Mlipuko huu wa Rooters za WIFI kwa kampuni za Simu ipi ni nzuri Kwa matumizi nyumbani?

Mlipuko huu wa Rooters za WIFI kwa kampuni za Simu ipi ni nzuri Kwa matumizi nyumbani?

Mkuu,
Kwa uzoefu wako kwenye hizi router za 5g kwa haya makampuni ya simu yote, kampuni gani inayotoa best 5g router in terms of quality of brand and service. Najua hili liko technical zaidi especially kwenye hardware part. It's something am eager to know before I make purchase decision.
Binafsi ninapoishi nimetest 4g zote kwa maana ya Airtel Tigo na Voda na so far nimeona kwa hapa kwangu zina respond vizuri tu.
Kinachonisukuma kwenda kununua 5g router ni kifurushi cha unlimited kwa sababu matumizi yangu ya kawaida nikinunua limited bundles zinaisha haraka sana.
Ntashukuru kwa majibu yako kwenye haya maeneo niliyouliza. Thanks
Mkuu mitandao ya simu huwa haitabiriki, utakaokupa Signal za 5G za uhakika consider huo zaidi, Na kama hakuna 5G kabisa test na 4G ya Halotel ufanye comparison na hao wengine.
 
Ufanyaji kazi ni mmoja, Microwave inasaidia kupunguza ping, 5G yenyewe by nature ina ping ndogo, uzuri wa 5G ni capacity hata kama mtakua wengi mtaani ngumu speed kudrop.

Starlink around 1.5m installation na kwa mwezi around 120,000 huku kwetu.
Habari Chief na wataalam wengine
Naombeni mnisaidie nimeambatanisha hapo na picha router yangu kila saa napata ujumbe kuwa connected without internet au network unstable..
Ni kampuni vodacom R20
 
Habari Chief na wataalam wengine
Naombeni mnisaidie nimeambatanisha hapo na picha router yangu kila saa napata ujumbe kuwa connected without internet au network unstable..
Ni kampuni vodacom R20
Connected without internet ina maanisha wifi ipo ila internet hakuna, mara nyingi hutokea hivi ikiwa internet imekata.

Hali hio hutokea vifaa vyote ama chako tu?
 
Kwa inategemeana na mahali ulipo kwani kuna maeneo mtandao A unashika sana wajati mtandao B unakuwa hafifu.

1.Fiber
Ndio chaguo lakwanza ikiwa upo maeneo yaliyofikiwa na mtandao wa fiber wa TTCL hasa maeneo ya mjini.Yapo makampuni binafsi yanasambaza fiber ila kwa gharama ya juu kidogo ukilinganisha na TTCL.

UZURI WA FIBER
*Ndio chanzo mama cha internet baada ya wire ndio ifuate wireless hivyo nisawa na kusema upo kwenye branch za mkongo wa Internet.
*Bei nafuu zaudi,Ikiwa na kima cha chini 55,000/= kwa 20 Mbps.
*Haiathiriwi na hali ya hewa.Ukizingatia inatumia wire toka chanzo hadi kwa mlaji hivyo changamoto za umbali,mvua,upepo nk havitokusumbua.
*Hamna Jam.Vifurushi ya unlimited hasa hivi vya kwenda kwa mlaji huwa ni shared network hivyo watumiaji wanapokuwa wengi kasi hupungua.Na hapo ndio utajua maana ya sentensi UP TO 10 Mbps,20 Mbps,30 Mbps nk wakimaanisha speed inaweza kuwa chini ya hapo ama ikafikia hapo.
*Free installation kwa TTCL kwa makampuni binafsi sijajua.

UBAYA WA FIBER
*Haihamishiki yani ipo fixed eneo ulipounganishwa hivyo huwezi kuhama nayo.
* Inachukua muda kuunganishwa kwa TTCL basi huchukua hata mwaka hasa vifaa vikiwaishia hawa sio wakuwategemea kabisa.Makampuni binafsi sijajua ila kama upo kwenye zone zao basi nisuala la wiki tu.
*Ipo limited.Inapatikana kwa wingi maeneo ya mjini kwa walio nje ya mji itakulazimu ugharamike nguzo na vifaa kufikishiwa yani nikama ilivyo kufungiwa umeme wa tanesco.
*Miundombinu kuharibika.Hasa kipindi cha mvua nguo kuanguka waya kukatika ndio kukatika kwa mtandao hadi waje kuunganisha tena.


ANTENA
Hii wanayo Vodacom na Airtel.Mfano huduma ya superkasa ya voda huwa wanaunganisha kwa kutumia antena maalum yenye kuwasiliana na mnara wao ulio karibu yako.Hii inakuwa na kasi moja tu ya 20 Mbps kwa 115000.
Airtel sijajua gharama zao upande wa antena.

UZURI WA ANTENA
*Antena hubust mtandao mana hufungwa nje ya jengo lako hivyo kunasa mawimbi kwa urahisi.
*Ndio utapata kifurushi cha 20mbps kwa 115000 upande wa voda kwa huduma ya supakasi.

UBAYA WA ANTENA
*Ipo fixed eneo lako ulipofungiwa.
*Inaweza kuathiwa na mvua,radi nk
*Lazima utangulize malipo ya miezi 2 ndio waje kukufungia ila pesa utarudishiwa baada ya kumaliza mkataba ikiwa hutaki kuendelea.
*Kwa voda kifurushi ni kimoja tu cha 2) Mbps.

ROUTER
Hapa kuna makampuni matatu voda,tigo na Airtel.
Vodacom wako na router 5G kwa kifurushi kinachoanzia 30 Mbps kwa 120,000.
Utalazimika kutanguliza kulipia miezi 2 ya kifurushi ukitakacho mfano 240000 kwa kifurushi cha 120000 ili usajiliwe.
Sababu ya sifa ya 5G hivyo vifaa vinapatikana maeneo yaliyofikiwa na 5G yao tu.

Airtel wako na router ya 5G kwa kifurushi kinachoanzia 10 Mbps kwa 70000...30 Mbps kwa 110000 nk
Utalazimika kulipia na 200000 ya kifaa (router)
Vifaa vinapatikana maeneo yaliyofikiwa na 5G yao tu.

Tigo wako na router ya 5G kwa kifurushi kinachoanzia 10 Mbps kwa 70000...30 Mbps kwa 100000 nk
Utalazimika kulipia kifaa router kitu kama 600000 hivi.

My take
Chukua router kulingana eneo ulipo ambapo mtandao husika suala la internet wapo vizuri.
Usidanganyike na neno 5G hii ni teknolojia tu ya usafirishaji mawimbi hivyo hata 4G inaweza kucover kifurushi chako.4G inaweza kufikia speed ya 100 Mbps - 150 Mbps huku 5G ikifikia 300 Mbps.
Hivyo hata kama upo eneo lisilo na 5G bado utapata mawasiliano kupitia 4G.
Zingatia sana 5G ikiwa unajiunga na 150 Mbps au zaidi.

*Vifurushi vyote na huduma zote ni unlimited yaani unatumia kwa kupimiwa speed sio GBs hivyo tumia uwezavyo.
*Kwa kuwa unlimited hii haimaanishi uunganishe marafiki na majirani wote kwenye WiFi yako kwa mtashea iyo speed uliojiunga.
*Ili kupata speed halisi ya kupakuwa file basi gawanya kwa 8 Mbps ulizojiunga.Namaanisha kwa mfano umejiunga kifurushi cha 10 Mbps inakuwa 10/8=1.25mbps yaani wakati unadownload basi speed iwe inasoma hadi kufikia 1.25 pale juu ya simu kwenye minara ya mtando na data connection ichezee hapo 700kbps-1.25mbps japo pia yaweza kupitiliza kulingana na eneo ulipo au wakati wa usiku.

Kwangu mimi kwa maeneo niliyopo ni best choice na kifurushi unaweza kubadili muda wowote yaani unacholipia ndio unachopatiwa.

TTCL panahitajika mkurugenzi mwenye uchungu na taifa na kuliinua shirika hilo la Umma linalouliwa na wachache fulanifulani.

Updates...
Tigo sasa wanatoa router zao kwa kulipia bando husika hivyo router inabaki kuwa mali ya kampuni...Hii inamaanisha ukilipia 100k kwa kifurushi cha 20mbps basi unapewa router ikiwa tayari na kifurushi husika.

Airtel ni wezi wanaambia watu router zao ni unlimited lakini ukweli ni kuwa ziko limited.Ukitumia hadi kufika kiasi fulani cha gb kulingana na kasi uliyojiunga basi wanakuwekea data cap yani wanapunguza speed hadi kufikia 2mbps mpaka pale muda wako uliobaki uishe au ununue upya.Haya nimeyajua kupitia mimi binafsi kuambiwa na huduma kwa wateja kuwa wako na user limit policy ambazo hawajaziweka wazi kwa wateja wao.Pia malalamiko yamejaa kwenye page zao mitandaoni.
Asante sana mkuu
 
Connected without internet ina maanisha wifi ipo ila internet hakuna, mara nyingi hutokea hivi ikiwa internet imekata.

Hali hio hutokea vifaa vyote ama chako tu?
Naelewa kuwa wifi ipo internet hakuna.
Lakini naona kama ni tatizo endelevu...
Tatizo hili linatokea kwa vifaa vyote.
Lakini nilishawahi kupata hilo tatizo mji fulani nchi fulani wenzangu wote wanapata wifi ila kwangu inagoma moaka naondoka.
 
TIgo na huduma yao ya fiber ni hovyo mavi matupuu, unalipa kama wanavotaka.....wakimaliza kuunganisha unaambiwa subiri password ndani ya masaa 24 uanze kutumia....leo ni wiki inaisha hakuna cha password wala ushuzi wowote....hawa jamaa wamezngua sana imagine wako serious kutembea na timu yao ile na magari mtaani kutujaza uongoo tu....tigo nyashiii maza fantaa nyiee🖕
 
TIgo na huduma yao ya fiber ni hovyo mavi matupuu, unalipa kama wanavotaka.....wakimaliza kuunganisha unaambiwa subiri password ndani ya masaa 24 uanze kutumia....leo ni wiki inaisha hakuna cha password wala ushuzi wowote....hawa jamaa wamezngua sana imagine wako serious kutembea na timu yao ile na magari mtaani kutujaza uongoo tu....tigo nyashiii maza fantaa nyiee🖕
Password ya router ama? Kuna mahusiano gani ya password na fiber? Sijaelewa?
 
Kutoka kwny fiber kuja kwny device yako konection inakuaje??
Kuna kua na Router ambayo ina ip adress, hio router ndio ina password ya kuingia kwenye router na password nyengine ya wifi, sema vyote viwili hivi sio necessary wewe kupata internet bali wifi. Mfano kama una desktop ama laptop Ina ethernet hata kama hujui password ya router kwa Ethernet cable itaconect na internet.
 
Back
Top Bottom