Mliowahi kukopa benki na badae kuachana na mikopo na kubaki na mitaji yenu tupeane ujuzi nasi tujikwamue

Mkuu, hayo ndo Wadau hawataki kusikia, nimejaribu kueleza hapo juu wamenijia juu. Ongeza na mikopo ya Elimu ya Juu. Mfano mzuri wa jinsi ambavyo mikopo haiwezi kumtoa mtu, ni jinsi nchi za Kiafrika zinavyokopa, lakini zinaendelea kuwa masikini.
Asilimia kubwa ya matajiri wanaendesha kazi zao kwa mikopo tena mikubwa ndugu..mikopo imewatoa wengi sana.
 
Aisee..et pesa chafu!
 
Nimesoma mawazo ya watu wote ukweli ni kwamba mikopo sio mizuri kabisa Mimi mpaka Sasa nadaiwa bank kila nikikalibia kumaliza nasema sito kopa Tena ila nikimaliza tu narudia kukopa Tena kwahiyo mikopo ni mateso
Hlo ndio tatizo kuu la mikopo..kuingia rahisi ila kutokA ni ngumu
 
Mimi nakopa Tala tu coz hawawezi nifilisi
Kwa upande wangu mikopo imenitoa sana pengine nisingefika hapa leo au ninge subir sana lkn ttzo limekuja awamu hii ya JPM mikopo imekua poison biashara zimeyumba sana nme maliza mkopo kwa sasa sikopi tena till further notice
Mikopo imesaidia wengi mkuu ila kwa wenye roho nyepesi lazima waikimbie.
 
mkuu huwa inawezekana ila dawa ya mkopo unahitaji nidhamu ya hali ya juu pia ukiweka mkopo katika biashara weka katika biashara ambayo tayar ushaona mwanzo waake na inaonekana ni biashara ya uhakika
pili usiweke mkopo katika vitu ambavyo unajua havirudishi ila vinatumia (liability) mfano nyumba, gari la matembezi, kulipa ada n.k
Inawezekana mkuu ila commitment ni jambo la kwanza
 
Asilimia kubwa ya matajiri wanaendesha kazi zao kwa mikopo tena mikubwa ndugu..mikopo imewatoa wengi sana.
Sikatai kuwa hawaendeshi biashara zao kwa mikopo, ninachosema ni kwamba unatakiwa kuwa makini na kuiheshimu sana pesa ya mkopo, vinginevyo italipwa na wategemezi wako; na hiyo ndo inatokea kwa matajiri wengi, wanaendelea kukopa mpaka uzeeni, wakifa mabenki yanauza mali walizoacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…