Inakuwaje wanangu wa Jamiiforums
Binafsi mimi nilikuwa mpenzi mtazamaji, na Hakuna kitu kilikuwa kinaniuzi kama kuona watu wakizichapa atokee mtu aje kugombolezea
Kwa wale mliowahi kuzichapa class mutuelezee sababu ilikuwa ni ipi, je bifu liliendelea, kama ulichapwa vp kisasi kilitokea
Kwa wale wapenzi watazamaji wenzangu ulikuwa unaenjoy nini wana wakizichapa class?
View attachment 1947737
Dah😂 umenikumbusha nipo darasa la 4 shule zetu izi za kidumu na mfagio huku kuna kupishana kukaa kwenye madawati...
Sasa mi nlikua nmekaa chini.. kuna bidada akapita akanikanyaga nkavumilia. Nlikua type hii ya wanafunzi wapole sana class na wanaofanya vizuri, bas bhana ... akaja kupita tena akanikanyaga mara ya pili, nkamshika nkamwambia umenikanyaga mara ya pili sasa ila hakujali.. ani alikua ni wale micharuko ya darasa...
Mara ya tatu alivopita akanikanyaga afu akasimamia apo apo weeeeh!! Kichaa changu cha kipemba kikaamka😂 nkamsukuma huku namwambia umenikanyaga nakuambia huniskii..
Akainuka tukashikana.. nlimshushia migumi ya mgongo mpaka wanadarasa wakafurahi, akaingia ticha watu kimya.. sa alivoona ticha na ile kuwa kaaibishwa maana alikua celebrity wa darasa akaanza kulia..
Ticha kuuliza kulikoni nkamuelezea, nkaambiwa nmekosea kwa hiyo nkachapwa fimbo 6 ila dada ndo aliaminika ndo mchokozi maana kwa hali ya kawaida mimi mpole siwezi kuchokoza mtu.
Tukio jingine hili ndo nliloapa stakuja kuzichapa tena mimi!
Ilikua kipindi nipo form 3.. enzi za ujana ujana na balehe.. as usual nlikua tu mpole na mkimya.. kuna mdada akaanza kunletea pigo za ki se nge .. yani ujinga ujinga tu.. anansema ovyo ovyo kwa watu... yan mpaka watu wanashangaa mi nawezaje kuwa na izo tabia afu nlikua prefect enzi izo..
Kumbe bhana boyfriend nliekuwa nae bi mdada alikua anamtaka na hana njia ya kumpata ... apo npo nae since form 1... akaona njia rahisi ni kunichafua asee nlikonda kwa kuvumilia kejeli za kijinga jinga...
Siku tumetoka skuli nkaona huu u se nge utaisha lini unaniathiri mkimya mimi.. nkasema hapana.. alikua na rafiki ake nkamdaka nkamwambia nna maswali nataka kukuuliza.. tuongee yaishe..
Kheeeh akawa ananijibu vibaya, alipokosea ni pale aliponitukana🤕 nlimchapa kofi la uso.. alivoona npo serious akataka tupigane nkajisemea kudadadeki nmevumilia sana ngoja tuheshimiane kidogo...
Mwenzie yupo mbele uko katangulia .. aliponitibua ni aliponkatia vifungo vya shati.. nlimpiga ngumi izo..(wakati nakua nmeishi na kaka zangu kwa hiyo michezo ya ngumi walinifundisha sana na karate na nlikua nafanya mazoezi sana ya mwili... ila msniogope mi mrembo tu 😂😂)
Bas nlikua natembea na vile vijiwembe vya surgery nlikitoa nlimchana chana.. mpaka tunakuja kuamuliwa nlikua nmemuumiza sana.. apo wadada walikua waogopa kunishka ilibidi wakaka ndo wanithibiti...
Baada ya kuona ule msala nkabadili njia nduki😂 hawakuniona .. bahati nzuri nlikua na sweta nkavaa nkaenda kupanda gar.. na skwenda shule wiki nzima..
Nlikuja tu kuambiwa mdada kachukua RB polisi na kesi ikaenda shule.. staff nzima haikuamini nlichofanya maana nlikua mpole mno wala sio muongeaji..
Kwa ustaarabu mkuu wa shule akamsihi ile kesi akafuta polisi ikamalizwa kishule.. nkapigwa suspension wiki 3.. na kazi za nje ya darasa wiki 1 nkavuliwa na uongozi na nliondoka na viboko vyangu 8 vya makalio!!!
Mpaka leo nmesema siji kupigana tena mimi hasa na mdada japokuwa juzi kati tu nmekoswa koswa na kupiga mtu😂😂😂