Opportunity Cost
JF-Expert Member
- Dec 10, 2020
- 9,034
- 6,913
Lusajo yuko Namungo fcWadau wa mechi umofia.
Nimeambiwa Taifa Stars 1 na DRC 1,ila somebody Lilayanti Lusajo yuko powa Sana sijui anachezea timu gani,ametoa pasi ya goli.
Kila la heri Taifa Stars
Kimsingi uimara wa ligi ya ndani umeimarisha wachezaji wetu.FT.
Congo Drc 1- 1 Tanzani
Mashindano yamekaaje ? Kundi letu Lina timu gan? Hii game ya ngapi kucheza?Kimsingi uimara wa ligi ya ndani umeimarisha wachezaji wetu.
Kama ligi itaendelea hivi by 2025 tutakuwa juu Sana maana na mwaka huu kuna mpunga wa Azam battle itakuwa ya kutosha.
Hongera Taifa Stars kwa sare ila nyumbani tuchezage Jihad Ili asitoke mtu.
Hii ni mechi ya kwanza katika kundi letu.Mashindano yamekaaje ? Kundi letu Lina timu gan? Hii game ya ngapi kucheza?
Mzamiru ni mchezaji mhimu sana, asingekuwepo hapo kati ingekuwa shida.Mzamiru hajui kabisa
Anarudisha pasi nyuma tu kila mara
Kundi la vibonde! Kati ya hizi timu 4! Tanzania, DRC, Benin na Madagascar! Hakuna timu ya kwenda huko Qatar! Na ikitokea, basi itaenda kubugizwa goli za kutosha kweli kweli na wenye mpira wao.Mashindano yamekaaje ? Kundi letu Lina timu gan? Hii game ya ngapi kucheza?
Taifa Stars ikomae tuu hasa hizi mechi za homeHii ni mechi ya kwanza katika kundi letu.
Kundi letu tuna timu za:
1.Madagascar
2.Benin
3.Dr Congo
4.Tanzania.
Madagascar watatusumbua,kuna wakati waliwapiga vigogo wa Afrika kwa kuwatumia wachezaji wa kawaida wanaocheza ulaya madaraja ya kawaida.
TFF ijifunze kwa Madagascar kuwafuatilia wachezaji wa kitanzania walio na umri mdogo na wanafanya vizuri huko nje katika ligi za kawaida waitwe ili walete ushindani ndani ya kikosi na wazoe kucheza timu ya Taifa.Wachezaji wa ndani wakati mwingine wanajisahau kujibidisha mchezoni.
Mfano sijawahi kumsikia yule mchezaji kijana Oscar Mkomola na wengineo wengi kuna wakati walikuwa timu ya vijana iliyoenda Gabon na walifika nusu fainali kama sijakosea.
Kundi gani halina vibonde?Kundi la vibonde! Kati ya hizi timu 4! Tanzania, DRC, Benin na Madagascar! Hakuna timu ya kwenda huko Qatar! Na ikitokea, basi itaenda kubugizwa goli za kutosha kweli kweli na wenye mpira wao.
Hakuna! Ila hili halina hata bingwa mmoja, au yule wa kumtabiria kufuzu. Yeyote atakayepita hapa, ataishia kwenye 10 bora.Kundi gani halina vibonde?