuoa ukishaoa ngumu sana.
 
Aise laki tatu unaiona ndogo usawa huu wa magu wakati hapa mimi take home ni laki na nusu na inatosha mimi na familia yangu na chenji inabaki
Mkuu hii uliyoandika sidhani kama ni kweli. Makazi vipi unapanga au ulishajenga au walao kuridhi nyumba? Japo inategemea pia mtu anaishi wapi? Kwa maana ya kijijini au mjini lakini hata tukiacha hiyo laki1.5 uliyosema, laki3 ya mleta mada nayo ni ndogo sana kusema ukweli.

Yaani hiyo laki3 upange nyumba, ulishe familia, usafiri (daladala+bodaboda), nk. Tuombe mtu kwenye familia asiumwe lakini uwape watoto daftari, nauli shule, nk kwa laki3 kwa kweli ningumu ndiyo maana kwa mjini wengi wanaangaika pembezoni mwa ajira zao ili walao maisha yaendelee hasa hasa kupata pa kulala na kwenda chooni si mchezo sembe lenyewe linapanda bei kila leo!!

Kama hayo uliyosema ni kweli basi mimi labda nitakuwa na chuma ulete, ananivuna maana nikijipima sina matumizi mabaya lakini kwa kafamilia kangu haka ka watu 6 kwa kweli laki1 huwa haitoshi hata wiki1 hata nijibane vipi! Hapo bado sijahesabu makazi na mengineyo kama kula kazini, na kuwezeshwa kwa watoto kwenda na kurudi shule.

Bado michango ya kiimani kama sadaka, zaka, mavuno, fungu la kumi, nk. Aisee laki3 sijui...
 
Huu ndio uzi unaotakiwa watu wamechangia kwa kuongea ukweli kabisa kutokana na uzoefu wao, Kwa maeneo ya vijijini ukijibana 300,000/- inatosha kibishi hivyohivyo.
 
Baada ya makato na kubakia 300,000 una mke na watoto, unawezaje kumudu familia kwa huo mshahara?

Tupeane uzoefu.
Kwanza hongera kwa mshahara.
Wewe na mwenza wako yawapasa mtambue kipato chenu ni 300,000/.
Kisha waweza fanya haya:
1. Watoto wasome shule za kawaida za serikali mfuatilie tu maendeleo yao kwa karibu.
2. Upatapo mshahara andika mahitaji makuu ya chakula mfano: mafuta lita 5 20,000, mchele kg 15 kwa 30,000/ unga kg 20 kwa 20,000, dagaa za 6000/ choroko/ njegere 6000/ sukari+ chumvi 11,000/ sabuni 6000/ mafuta ya kujipaka nunua vikopo 2 cha watoto 2000 na wazazi 3000/ .
3.Weka bajeti ya mboga mboga na matunda 60,000 kwa mwezi yaani 2000@day.
4. Mahitaji ya watoto kama wanasoma nunua kwa vipindi mfano: mwezi huu wanunulie soksi, nguo za ndani na daftari(bei ya jumla ili vikae muda na unafuu), mwezi mwingine unawanunulia kingine.

N:B kwa kuanzia umizeni akili mtafute mtaji wa laki 1 muanzishe biashara ndogo itakayoweza kuwapatia japo 2000 tu kwa siku kisha mtaendelea.
 
Unga kilo 15 sh 15,000,Mchele kilo 20 sh 40,000,mafuta ya kula Lita 5 sh 20,000 gesi sh 20,000, mkaa gunia Dogo sh 20,000,Maharage kilo 10 sh 20,000 jumla sh 135,000/= Umeme 10,000 ,Maji 10,000 MPE wife 50,000 wewe weka 100,000 mwezi unakatika bila presha
 
Tudeal twa kazini tulikuwa tunatubeba sasa jpm kabana.
 
Take home yangu ni 229,000/ but Nina nyumba japo ya kawaida tu,mke na watoto wanakula na nyumbani kwa wazazi natoa huduma,hii kitu ni mipango tu mkuu,huwezi amini huwa nasevu na akaunti yangu haipungui million kwa tahadhari
Natamani nipate elimu mkuu jinsi gani wewe unaweza daaa.
 
Na ukizingatia na nyumba zenyewe za kupanga kwa waswahili machuma ulete kibao
Watu hawana mshahara kabisa.... MTU amekopa hadi salary slip inamdai na anaishi..

Kifupi unaishi Kwa taabu sana.

Hiyo laki tatu wadau hapo juu wanasema upunguze vitu visivyo vya lazima. Em wavitaje!?

Hela ndogo sana hiyo..
 
Back
Top Bottom