Mliowahi weka fedha kwenye "Fixed account" naomba mnielimishe hapa

UMUNYU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Posts
726
Reaction score
564
Mliowahi weka fedha zenu kwenye akaunti ya muda maalumu Ninaomba ushauri wenu!

Riba ikoje,kwa kiwango gani na kwa muda gani?Benki ipi ni nzuri!

Naomba ufafanuzi hasa kwenu nyie ambao mlishatumia akaunti hiyo!

Nilijaribu kupita benki kadhaa nilichogundua kila benki inavutia kwake!
 
Faida ni kidogo sana

Mfano NMB ukiweka fixed deposit ya TShs 10,000,000/=
Unapewa faida ya 6% kwa mwaka mmoja
Mwisho wa mwaka utapata faida almost TShs 600,000/=
Ukija kuondoa kodi hapo unabaki na kama TShs 530,000/=

Na ukijakuwekeza UTT-AMIS faida inakua approximately mara mbili (10% mpaka 15%) ya hizo fixed deposits.

All the best [emoji1545]
 
Faida ni kidogo sana

Mfano NMB ukiweka fixed deposit ya TShs 10,000,000/=
Unapewa faida ya 6% kwa mwaka mmoja
Mwisho wa mwaka utapata faida almost TShs 600,000/=
Ukija kuondoa kodi hapo unabaki na kama TShs 530,000/=

N ukijakuwekeza UTT faida inakua approximately mara mbili (10% mpaka 15%) ya hizo fixed deposits.

All the best [emoji1545]
Asante kwa ushauri nitaufanyia kazi!UTT ni nini?
 
Mliowahi weka fedha zenu kwenye akaunti ya muda maalumu Ninaomba ushauri wenu!!Riba ikoje,kwa kiwango gani na kwa muda gani?Benki ipi ni nzuri!Naomba ufafanuzi hasa kwenu nyie ambao mlishatumia akaunti hiyo!!Nilijaribu kupita benki kadhaa nilichogundua kila benki inavutia kwake!
Riba ipoje --- haipo fixed, ukienda kinyonge na kishamba wanakula kichwa

Benki ipi nzuri -- inategemea ila uzuri wa benk ni ile itayokupa riba kubwa wala sio uzuri kwa maana ya brand
 
Ni mfuko wa kuwekeza pesa unaoendeshwa serikali.

Unaweka zako pesa na kuwa unapata faida ya approximately 0.027% kila siku ya pesa ulizowekeza.
Sawa,sasa hii ni benki au ninini?Mtu anafungua akaunti wapi?Kiwango cha chini cha kufungua akaunti ni kipi?
 
Ni mfuko wa kuwekeza pesa unaoendeshwa serikali.

Unaweka zako pesa na kuwa unapata faida ya approximately 0.027% kila siku ya pesa ulizowekeza.
Kwa hiyo nikiwekeza Milioni moja, kwa siku napata elfu 27,000. Kwa mwezi napata 810,000?.
Au mie ndio sijaelewa.
Naomba kueleweshwa.
 
Mliowahi weka fedha zenu kwenye akaunti ya muda maalumu Ninaomba ushauri wenu!

Riba ikoje,kwa kiwango gani na kwa muda gani?Benki ipi ni nzuri!

Naomba ufafanuzi hasa kwenu nyie ambao mlishatumia akaunti hiyo!

Nilijaribu kupita benki kadhaa nilichogundua kila benki inavutia kwake!
CRDB
FDR- 10% per Year.
Mzigo Flex-9% per year.
Kijani Bond-10.25% per Year.

TPB
11%per year

UTT
Liqiuid fund 1% kwa mwezi (inaweza panda au Shuka , kulingana na Soko).
 
Riba ipoje --- haipo fixed, ukienda kinyonge na kishamba wanakula kichwa

Benki ipi nzuri -- inategemea ila uzuri wa benk ni ile itayokupa riba kubwa wala sio uzuri kwa maana ya brand

Unaumingiza mwenzako chaka hapa kwa kiasi fulani, ukiachilia mbali hiko ulichokisema kama muwekezaji inapaswa kujua usalama wa fedha zako mahali unapoziweka.

Mara nyingi ukiona riba inakuwa kubwa ujue benki zinapitia changamoto ya ukwasi, hivyo zinawavutia wateja waweke fedha. Hii pia huathiri hadi gharama za mikopo mara nyingine uchechefu wa mikopo kuanza kutokea.

Sasa hapo usipokuwa makini ndo kuna ile misala ya benki kuwa chini ya uangaliza benki kuu ama hatimae kuondoshwa kabisa. Nadhani utaelewa fidia unazoanza kupata. Kama ilikuwa senti yako ya mwisho presha lazima ikupate.
 
Fungua zote ila usifungue kwenye benki moja ipo hapo makumbusho upande wa kushoto kama unaenda mwenge . Niliweka fixed account ya million 4 kwa mwaka Baada ya kushawishiwa na wafanyakazi wa hapo kupewa riba nzuri lakini siku ya kumachua wakaanza sura zao halisi mara makato ya uendeshaji mara kodi ya serikali unajua mara sijui upuuzi gani waliishia kunipa faida elfu 60 na pole nyingi sitaki kuwasikia nikablock na namba zao.

Ushauri fanyia biashara hiyo hela hata kwenye kukaanga chips achana na huu udanganyifu wa Fixed account utakuja kunikumbuka
 
Usiogope kuweka hela kwenye fixed deposit account. Kitu cha kuzingatia ni benki unayoenda kuwekeza ili usije ukaishia kupata hasara.
Benki zenye mkono wa serikali mara nyingi zinaaminika na ni ngumu kufilisika kirahisi tofauti na benki za jumuiya au kikundi. Mifano inajulikana ya benki zilifilisika katika siku za karibuni...
 
Fungua zote ila usifungue kwenye benki moja ipo hapo makumbusho upande wa kushoto kama unaenda mwenge . Niliweka fixed account ya million 4 kwa mwaka Baada ya kushawishiwa na wafanyakazi wa hapo kupewa riba nzuri lakini siku ya kumachua wakaanza sura zao halisi mara makato ya uendeshaji mara kodi ya serikali unajua mara sijui upuuzi gani waliishia kunipa faida elfu 60 na pole nyingi sitaki kuwasikia nikablock na namba zao.

Ushauri fanyia biashara hiyo hela hata kwenye kukaanga chips achana na huu udanganyifu wa Fixed account utakuja kunikumbuka
ACCESS BANK
Nasikia pia mikopo yao ni chupi mkononi.
 
Mliowahi weka fedha zenu kwenye akaunti ya muda maalumu Ninaomba ushauri wenu!

Riba ikoje,kwa kiwango gani na kwa muda gani?Benki ipi ni nzuri!

Naomba ufafanuzi hasa kwenu nyie ambao mlishatumia akaunti hiyo!

Nilijaribu kupita benki kadhaa nilichogundua kila benki inavutia kwake!
Depreciation ujue shilingi Iko je wekeza kwenye estate
 
Kwa hiyo nikiwekeza Milioni moja, kwa siku napata elfu 27,000. Kwa mwezi napata 810,000?.
Au mie ndio sijaelewa.
Naomba kueleweshwa.
Hapo ufafanuzi tunaomba utueleweshe ndugu
 
Back
Top Bottom