Mliosoma mashule ya international hebu mkuje hapa tuwafundishe hizi mambo

Kwahiyo unataka kuwafundisha wa international jinsi ya kukwepa foleni ya chakula?

Au namna ulivyokula makonzi?
 
Ni kweli kwasababu hatutafuniwi.

Hatuna vitabu.

Tunajitafutia.

Mwalimu anakuapia lazima ufeli.

Darasa unalofanyia mtihani watu wanat01mbania.

Walimu hawajielewi.

4 ya 28 ya kata ni strong kuliko ya private.
Acha kujifariji mkuu div four ni ile ile uwe private au government. ...
Na nani kakwambia shule zote za private wanatafuniwa..kikubwa kwa mwanafunzi ni discipline anajiwekea kwenye masomo na akili yake..
Kwahio ujinga wa wanafunzi ndio sababu ya kufeli
 
Ndio tatizo letu..yaani watu wanaona uhuni na kuvunja sheria kama ndio ujanja..
wakati wenzao wana memories za ushindi wa debate na shule nyingine , ushindi wa ligi za inter school n.k
Shule za kata zina matatizo mengi sana ukiwa private hata mwalimu anakuheshim sasa Shule za Gvt Mwalimu ana stress ikizangia na wewe ndio ngeli imekaa kushoto na haumuelewi kabisa atakupiga akuue kabisa
 
Kwani nani hajui kama nyinyi mnatafuniwa?

Mimi nipo kidato cha tatu mwalimu aligoma kutufundisha mwaka mzima tunaingia kidato cha nne mwalimu wa kidato cha nne anasema kuna vitu sitafundisha mlijifunza kidato cha tatu.

Nyiye mayai si mngeandamana?
 
Siku za wali nlikuwa naenda kwenye foleni saa 7 badala ya nane nikiwa na kile kisado cha lita 3 ili punga lionekane chache mgawaji apate moyo wa kuongeza kidogo..
[emoji1] [emoji1]
Siku zinaenda aiseeh!
Haa haa haa haa aiseee tutamis sana hiz zama
 
Hii ya kukaanga dagaa imenikumbusha wakati nipo olevo.
 
Kwani nani hajui kama nyinyi mnatafuniwa?

Mimi nipo kidato cha tatu mwalimu aligoma kutufundisha mwaka mzima tunaingia kidato cha nne mwalimu wa kidato cha nne anasema kuna vitu sitafundisha mlijifunza kidato cha tatu.

Nyiye mayai si mngeandamana?
Advance nimesoma private nimepewa vitabu shuleni , walimu walikua ni wa shida , tulikua hatuna ruhusa za kwenda mjini kupiga mapindi tution kama wanafunzi wa government, usiku tulikua haturuhusiwi kutoboa mwisho kusoma ilikua ni saa nne na dk 45 baada ya hapo taa zinazimwa. Tulichopewa ilikua ni vitabu vya kutosha tu

Lakini kwa discipline tuliyokua nayo darasa langu la pcb waliopata div 3 walikua wachache wengi ilikua ni div 1 na 2... nenda kaangalie wale wa government waliokua na 24hrs ya kujisomea na uhuru wa kwenda town kusoma tution wengi walipata ngapi?
 
Dhaaaaaaaa aiseeee
I wish miaka irud nyuma nirud
Zang kwalamahondo primary kusoma
Na kuiba msos wa waalimu
 
Kwani nani hajui kama nyinyi mnatafuniwa?

Mimi nipo kidato cha tatu mwalimu aligoma kutufundisha mwaka mzima tunaingia kidato cha nne mwalimu wa kidato cha nne anasema kuna vitu sitafundisha mlijifunza kidato cha tatu.

Nyiye mayai si mngeandamana?
Unadhani ni sifa kusoma bila kufundishwa na mwalimu ?
 
Hapo waombaji sasa...wa kujibeatisha[emoji1] [emoji1]
 
Long t sana niliwai mwaga ndoo ya nyama kisa utata wa kuongezewa nyama kilichofua mbio ziliniokoa.Watoto wa day hawajui iz
 
Hapo waombaji sasa...wa kujibeatisha[emoji1] [emoji1]



Acha kabisa waombaji hawakosiiii.. Nami siku nikidorora natolea jicho kwa wenzangu lol Yani jumapili nikitoroka siku nzima sili chakula cha shule hahahahaha.......boarding gvt schools bana


Cc Smart911
 
Shule za bweni za serikali zimetufundisha sana maisha. nakumbuka nimeenda kidato cha 5 siku ya kwanza ugali maharage ule ugali ulinishinda kabisa kwanza nilishangaa tunakula ugali na kijiko ugali ukiukata na kijiko unakatika kama vile unakata biscuit haibaki hata chembe kwenye kijiko. Nilipouweka mdomoni hivi nilihisi wamepikia mahindi ya kutengenezea pombe komoni. Baadae nilikuja uzoea nikawa mpaka narudia. Mboga za majani za kuuzwa kijiko kimoja sh 50 zilionekana kama Almasi wakati nyumbani siku mama akipika ugali na mboga za majani pekee bila mboga zingine nilikua nachukia kweli
 
Hii inanikumbusha mlokole mmoja karudi na pilau kwenye tranca na cake ya besiday mida watu wanaenda prepo watu tuka piga u-turn aliporudi alikuta bonge la nguna!
 
Nakumbuka kuna siku litambara lilipatikana kwenye sufuria la maharage muda wa kugawa chakula jioni...watu wakavumisha eti "mchupi" wa mpishi umekutwa kwenye maharage..
Tuliokuwa tunaelekea kumaliza kula sasa tukaanza kila mmoja na reaction yake...
Wa kujitapisha, wa kufyonza, yaani ikawa balaa tupu..
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nilikuwa naoga siku ya wali au nyama ndio mtaniona bafuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…