Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa shule hii,acha niwe nakesha JF.Kwa inategemeana na mahali ulipo kwani kuna maeneo mtandao A unashika sana wajati mtandao B unakuwa hafifu.
1.Fiber
Ndio chaguo lakwanza ikiwa upo maeneo yaliyofikiwa na mtandao wa fiber wa TTCL hasa maeneo ya mjini.Yapo makampuni binafsi yanasambaza fiber ila kwa gharama ya juu kidogo ukilinganisha na TTCL.
UZURI WA FIBER
*Ndio chanzo mama cha internet baada ya wire ndio ifuate wireless hivyo nisawa na kusema upo kwenye branch za mkongo wa Internet.
*Bei nafuu zaudi,Ikiwa na kima cha chini 55,000/= kwa 20 Mbps.
*Haiathiriwi na hali ya hewa.Ukizingatia inatumia wire toka chanzo hadi kwa mlaji hivyo changamoto za umbali,mvua,upepo nk havitokusumbua.
*Hamna Jam.Vifurushi ya unlimited hasa hivi vya kwenda kwa mlaji huwa ni shared network hivyo watumiaji wanapokuwa wengi kasi hupungua.Na hapo ndio utajua maana ya sentensi UP TO 10 Mbps,20 Mbps,30 Mbps nk wakimaanisha speed inaweza kuwa chini ya hapo ama ikafikia hapo.
*Free installation kwa TTCL kwa makampuni binafsi sijajua.
UBAYA WA FIBER
*Haihamishiki yani ipo fixed eneo ulipounganishwa hivyo huwezi kuhama nayo.
* Inachukua muda kuunganishwa kwa TTCL basi huchukua hata mwaka hasa vifaa vikiwaishia hawa sio wakuwategemea kabisa.Makampuni binafsi sijajua ila kama upo kwenye zone zao basi nisuala la wiki tu.
*Ipo limited.Inapatikana kwa wingi maeneo ya mjini kwa walio nje ya mji itakulazimu ugharamike nguzo na vifaa kufikishiwa yani nikama ilivyo kufungiwa umeme wa tanesco.
*Miundombinu kuharibika.Hasa kipindi cha mvua nguo kuanguka waya kukatika ndio kukatika kwa mtandao hadi waje kuunganisha tena.
ANTENA
Hii wanayo Vodacom na Airtel.Mfano huduma ya superkasa ya voda huwa wanaunganisha kwa kutumia antena maalum yenye kuwasiliana na mnara wao ulio karibu yako.Hii inakuwa na kasi moja tu ya 20 Mbps kwa 115000.
Airtel sijajua gharama zao upande wa antena.
UZURI WA ANTENA
*Antena hubust mtandao mana hufungwa nje ya jengo lako hivyo kunasa mawimbi kwa urahisi.
*Ndio utapata kifurushi cha 20mbps kwa 115000 upande wa voda kwa huduma ya supakasi.
UBAYA WA ANTENA
*Ipo fixed eneo lako ulipofungiwa.
*Inaweza kuathiwa na mvua,radi nk
*Lazima utangulize malipo ya miezi 2 ndio waje kukufungia ila pesa utarudishiwa baada ya kumaliza mkataba ikiwa hutaki kuendelea.
*Kwa voda kifurushi ni kimoja tu cha 2) Mbps.
ROUTER
Hapa kuna makampuni matatu voda,tigo na Airtel.
Vodacom wako na router 5G kwa kifurushi kinachoanzia 30 Mbps kwa 120,000.
Utalazimika kutanguliza kulipia miezi 2 ya kifurushi ukitakacho mfano 240000 kwa kifurushi cha 120000 ili usajiliwe.
Sababu ya sifa ya 5G hivyo vifaa vinapatikana maeneo yaliyofikiwa na 5G yao tu.
Airtel wako na router ya 5G kwa kifurushi kinachoanzia 10 Mbps kwa 70000...30 Mbps kwa 110000 nk
Utalazimika kulipia na 200000 ya kifaa (router)
Vifaa vinapatikana maeneo yaliyofikiwa na 5G yao tu.
Tigo wako na router ya 5G kwa kifurushi kinachoanzia 10 Mbps kwa 70000...30 Mbps kwa 100000 nk
Utalazimika kulipia kifaa router kitu kama 600000 hivi.
My take
Chukua router kulingana eneo ulipo ambapo mtandao husika suala la internet wapo vizuri.
Usidanganyike na neno 5G hii ni teknolojia tu ya usafirishaji mawimbi hivyo hata 4G inaweza kucover kifurushi chako.4G inaweza kufikia speed ya 100 Mbps - 150 Mbps huku 5G ikifikia 300 Mbps.
Hivyo hata kama upo eneo lisilo na 5G bado utapata mawasiliano kupitia 4G.
Zingatia sana 5G ikiwa unajiunga na 150 Mbps au zaidi.
*Vifurushi vyote na huduma zote ni unlimited yaani unatumia kwa kupimiwa speed sio GBs hivyo tumia uwezavyo.
*Kwa kuwa unlimited hii haimaanishi uunganishe marafiki na majirani wote kwenye WiFi yako kwa mtashea iyo speed uliojiunga.
*Ili kupata speed halisi ya kupakuwa file basi gawanya kwa 8 Mbps ulizojiunga.Namaanisha kwa mfano umejiunga kifurushi cha 10 Mbps inakuwa 10/8=1.25mbps yaani wakati unadownload basi speed iwe inasoma hadi kufikia 1.25 pale juu ya simu kwenye minara ya mtando na data connection ichezee hapo 700kbps-1.25mbps japo pia yaweza kupitiliza kulingana na eneo ulipo au wakati wa usiku.
Kwangu mimi kwa maeneo niliyopo ni best choice na kifurushi unaweza kubadili muda wowote yaani unacholipia ndio unachopatiwa.
TTCL panahitajika mkurugenzi mwenye uchungu na taifa na kuliinua shirika hilo la Umma linalouliwa na wachache fulanifulani.
Kuna vijana waliagiza starlink devices ili waje kuuza bongo .. nasikia walikamatwa kwa kukosa vibali TCRA, Je, ni kweli?Ufanyaji kazi ni mmoja, Microwave inasaidia kupunguza ping, 5G yenyewe by nature ina ping ndogo, uzuri wa 5G ni capacity hata kama mtakua wengi mtaani ngumu speed kudrop.
Starlink around 1.5m installation na kwa mwezi around 120,000 huku kwetu.
Chukua Tigo au Airtel. Kasi yao ni nzuri, yaani unapata value for money; hali kadhalika pia bei yao ni nafuu ukilinganisha na Vodacom.Naona kama kwa sasa limeingia wimbi la kutangaza na kuuza Rooters za WIFI kwa makampuni ya simu nchini.
Kila mmoja anavutia kwake kwa vifurushi vya Mbps 10, 20 na 30 ambavyo ni kwa 4G na 5G unlimited mwezi mzima.
Je, ninunue toka kwa kampuni gani ambayo huduma zake katika hili ni reliable na price friendly kwa matumizi ya nyumbani?
Msaada tafadhali kwa walio experienced huduma hii iliyokuja kwa kasi!
Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Sina uhakika ila kama unauza ndio watakukamata, ila kama unalo matumizi ya nyumbani sidhani kama hata wana time na wewe. Niliwahi kuona mtu alituma picha humu NMB Namanga wanatumia.Kuna vijana waliagiza starlink devices ili waje kuuza bongo .. nasikia walikamatwa kwa kukosa vibali TCRA, Je, ni kweli?
No kweli kuna story humu jf na picha zao msijiletee matatizo not worth it.Kuna vijana waliagiza starlink devices ili waje kuuza bongo .. nasikia walikamatwa kwa kukosa vibali TCRA, Je, ni kweli?
Smile imenunuliwa na vodacom mwaka huu sijui kama bado wanatoa huduma.Jamani hii kampuni ya simu Smile baso wapo? Kuna mini wi fi pocker router nimekikuta ofisini, kama wapo nikitumie
Tigo ni lazima kila mwezi ununue kifurushi chake kwa miezi 24 (non stop) usipofanya hivyo deni lako la mwezi husika litawekwa siku ukinunua kifurushi kuyakataa kulipa deni. Mfano kama umechagua kifurushi cha laki 1 kwa mwezi ni lazima kila mwezi ulipe laki 1 hadi miezi 24 iishe baada ya hapo utajua unaamua ununue au usinunueChukua Tigo au Airtel. Kasi yao ni nzuri, yaani unapata value for money; hali kadhalika pia bei yao ni nafuu ukilinganisha na Vodacom.
Shukrani mkuuKwa inategemeana na mahali ulipo kwani kuna maeneo mtandao A unashika sana wajati mtandao B unakuwa hafifu.
1.Fiber
Ndio chaguo lakwanza ikiwa upo maeneo yaliyofikiwa na mtandao wa fiber wa TTCL hasa maeneo ya mjini.Yapo makampuni binafsi yanasambaza fiber ila kwa gharama ya juu kidogo ukilinganisha na TTCL.
UZURI WA FIBER
*Ndio chanzo mama cha internet baada ya wire ndio ifuate wireless hivyo nisawa na kusema upo kwenye branch za mkongo wa Internet.
*Bei nafuu zaudi,Ikiwa na kima cha chini 55,000/= kwa 20 Mbps.
*Haiathiriwi na hali ya hewa.Ukizingatia inatumia wire toka chanzo hadi kwa mlaji hivyo changamoto za umbali,mvua,upepo nk havitokusumbua.
*Hamna Jam.Vifurushi ya unlimited hasa hivi vya kwenda kwa mlaji huwa ni shared network hivyo watumiaji wanapokuwa wengi kasi hupungua.Na hapo ndio utajua maana ya sentensi UP TO 10 Mbps,20 Mbps,30 Mbps nk wakimaanisha speed inaweza kuwa chini ya hapo ama ikafikia hapo.
*Free installation kwa TTCL kwa makampuni binafsi sijajua.
UBAYA WA FIBER
*Haihamishiki yani ipo fixed eneo ulipounganishwa hivyo huwezi kuhama nayo.
* Inachukua muda kuunganishwa kwa TTCL basi huchukua hata mwaka hasa vifaa vikiwaishia hawa sio wakuwategemea kabisa.Makampuni binafsi sijajua ila kama upo kwenye zone zao basi nisuala la wiki tu.
*Ipo limited.Inapatikana kwa wingi maeneo ya mjini kwa walio nje ya mji itakulazimu ugharamike nguzo na vifaa kufikishiwa yani nikama ilivyo kufungiwa umeme wa tanesco.
*Miundombinu kuharibika.Hasa kipindi cha mvua nguo kuanguka waya kukatika ndio kukatika kwa mtandao hadi waje kuunganisha tena.
ANTENA
Hii wanayo Vodacom na Airtel.Mfano huduma ya superkasa ya voda huwa wanaunganisha kwa kutumia antena maalum yenye kuwasiliana na mnara wao ulio karibu yako.Hii inakuwa na kasi moja tu ya 20 Mbps kwa 115000.
Airtel sijajua gharama zao upande wa antena.
UZURI WA ANTENA
*Antena hubust mtandao mana hufungwa nje ya jengo lako hivyo kunasa mawimbi kwa urahisi.
*Ndio utapata kifurushi cha 20mbps kwa 115000 upande wa voda kwa huduma ya supakasi.
UBAYA WA ANTENA
*Ipo fixed eneo lako ulipofungiwa.
*Inaweza kuathiwa na mvua,radi nk
*Lazima utangulize malipo ya miezi 2 ndio waje kukufungia ila pesa utarudishiwa baada ya kumaliza mkataba ikiwa hutaki kuendelea.
*Kwa voda kifurushi ni kimoja tu cha 2) Mbps.
ROUTER
Hapa kuna makampuni matatu voda,tigo na Airtel.
Vodacom wako na router 5G kwa kifurushi kinachoanzia 30 Mbps kwa 120,000.
Utalazimika kutanguliza kulipia miezi 2 ya kifurushi ukitakacho mfano 240000 kwa kifurushi cha 120000 ili usajiliwe.
Sababu ya sifa ya 5G hivyo vifaa vinapatikana maeneo yaliyofikiwa na 5G yao tu.
Airtel wako na router ya 5G kwa kifurushi kinachoanzia 10 Mbps kwa 70000...30 Mbps kwa 110000 nk
Utalazimika kulipia na 200000 ya kifaa (router)
Vifaa vinapatikana maeneo yaliyofikiwa na 5G yao tu.
Tigo wako na router ya 5G kwa kifurushi kinachoanzia 10 Mbps kwa 70000...30 Mbps kwa 100000 nk
Utalazimika kulipia kifaa router kitu kama 600000 hivi.
My take
Chukua router kulingana eneo ulipo ambapo mtandao husika suala la internet wapo vizuri.
Usidanganyike na neno 5G hii ni teknolojia tu ya usafirishaji mawimbi hivyo hata 4G inaweza kucover kifurushi chako.4G inaweza kufikia speed ya 100 Mbps - 150 Mbps huku 5G ikifikia 300 Mbps.
Hivyo hata kama upo eneo lisilo na 5G bado utapata mawasiliano kupitia 4G.
Zingatia sana 5G ikiwa unajiunga na 150 Mbps au zaidi.
*Vifurushi vyote na huduma zote ni unlimited yaani unatumia kwa kupimiwa speed sio GBs hivyo tumia uwezavyo.
*Kwa kuwa unlimited hii haimaanishi uunganishe marafiki na majirani wote kwenye WiFi yako kwa mtashea iyo speed uliojiunga.
*Ili kupata speed halisi ya kupakuwa file basi gawanya kwa 8 Mbps ulizojiunga.Namaanisha kwa mfano umejiunga kifurushi cha 10 Mbps inakuwa 10/8=1.25mbps yaani wakati unadownload basi speed iwe inasoma hadi kufikia 1.25 pale juu ya simu kwenye minara ya mtando na data connection ichezee hapo 700kbps-1.25mbps japo pia yaweza kupitiliza kulingana na eneo ulipo au wakati wa usiku.
Kwangu mimi kwa maeneo niliyopo ni best choice na kifurushi unaweza kubadili muda wowote yaani unacholipia ndio unachopatiwa.
TTCL panahitajika mkurugenzi mwenye uchungu na taifa na kuliinua shirika hilo la Umma linalouliwa na wachache fulanifulani.
Updates...
Tigo sasa wanatoa router zao kwa kulipia bando husika hivyo router inabaki kuwa mali ya kampuni...Hii inamaanisha ukilipia 100k kwa kifurushi cha 20mbps basi unapewa router ikiwa tayari na kifurushi husika.
Airtel ni wezi wanaambia watu router zao ni unlimited lakini ukweli ni kuwa ziko limited.Ukitumia hadi kufika kiasi fulani cha gb kulingana na kasi uliyojiunga basi wanakuwekea data cap yani wanapunguza speed hadi kufikia 2mbps mpaka pale muda wako uliobaki uishe au ununue upya.Haya nimeyajua kupitia mimi binafsi kuambiwa na huduma kwa wateja kuwa wako na user limit policy ambazo hawajaziweka wazi kwa wateja wao.Pia malalamiko yamejaa kwenye page zao mitandaoni.
Mtandao gani haoNchi yetu bado internet ni zengwe Tu hizo router za mitandao ya simu ni wezi mpaka basi ukitumia router maumivu na ukiweka bundle la kawaida ndio maumivu mara mbili
Wanakuumiza kwenye spidi ukilipia utapata speed ya Kasi Kwa siku 3 za mwanzo baada ya hapo ni usanii tu
Airtel ambao ndio walau wanasema wako friendlyMtandao gani hao
duuhAirtel ambao ndio walau wanasema wako friendly
Kwa maana hiyo hata kama eneo langu sina 5G mkoani, nikichukua airtel ya 5G itaoperate 4G fresh tu?Inategemea ulijiunga huduma gani, kama ni ile ya Antena inatumia Microwave signal, lazima ziwepo.
Nafkiri huduma zote za 5G hazina hii limitation.
Airtel watu wananunua mjini na kutumia mkoani.
Ita operate sema kuna possibility Waka throttle speed.Kwa maana hiyo hata kama eneo langu sina 5G mkoani, nikichukua airtel ya 5G itaoperate 4G fresh tu?
Kwa mitandao ya simu Airtel wapo friendly zaidi, Gharama ndogo za kujisajili ambayo ni laki 2, wanakupa router na powerbank incase umeme unakatika ama upo nje ya nyumba. Vifurushi vyao vinaanzia 70,000 kwa mwezi
Voda pia wapo vizuri ila wame target zaidi wafanyabiashara, usajili bure ila utahitaji ka kila mwezi kulipa, vifurushi vinaanzia 120,000
Tigo wao gharama ghali sana kujiunga 650,000 ila kwa mwezi ni 70,000
Angalia kwako mambo haya
1. Unapata 5G? Kama unapata ni mtandao upi?
2. Pima speed zote za 4G na 5G angalia mtandao upi unazidi speed husika unayotaka kununua...
Then chagua mtandao kutokana na quality ya mtandao ya eneo lako, u naweza toa hela nyingi ukaishia kupata speed mbovu.