Mliopo Uwanjani tupeni matokeo ya Taifa Stars Vs DRC

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2020
Posts
9,034
Reaction score
6,913
Wadau wa mechi umofia.

Nimeambiwa Taifa Stars 1 na DRC 1,ila somebody Lilayanti Lusajo yuko powa Sana sijui anachezea timu gani,ametoa pasi ya goli.

Kila la heri Taifa Stars
 
Taifa starts hamna kitu kila saa tupo tuna hemewa langoni ni butua butua tu
 
Huyu kibabage nae hovyo, hakuna cha maana anachokifanya
 
Kimsingi uimara wa ligi ya ndani umeimarisha wachezaji wetu.

Kama ligi itaendelea hivi by 2025 tutakuwa juu Sana maana na mwaka huu kuna mpunga wa Azam battle itakuwa ya kutosha.

Hongera Taifa Stars kwa sare ila nyumbani tuchezage Jihad Ili asitoke mtu.
Mashindano yamekaaje ? Kundi letu Lina timu gan? Hii game ya ngapi kucheza?
 
Hii ni mechi ya kwanza katika kundi letu.
Kundi letu tuna timu za:
1.Madagascar
2.Benin
3.Dr Congo
4.Tanzania.
Madagascar watatusumbua,kuna wakati waliwapiga vigogo wa Afrika kwa kuwatumia wachezaji wa kawaida wanaocheza ulaya madaraja ya kawaida.

TFF ijifunze kwa Madagascar kuwafuatilia wachezaji wa kitanzania walio na umri mdogo na wanafanya vizuri huko nje katika ligi za kawaida waitwe ili walete ushindani ndani ya kikosi na wazoe kucheza timu ya Taifa.Wachezaji wa ndani wakati mwingine wanajisahau kujibidisha mchezoni.

Mfano sijawahi kumsikia yule mchezaji kijana Oscar Mkomola na wengineo wengi kuna wakati walikuwa timu ya vijana iliyoenda Gabon na walifika nusu fainali kama sijakosea.
 
Kundi la vibonde! Kati ya hizi timu 4! Tanzania, DRC, Benin na Madagascar! Hakuna timu ya kwenda huko Qatar! Na ikitokea, basi itaenda kubugizwa goli za kutosha kweli kweli na wenye mpira wao.
 
Taifa Stars ikomae tuu hasa hizi mechi za home
 
Kundi la vibonde! Kati ya hizi timu 4! Tanzania, DRC, Benin na Madagascar! Hakuna timu ya kwenda huko Qatar! Na ikitokea, basi itaenda kubugizwa goli za kutosha kweli kweli na wenye mpira wao.
Kundi gani halina vibonde?
 
Back
Top Bottom