Mliowahi kutumia bati za kampuni ya BATI BOMBA LTD au kampuni zozote ndogo za mabati

Naomba mrejesho wa hizo bati za Taishani kwa mwaka huu 2024, bado zina hali nzuri? Nataka kufanya maamuzi mkuu.
 
Bati za Covermax za ALAF ukiezekea nyumba inanyooka hatari.

Huwa nikiangalia paa la nyumba yangu najkuta natabasamu tu
 
Wakuu nahitaji bati gauge28 kampuni yoyote angalau yenye bei ndogo nimegusa alaf hapagusiki msaada unahitajika
 
Hakuna bati isiyopauka zinapishana tu muda , ujanja sasa hivi ni kununua bati rangi inaitwa charcoal gray basi hiyo ukinunua inakua kama nyeusi hivi ,
Uzuri wake inapauka haraka sana ila ule mpauko ndio unakuja kuleta rangi moja tamu sana ,

Sio ukachukua mabati mekundu sijui bluu utakua ukiangalia paa lako unameza mate ya uchungu
 
Mbona dar Kuna viwanda vingi sana!! Nenda maeneo ya tazara utakutana na viwanda vingi sana chagua kiwanda kimoja Kati ya dragon,kinglion,bati Bomba etc.
Viwanda vipo mkuu sema madalali wengi mimi sitaki kuzunguuka maviwandani ningepata mtu aliewahi kununua kwa bei nzuri anielekeze ingekuwa poa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…