LeopoldByongje
JF-Expert Member
- Apr 28, 2008
- 372
- 13
Katika Kitabu Cha Quar'ani, Mwenyezi Mungu anaposema anatumia wingi onaHakika sisi tutairithi ardhi na walio juu yake. Na kwetu watarejeshwa.19:40. Nasi kwa rehema zetu tukampa nduguye, Harun, awe Nabii. 19:53
Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Mwenyezi Mungu humuacha akapotea amtakaye, na akamwongoa amtakaye. Naye ni Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima 14:4.
Na tulimtuma Musa pamoja na miujiza yetu, tukamwambia: Watoe watu wako kwenye giza uwapeleke kwenye mwangaza. Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu. Hakika katika hayo zipo ishara kwa kila mwenye kusubiri akashukuru 14:5.
Na mtaje Musa katika Kitabu. Hakika yeye alikuwa ni mwenye kuchaguliwa, na alikuwa Mtume, Nabii. 19:51.
Na tulimwita upande wa kulia wa mlima na tukamsogeza kunong'ona naye19:52.
Nasi kwa rehema zetu tukampa nduguye, Harun, awe Nabii"19:53
JE, umewahi kujiuliza ni kwa nini?