Mliopona maumivu ya mgongo, kiuno, na viungo mlitumia dawa gani?

Mm nilipata hilo tatizo kwa muda mrefu sana hadi nikakata tamaa,nikajiongeza kwa kubadili lifestyle hadi sasa limekwisha kabisa.Nimenunua baiskeli kwa ajili ya mazoezi,napumzika muda wa kutosha lkn nimeachana na vyakula vya sukari na wanga napiga matunda na maji ya kutosha
 
Acheni kulala magodoro Sio sifa lalieni vislesi vya godoro,mbao au mpira
 
Kwa waliofanya kazi za kukesha miaka mfano madereva walinzi madaktari ni watumie dawa gani ili kurejesha mwili urudi sawa kwenye mpangilio wake maana tatizo kubwa ni ukosefu wa usingizi baada ya kuacha kazi hizo
 

Nenda muhimbili pale MoI wameleta treatment kwa ajili yenu kwa gharama ndogo tu ya million moja wahi nafasi ni chache
 
Nakutumia na bei yake kabisa ili ujipime usimtafute daktari kama huna hio hela. Pia kuna sawa nyingine za ku spray na kupaka haziko hapo
 
Fanya mazoezi kula vizur upumzishe mwili wako maumivu yote kwisha
 
Ukiongeza na Physiotherapy itakufaa.

Ukipata Chiropractic sessions utapata nafuu kwa haraka zaidi (ukipata chiropractician anayejua session 3 zitatosha kurejesha kwenye ubora wako).

Kila la heri mkuu
 
Mshauri afanye physiotherapy pia. Itamuimarisha zaidi

Best wishes
 
Mkuu, ndugu yako ameshapona?
 
Mkuu, ndugu yako ameshapona?
Bado ndugu yangu tunajitahidi kutumia dawa kila tunayoambiwa lakini ni kama zinatuliza tu badae tatizo linaanza upya kama kuna solution huko tusaidiane mkuu
 
Lala chini usilale kitandani kwa siku 3 tu lalia mkeka mgogo ukiwa chini
 
Bado ndugu yangu tunajitahidi kutumia dawa kila tunayoambiwa lakini ni kama zinatuliza tu badae tatizo linaanza upya kama kuna solution huko tusaidiane mkuu
Mpatie chai ya alkasusi. Ile ni dawa mujarabu kwa ishu za kiuno na mgongo.

Nilivyojifungua watoto mapacha mwaka huu nilikuwa naumwa Sana kiuno na mgongo. Nikashauriwa nitumie alkasusi. Ndugu wakaninunulia Tanga pakiti sita. Nikawa natumia kama chai yangu asubuhi mchana jioni. Nilipona kabisa. Hadi muda huu nipo fiti, siweki mito na manguo nguo ili kuegemea sehemu yoyote.
 
Kiuno kipone kwa alikasusus pasipo mikando we ulisikia wapi
 
Asante kwa ushauri ndugu shukrani kweli kweli tutajaribu na hiyo pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…