Mliowahi kukopa benki na badae kuachana na mikopo na kubaki na mitaji yenu tupeane ujuzi nasi tujikwamue

Sasa unajikanyaga mbona umesema africa inadhani kupoka ni solve ttzo tena una sema mataifa yana kopa yana acha madeni niku elewe vp
 
Auze Asset yake kama vile shamba au mifugo.
mkuu una low IQ sana sasa mtu anatoa wapi hizo assets wkt ndo ana anza biashara na kma anazo hizo asset kazipata kwa biashara tena aziuze kuongeza mtaji alipozitata? atakua ana fanya monkey bussiness
 
Sasa unajikanyaga mbona umesema africa inadhani kupoka ni solve ttzo tena una sema mataifa yana kopa yana acha madeni niku elewe vp
Unielewe hivi hayo madeni hayatakaa yalipwe, na pia hayaleti maendeleo, bali yanaleta utegemezi.
 
mkuu una low IQ sana sasa mtu anatoa wapi hizo assets wkt ndo ana anza biashara na kma anazo hizo asset kazipata kwa biashara tena aziuze kuongeza mtaji alipozitata? atakua ana fanya monkey bussiness
Hujaona Wamaasai wakiuza ng'ombe na kujenga Hotel/Guest House kule Morogoro ?
 
Namna ya kujitoa kwa mikopo na kujitegemea ni kutengeneza kapu la savings. Mfano unatengeneza faida ya Tsh 250000, save 50, nyingine lipa madeni plus other costs, jipangie kipindi mfano cha 5 yrs, then tumia saving kuendeleza biashara.

Mind you, matajiri wengi hasa wa kati mikopo ndo inawaweka mjini.
 
Mkuu ukitaka mtaji ukue basi usifanye swala lolote la kimaendeleo.

Wengi tunakopa ili tuweze kupata tulivyoshindwa kuvipata kabla.
Hilo ni kweli mkuu,
Nakumbuka back in 2008 naanza ujasiliamali.

Biashara inaenda vizur, basi nkaingiwa na wazo LA kukopa niongeze mtaji.

Nakumbuka,
Nlkopa 3mil pale crdb, dhamana ilkua ni shamba LA miti LA mama yangu.

Nkaingiza kama laki 9 kwenye finishing ya nyumba, mil 1.2 nkanunua pikipiki ya kutembelea, Afu laki 9 nikanunua mzigo

Siwezi kusahau,
Baada ya miez 6 tu nilianza kuonja joto LA jiwe kwenye marejesho benki.

Aisee,
Nilifikia hatua ya kuuza kitanda, TV, na kabati LA vyombo ili kulipa deni LA benki.
Pikipiki yenyewe niliuza kwa hasara( laki 5) ili nisiadhirike.

Nakumbuka
jins mama alivoangua kilio usiku kucha aliposikia jina langu lipo kwenye wadaiwa Sugu wa CRdb ambao baada ya siku 90 Mali zilizowekwa dhamana zitapigwa mnada.

Ila namshukuru mungu,
Nilipambana mpaka nikamaliza deni lao.

TOKEA HAPO NMEKUA MAKINI NA PESA ZA MIKOPO.

KIUHALISIA KUPITIA HAPO NLIJIFUNZA KUA NA NIDHAMU NA PESA YA MKOPO.

NA BILA MKOPO, NI NGUMU SANA KUENDELEA KIMAISHA.

CHA MUHIMU,
NI KUKOPA KWA LENGO MAALUM, NA PESA YA MKOPO IELEKEZWE KWENYE LENGO MAALUM.

NB:
Nilikopa, Ninakopa na Nitaendelea kukopa.

Mchawi wetu ni nidhamu ya pesa
 
Hivi wale wamiliki wa zile supermarket kubwa waliokuwa wamekeza humu nchini na bdae tukasikia wamefilisika sababu ya mikopo walikuwa hawajui namna ya kuinvest?
Tujifunze kufanya kazi na kidogo tulichonacho kuliko hii "artificial wealth". What's the point of of living in a 300m Mansion ambayo ipo morgaged for 20 years?
Life is very unpredictable marejesho tuseme 3m kwa miaka 5 una uhakika gani biashara itakuwepo au ndiyo ile wanasema "it's just a matter of risking" ?
Kama msingi wako ni mkopo siku ile unafika ofisini credit manager anakwambia zungusha kwanza akaunti miezi sita na uko desperate ndiyo utajua maisha ya mikopo yakoje.
 
Kila biashara INA changamoto zake, ila haiwez KUA kigezo cha moja kwa moja kuwaogopesha watu wasikope.

Kukopa ni lazima, matajiri asilimia almost 90+ wanamikopo.

Mo dewji na utajiri wake wote, ana deni kubwa sana pale CRDB

Bakhresa na utajiri wake wote,ana deni kubwa sana pale Barcrays.

Na wengineo wengi, na hawajaacha kukopa.

Wanakopa na kufungua miradi mipya kila kukicha
 
Kuna mikopo ina faida sana endapo utaitumia vizuri. Nina rafiki yangu alikopa pesa bank yeye aliamua kuwekeza kwenye ardhi. Alikuwa ananunua ardhi kwa bei nzuri baada ya miaka miwili anauza anaenda kununua sehemu nyingine kwa bei nzuri. Jamaa aliweza kupata mitaji ya kutumia njia hiyo ya kununua na kuuza ardhi
 
Matajiri wengi wanafanya hiyo biashara,

Mo hutumia mashamba yake ya mkonge kuchukua mikopo kwenye mabenki.

Kisha mikopo ile huipeleka kwenye kununua ardhi na nyumba za watu wenye Shida za kuuza kwa haraka.

Baada ya mda,
Huziuza zile nyumba/viwanja kwa faida.
 
Iyo mikopo tuna ngangania tu, ila Mwenyezi Mungu kayakataza hayo...(riba) Familia nyingi leo zinapitia wakati mgumu sana. Wazungu watatuletea mengi sana...
 
Kwanza mkopo sio pesa yako licha ya kwamba unapewa wewe, mkopo ni sawa na mtu kuishi nyumba ya kupanga, lazima ujue kuna siku utaondoka humo uende kwako au kupanga kwingine. Kuna watu wakipewa mkopo, uwe wa chuo a.k.a Boom, still ni mkopo utumie kwa swala uliloombea tu na sio vinginevyo. Kuna watu wana kopa pesa ya biashara, halafu nusu ya pesa ya mkopo anakula bata. Ukopaji wa namana hiyo lazima utalia tu.
Mimi nimewahi kukopa ile credit card ya master card, ile pesa nilidhani yangu for a moment, niliitumia vibaya. Sasa walipoanza kunidai nikawa nalipa ile minimum, nilikona deni haliishi na nikawa naona wananidai pesa nyiingi ingawa walinikopesha kidogo, nililipa kwa muda mrefu, na siku nilipokuwa nalipa pesa ya mwisho nilienda bank nikaomba na statement kama prove. Niliapa sitakopa tena. interest ilikuwa juu kitu sikujua wakati napewa MasterCard, nilikuja kujua wakati nalipa.
Mikopo sio mizuri ingawa kama walivyosema watangulizi, kopa lakini uwe na nidhamu na pesa ya mkopo.
 
Mkuu unasema kukopa halafu ukanunua gari haina shida? labda iwe gari ya biashara ila kama ni ya kutembelea utakuwa umeongeza liability tu vilevile ukikopa ili ujenge nyumba ya kupanga pia sio sahihi kwasababu itakuchukua muda mrefu pesa iliyotumika kujengea kurudi, tuchukulie umejenga nyumba yenye vyumba sita kwa million 30 na kila chumba ni elfu 50 kwa mwezi: 6x50= 300,000/= laki tatu kwa miezi 12 jumla itakuwa 3,600,000/= milion tatu na laki sita, tuone itachukua muda gani kurudisha gharama za ujenzi 30,000,000/=
3,600,000/= ukigawanya unapata 8.3 inamaana itakuchukua miaka 8 kurudisha gharama za ujenzi hivyo basi simshauri mtu akope ili ajenge nyumba ya kupangisha halafu akitegemea kodi atakayopata ndo arudishe benki
Unaweza kukopa million kumi halafu ukaziingiza kwenye biashara ambayo pesa yako ikarudi baada ya mwaka.
 
Haswa watu wengi wanafanya kama ulivyofanya wewe unakopa halafu unatoa pesa ya mkopo halafu unaiweka sehemu ambayo sio uliyokusudia. Wewe ulitakiwa kukopa laki tisa tu kwasababu ndio uliyokuwa unaihitaji
 
Haswa watu wengi wanafanya kama ulivyofanya wewe unakopa halafu unatoa pesa ya mkopo halafu unaiweka sehemu ambayo sio uliyokusudia. Wewe ulitakiwa kukopa laki tisa tu kwasababu ndio uliyokuwa unaihitaji
Ilkua ndo Mara yangu ya kwanza kukopa.

Nilishawishiwa na Rafki yangu mmoja pamoja na mdada wa crdb walokua Wakihamasisha mikopo.

Ila kupitia hilo, Siwezi kujutia. Ilisababisha nmejifunza kitu maishani

Baada ya hapo, Pesa ya mkopo nmekua na nidhamu nayo ya hali ya juu



Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Hongera sana, always we learn through mistake
 
Embu fafanua, unakopaje "credit card"?
 
Mkopo aseee acha tu nakamkopo ka 20M hapo NBC kananisumbua akili sana kila nikiangalia salary slip ndo nachoka mazima hiyo hela wanayokata
Nimeapa sitakopa teeeeenaa nimejuta better kudunduliza tu na kuridhika na ulicho nacho
Na walivyo na maneno matamu mungu anawaona
 
Embu fafanua, unakopaje "credit card"?
Unapoomba CreditCard unapewa ikiwa na pesa kiasi flani ambacho ni mkopo kwako, unatumia vyovyote utakavyo, lakini unapolipa hiyo pesa kuna interest 19.36...% unalipia. Unapewa Card inapesa, hiyo pesa siyo yako ni mkopo unaopaswa kuulipia with interest.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…