Mlipuko huu wa Rooters za WIFI kwa kampuni za Simu ipi ni nzuri Kwa matumizi nyumbani?

Na vipi kuhusu satellite Internet mfano hawa Konnekt wana program yao ile ya xpress wi fi vip kunamtu ashawahi deal na hizi mambo
 
Kwa shule hii,acha niwe nakesha JF.
Kongole sana na MUNGU akubariki ndugu.
 
Ufanyaji kazi ni mmoja, Microwave inasaidia kupunguza ping, 5G yenyewe by nature ina ping ndogo, uzuri wa 5G ni capacity hata kama mtakua wengi mtaani ngumu speed kudrop.

Starlink around 1.5m installation na kwa mwezi around 120,000 huku kwetu.
Kuna vijana waliagiza starlink devices ili waje kuuza bongo .. nasikia walikamatwa kwa kukosa vibali TCRA, Je, ni kweli?
 
Chukua Tigo au Airtel. Kasi yao ni nzuri, yaani unapata value for money; hali kadhalika pia bei yao ni nafuu ukilinganisha na Vodacom.
 
Kuna vijana waliagiza starlink devices ili waje kuuza bongo .. nasikia walikamatwa kwa kukosa vibali TCRA, Je, ni kweli?
Sina uhakika ila kama unauza ndio watakukamata, ila kama unalo matumizi ya nyumbani sidhani kama hata wana time na wewe. Niliwahi kuona mtu alituma picha humu NMB Namanga wanatumia.
 
Jamani hii kampuni ya simu Smile baso wapo? Kuna mini wi fi pocker router nimekikuta ofisini, kama wapo nikitumie
 
Kuna vijana waliagiza starlink devices ili waje kuuza bongo .. nasikia walikamatwa kwa kukosa vibali TCRA, Je, ni kweli?
No kweli kuna story humu jf na picha zao msijiletee matatizo not worth it.
 
Mrejesho wakuu. Tuishi na router ipi kwasasa yenye unafuu? Unlimited data package.

-Kaveli-
 
Vipi kuhusu universal routers, ipi ni the best? Bei zipoje? upatikanaji wake?

-Kaveli-
 
Chukua Tigo au Airtel. Kasi yao ni nzuri, yaani unapata value for money; hali kadhalika pia bei yao ni nafuu ukilinganisha na Vodacom.
Tigo ni lazima kila mwezi ununue kifurushi chake kwa miezi 24 (non stop) usipofanya hivyo deni lako la mwezi husika litawekwa siku ukinunua kifurushi kuyakataa kulipa deni. Mfano kama umechagua kifurushi cha laki 1 kwa mwezi ni lazima kila mwezi ulipe laki 1 hadi miezi 24 iishe baada ya hapo utajua unaamua ununue au usinunue

Ujinga wa Tigo router haupewu siku hiyo hiyo itakubidi usubiri siku 13 hadi 20 hata mwezi ndiyo upewe router eti wanafanya setting

Airtel wao hawafanyi hivyo ununue au usinunue. Hawana shida. Yaani utanunua kifurushi ili ukitumie kuisha muda wake kutakata siku ukinunua wanaanza kuhesabu hiyo siku .. gharama ya router za Airtel ni nafuu sanaa sanaa unapewa bure gharama ni kifurushi
Airtel router unapewa siku hiyo hiyo.

Kuhusu speed chagua Router ya mtandao unaondoka vizuri kwenye Eneo lako .

Kwa waliopo Dar siyo sehemu zote kuna 5G hivyo speed haitakuwa sawa hasa kwa wale wenye uhitaji wa kupakua file kubwa kubwa .

Sina uzoefu na Tigo katika speed sana

Airtel kuna wakati speed inakuwa chini sana haijalishi kasi ya kifurushi chako .
 
Shukrani mkuu
 
Nchi yetu bado internet ni zengwe Tu hizo router za mitandao ya simu ni wezi mpaka basi ukitumia router maumivu na ukiweka bundle la kawaida ndio maumivu mara mbili
Wanakuumiza kwenye spidi ukilipia utapata speed ya Kasi Kwa siku 3 za mwanzo baada ya hapo ni usanii tu
 
Mtandao gani hao
 
Tangu mwaka jana mwezi wa nane natumia Vodacom 5G kifurushi cha 30Mbps kwa kweli ni internet ya uhakika sana, sijui mitandao mingine ila voda is unmatched
 
Inategemea ulijiunga huduma gani, kama ni ile ya Antena inatumia Microwave signal, lazima ziwepo.

Nafkiri huduma zote za 5G hazina hii limitation.

Airtel watu wananunua mjini na kutumia mkoani.
Kwa maana hiyo hata kama eneo langu sina 5G mkoani, nikichukua airtel ya 5G itaoperate 4G fresh tu?
 
Mkuu,
Kwa uzoefu wako kwenye hizi router za 5g kwa haya makampuni ya simu yote, kampuni gani inayotoa best 5g router in terms of quality of brand and service. Najua hili liko technical zaidi especially kwenye hardware part. It's something am eager to know before I make purchase decision.
Binafsi ninapoishi nimetest 4g zote kwa maana ya Airtel Tigo na Voda na so far nimeona kwa hapa kwangu zina respond vizuri tu.
Kinachonisukuma kwenda kununua 5g router ni kifurushi cha unlimited kwa sababu matumizi yangu ya kawaida nikinunua limited bundles zinaisha haraka sana.
Ntashukuru kwa majibu yako kwenye haya maeneo niliyouliza. Thanks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…