Mkuu, heshimu mawazo ya watu wengine kama ambavyo na ya kwako yanaheshimiwa. Hatuwezi wote kufikria kitu kimoja. Aidha, humu JF ni tuko kwenye Mdahalo, sithani kama ingekuwa Mdahalo wa wazi yaani mimi na wewe tunaonana, ungeweza kuniambia niache "stupidity" kwa jambo wazi kama hili. Ni kweli inafahamika kuwa kutokana na mabadiliko ya aiana ya maisha ambayo watu wamekuwa wakiishi, wamebanwa na income yao imepungua so uwezo wa kuwa dispose hyo income kwenye biashara umepungua ndo maana baadhi ya watu wanalalamika kuwa biashara zao zinayumba. Vilel vile, kuondoa watumishi wenye vyeti feki kumepunguza idadi ya wateja katika biashara. Hoja yangu sio wafanya biashara kuendelea kulalamika, wanapaswa kujipanga kuendeleza biashara yao kwa aina hiyo ya kipato maana ndicho kipato halali. Hii ni kwa sababu kipindi cha nyuma watu walikuwa wanapata pesa amabazo hawana uchungu nazo, vivyo hivyo na matumuzi yalikuwa ya ovyo ndo maana wafanya biashara nao walikuwa wanaona wanapata pesa nyingi lakini zilikuwa chafu. Pia, hata hao wafanyabiashara walikuwa hawalipi kodi ipasavyo, watu pekee waliokuwa wanalipa kodi halali ni wafanyakazi wa Sekta ya Umma. Shikirisha ubongo wako, wacha Mhe. Rais aweke mazingira mazuri ambayo baadaye kila mtu atafaidi matunda ya uhuru.