Mlioweza kuiishi sheria hii ya utajiri njooni mnipe mbinu

Friedrich Nietzsche

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
2,095
Reaction score
3,649
Kati ya sheria au Rule ngumu katika kujenga na kuimarisha kipato au kusaka utajiri ni hii

1. “Earn before you Spend”

Hii rule nimejaribu miaka mitatu sasa siiwezi hasa kwa wafanyakazi ndio kazi kweli kweli

Kifupi sheria inasema “usitumie kabla hujaingiza” zile siku ambazo hujaingiza hela yeyote usitumie hata senti

Ukiingiza fedha ndio unaweza kutumia tena matumizi yasizidi ulichoingiza au yaendane.

Kama umeweza hii sheria tuambie unatumia mikakati gan? maana mi najikutaga wiki zime nimespend na sija earn hata mia
 
Nilichoelewa ni unatakiwa uwe bahili, usiwe mtu wa tamaa kwa kila unachoona kwakuwa una hela basi unanunua tu hata kazi ya hicho kitu huna, ama ni ile kwenda na matoleo kila toleo unataka, huweki akiba hata kidogo ukipata shida tu kidogo lazima ukakope kausha damu mara wezesha mara ile voda sijui inaitwaje yani huna uvumilivu wa kuishi kutokana na chako kidogo na kutunza kidogo kwa ajili kufungua biashara.
 
 
Kitu wengi ambacho hawakielewi ni kuwa UTAJIRI UPO KIROHO SANA! ndo maana si kila mtu anaweza kuwa tajiri wengine ni wasindikizaji tu.
Ili uwe tajiri lazima upitie mambo fulani ya kiroho na ku break au kujua hizo codes za utajiri.
Ndo maana kama ulishawahi sikia mtu anasema kuwa pamoja na kusoma au kutokusoma katika ukoo wetu hakujatokea tajiri hata mmoja!

Mambo yote ya kufanikiwa au kutofanikiwa au vikwazo vya kimafanikio vipo Bayana/wazi katika ulimwengu wa roho.
Ulimwengu wa roho una pande mbili Nuru na giza! Huko kwingine endelea.......

NB; Utajiri upo kiroho sio wote wanaweza kuwa matajiri unless umezijua codes za kiroho zitakazokupa utajiri. Ili uziweze kuzijua hizo codes lazima uziishi hizo codes so inahitaji uthubutu na roho ngumu!
 

Fungua hizo codes sasa tuzijue kiongozi
 
Fungua hizo codes sasa tuzijue kiongozi
Hizo mkuu unafungua wew mwenyew kwa imani ulio nayo na mapito yako ukiyatathimin na kujitambua,hakuna mtu anaweza kukufungulia,

Trust me kuwa tajiri sio rahisi chief inahitaji A lot of sacrifice kimwili na kiroho.
Usione watu wanamiliki masheli,makampuni e.t.c beyond that kuna kujitoa kweli kweli na kuziishi hizo kanuni.
 
Halafu chukua hii sijui kama utaiweza

'Tumia pesa ya pesa Yako"
 
H
Hii ngumu kwa kweli nimepata book,nimekopa vitu vya book3!
 

ELEZEA TUNAWEZAJE!! maana kuna walokole wana iman ila wanazid kua masikini tu
 
Sasa si ndo uviseme hivyo kiroho na kimwili ili tuvijue? Ni inakuaje yani? Maana usiseme tu hapa pasi kufafanua, maana yake na wewe utakua hujui ila unatupanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…