Mliowahi kuagiza bidhaa kutoka Marekani kwa kutumia kampuni ya Myus

Mliowahi kuagiza bidhaa kutoka Marekani kwa kutumia kampuni ya Myus

Elon Mzebuluni

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2016
Posts
225
Reaction score
139
Habari wakuu. Poleni na majukumu.

Ni mara ya tatu Naagiza bidhaa mbalimbali kutoka ebay kupitia kampuni ya myus. Mara mbili nimepokea bidhaa nilizoagiza bila changamoto yeyote. Mara hii ya tatu bidhaa inaonekana imefika dar es salaam na inaleta meseji ya Clearance delay- import.
Clearance instructions from the importer are required. Importer must provide instructions.

Nimeambatanisha na picha hapo.

Je mliowahi kumbana na hii changamoto mlitatua vipi maana nimekwama sielewi cha kufanya.

Asante.
Screenshot_20221019-055749_Chrome.jpg

Screenshot_20221019-090949_FedEx.jpg
 
inaleta meseji ya Clearance delay- import.
Clearance instructions from the importer are required. Importer must provide instructions.

Nimeambatanisha na picha hapo.
Ni swala la
  • Clearance
  • Malipo ya tozo [ VAT / TAX ]
Nini cha kufanya
- Piga simu kwa kampuni iliyohuiska kukusafirishia, wape tracking number na watakupa mwongozo hatua kwa hatua, utalipia ghrama zote zinazopaswa kulipia.
 
Myus walitumia fedex kusafirisha bidhaa kuja TZ so inabidi niwasiliane na hao fedex?
 
Myus walitumia fedex kusafirisha bidhaa kuja TZ so inabidi niwasiliane na hao fedex?
Sahihi, FEDEX ndio watashughulika na taratibu zote za clearance, hadi mzigo wako unakuwa tayari kwa kuchukuliwa.
- Google "Customer Support | FedEx Tanzania" chukua namba kisha wapigie.
 
Kikuu wako poa sana, toka mzigo wangu wa aliexpress upotee kimasihara, nimeweka kambi kikuu.
Nashangaa hakuna kampuni la marekani linalowafikia....Au wanadharau soko la Africa?
China soon atakuwa superpower
 
Sahihi, FEDEX ndio watashughulika na taratibu zote za clearance, hadi mzigo wako unakuwa tayari kwa kuchukuliwa.
- Google "Customer Support | FedEx Tanzania" chukua namba kisha wapigie.
Asante sana mkuu, ngoja nifuatilie nitaleta mrejesho
 
Ni swala la
  • Clearance
  • Malipo ya tozo [ VAT / TAX ]
Nini cha kufanya
- Piga simu kwa kampuni iliyohuiska kukusafirishia, wape tracking number na watakupa mwongozo hatua kwa hatua, utalipia

Sahihi, FEDEX ndio watashughulika na taratibu zote za clearance, hadi mzigo wako unakuwa tayari kwa kuchukuliwa.
- Google "Customer Support | FedEx Tanzania" chukua namba kisha wapigie.
Mkuu nimefanikiwa kuwapata, je unashauri nitumie hao hao fedex kufanya clearance au nitumie broker mwingine kufanya clearance. Maana wamenipa options wao au wengine.
 
je unashauri nitumie hao hao fedex kufanya clearance au nitumie broker mwingine
Hapo utakuwa hujatatua tatizo la gharama.

-Ukisema kazi iende kwa agent mwingine, ili kutoa Documents za mzigo inatakiwa ulipe Document fee ambayo wao hutoza ni TZS 88,000,
-na baada ya kupa document ukienda kwa vlearng agent mwingine naye atahitaji umlipe ili akufanyie kazi. Na huwa sio chini ya 120,000

-Fanya hesabu, utaona ni bora wao wakaendelea na kazi,na ukawalipa hiyo TZs. 150,000 wanayohitaji.

NB | Next time kwa manunuzi ya USA hakikisha unatumia huduma yangu ya BUY4ME | Nunua bidhaa kutoka Mataifa 15 ikiwemo USA, UK, UAE na China sasa
  • Ambapo Agent fee ni TZs. 60,000 tu.
  • Then utalipia zile Tozo za TRA na TBS kama kawaida.
Uwepo wa huduma yangu ya BUY4ME imetatua changamoto yingi sana, ikiwemo hiyo iliyokupata wewe sasa, mimi ilinipata Miaka kadhaa iliyopita na niliandika hapa | Hili Halijapata Ufumbuzi kuhusu Ununuzi wa Vitu kwa Njia ya Mtandao (Online Purchase)
1666185437149.png
 
Back
Top Bottom