Mliowahi kutumia bati za kampuni ya BATI BOMBA LTD au kampuni zozote ndogo za mabati

Mliowahi kutumia bati za kampuni ya BATI BOMBA LTD au kampuni zozote ndogo za mabati

Mimi nimewahi kuezeka nyumba kwa kutumia mabati ya rangi. Mwaka 2014 niliezeka nyumba kwa mabati ya kampuni ya Ando. Huu ni mwaka Wa 8 sasa bati lipo vizuri. Na mwaka jana nimeezeka nyumba nyingine kwa mabati ya Kampuni ya Taishan, ni mwaka sasa sijaona tatizo lolote lile, labda kwa miaka ijayo.
Naomba mrejesho wa hizo bati za Taishani kwa mwaka huu 2024, bado zina hali nzuri? Nataka kufanya maamuzi mkuu.
 
Bati za Covermax za ALAF ukiezekea nyumba inanyooka hatari.

Huwa nikiangalia paa la nyumba yangu najkuta natabasamu tu
 
Wakuu nahitaji bati gauge28 kampuni yoyote angalau yenye bei ndogo nimegusa alaf hapagusiki msaada unahitajika
 
Hakuna bati isiyopauka zinapishana tu muda , ujanja sasa hivi ni kununua bati rangi inaitwa charcoal gray basi hiyo ukinunua inakua kama nyeusi hivi ,
Uzuri wake inapauka haraka sana ila ule mpauko ndio unakuja kuleta rangi moja tamu sana ,

Sio ukachukua mabati mekundu sijui bluu utakua ukiangalia paa lako unameza mate ya uchungu
 
Mbona dar Kuna viwanda vingi sana!! Nenda maeneo ya tazara utakutana na viwanda vingi sana chagua kiwanda kimoja Kati ya dragon,kinglion,bati Bomba etc.
Viwanda vipo mkuu sema madalali wengi mimi sitaki kuzunguuka maviwandani ningepata mtu aliewahi kununua kwa bei nzuri anielekeze ingekuwa poa sana
 
Back
Top Bottom