Mliowahi kukopa benki na badae kuachana na mikopo na kubaki na mitaji yenu tupeane ujuzi nasi tujikwamue

Duh! Mkuu pole sana.. Very interesting story ingawa hukusema alikopa kiasi gani..
Kwa ujumla mikopo ina kanuni zake.
Kwanza, usikope for biashara mpya unless ni long term.
Pili, usikope kwa kushawishiwa, kopa kama biashara inahitaji hvyo, tena kiasi sahihi, na kuna hesabu zake.
Unaeza kuta mtu ana biashara ya mtaji wa kama m30, biashara inahitaji jeki (working capital) ya 4m, anaenda kuchukua 15m. Maana yake 11m itakuwa idle au itatumiwa kwny mambo tofauti. Deni kama hilo halilipiki kamwe.
Pia, deni ya muda mfupi ikizidi 20% ya mtaji inakuwa kama kamari.
Kingine, usithubutu kuweka dhamana nyumba unayoishi, tumia kiwanja, shamba au nyumba ya ziada. Hii itakuepusha na ugonjwa wa moyo.
Kumbuka pia, kama umeamua kujilipua na mkopo, ni afadhali benki (au Saccos za jumuia kwa mikopo midogo) kuliko ki-microfinance cha mtu.. wanasema kwny hizi micro, mkopeshaji akipenda dhamana uliyoweka ataichukua tu.. Na pia usisahau kuelewa na kujiridhisha na masharti yote ya mkopo kabla ya kujifunga kwny mkataba
 

Uzuri ni kwamba sijawah kukosa bank..Ila nilijiunga manager saccoss ambapo miez miwili ilopita nilikopa milion10.7 kwa ajili ya shughuli zangu..nakatwa taratibu kwenye mshahara kwa miaka3 wala sitaabiki...na bado shares zangu zinazidi kuongezeka.
Nakushauri hamia Saccoss
 
Ongera sana mkuu.

Ila hapa nazungumzia wale risktaker kama sisi
 
Mkuu mm sio kwamba nipo kwenye danger zone kivile!

Ila nataka kupata namna ya kujinasua yaan niachane na mikopo kabisa na nibaki salama bila kuyumba.
 
Unaweza kujinasua Kwa kupunguza kiasi cha mkopo kila unapokopa mpaka ukaja kuacha. Kama nimekuelewa vizuri wewe unaongeza kiasi cha mkopo au unarenew same loan amount kwa hiyo unajikuta in the same vicious cycle
 
Unachosema ni kweli mkuu... Mi nmefanya sana kazi bank, moja ya vitu ni kwamba benki haipendi kukopesha watu wanaoenda kuomba mkopo bali watu ambao benki inawafuata kuwaomba wakope. Na hao mara nyingi wanakua hawajaplan juu ya mkopo vizuri na inaweza kuwa mwanzo wa kuanguka kama ilivyokua kwa mzee wako
 
Shida nafikiria sio kutorudia shida ni nini unataka je baada ya mkopo kuisha mtaji wako umekua? Kama ndio ni kwa kiwango inachotaka? Kama ndio then naamin hautokopa tena.
Shida ni kwamba hatujui ukomo wetu
 
Hili suala la mkopo ni balaa nmemaliza mkopo wangu wa benki mwezi July tu nlikopa stanbic then mkopo nkauza NBC mwaka 2014. Nimeapa sitokopa tena Bank kwa sasa nmebakiza mkopo wa kazini nao unaisha January.
 
Hili suala la mkopo ni balaa nmemaliza mkopo wangu wa benki mwezi July tu nlikopa stanbic then mkopo nkauza NBC mwaka 2014. Nimeapa sitokopa tena Bank kwa sasa nmebakiza mkopo wa kazini nao unaisha January.
Mikopo ni zaidi ya adui wa maisha
 
Shida nafikiria sio kutorudia shida ni nini unataka je baada ya mkopo kuisha mtaji wako umekua? Kama ndio ni kwa kiwango inachotaka? Kama ndio then naamin hautokopa tena.
Shida ni kwamba hatujui ukomo wetu
Mkuu ukitaka mtaji ukue basi usifanye swala lolote la kimaendeleo.

Wengi tunakopa ili tuweze kupata tulivyoshindwa kuvipata kabla.
 
Point!
 

Huyu Mzee kama namfahamu hivi,Sio Bwana Getano kweli huyu?

Back in 2005 hii story ya kuzawadiwa na CRDB ilitrend sana kule home Lake Zone n I think ni Getano ndo alipewa hiyo zawadi

Nina washkaji zangu huyu Getano ni Uncle yao n I know them deep down sema sikuwahi kujua kama Yule mzee alifilisika back then
 
Kuna mtu aliniambia siku ile unapeleka hati ya nyumba yako benki kama dhamana, ndiyo mwisho wa kuiona hiyo hati huwa haitoki benki .
Hakuna hata tajiri mmoja aliyeweza kutoa hati yake benki na kuirudisha nyumbani . Unakopa kuongeza mtaji lkni mwishowe hata mtaji wako uliokuwa nao utapotea.
Cha muhimu ukiona unaomba kufanyiwa topup ujue biashara yako imeisha ni kusubiria mnanda.
 
Aisrr aisee mbona hatari sana.
 
Hapo kwa binamu&ndugu umenigusa
 
Aisrr aisee mbona hatari sana.
Huu ni ukweli mchungu kabisa
 
Naomba mnipe ufafanuzi zaidi wajuzi,,, nimekopa benk flani nimelipa mkopo wangu kwa asilimia 70% Biashara imeyumba kidogo na nimewandikia barua kuwa mzunguko umekuwa mdogo je hili linaweza kuniletea shida? Kama kuuza dhamani nk?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…