Mlipuko mkubwa watokea mji mkuu wa Lebanon, Beirut. Watu zaidi ya 78 wafariki na zaidi ya 4,000 kujeruhiwa

Hezbollah Ni kijikundi tu hapo Lebanon. Washapasuliwa Mara kadhaa ila hawakomi
Ni kweli hawa ni vigilante group ila cio wadogo km unavyofikiria mkuu.silaha kubwa ya vita ni hari "spirit" ya wapiganaji wako.
 
Naamini ni utunzaji mbovu wa silaha kwenye ghala. Anayesema ni Hezbollah, hawa hawana makazi eneo hili la Beirut wao wako field za nje ya miji uko na juzi hapa Israel imedai wana roketi zimeelekezwa kwao.
Ajari itakuwa ni kutokana na depot ya milipuko maana tumeona rangi za mafataki kwanza kisha mlipuko mkubwa. Kuwepo kwa mushroom cloud na shockwave kunafanya iwepo imani ya some sort of nuclear warhead ndogo sana.

Hata hivyo kuna uwezekano Israel anahusika kwa kujishikiza kwenye uzembe wao. Maana bandari hupokea baadhi ya silaha kutoka Iran kwenda Hezbollah lakini mara nyingi wanatumia mpaka wa Syria ambao hushambukiwa sana na Israel.

Taarifa za awali za serikali zinaonesha ni ajari, ingekuwa shambulizi Hezbollah wangeshajiapiza muda mrefu. Israel hapendi vita hata wiki iliyopita wapiganaji wanne wa Hezbollah waliingia mipakani lakini command ya jeshi ikaomba ruhusa ya kushambulia kwa Netanyahu akakataa ikabidi wawaache watoke. Ukishambulia Hezbollah wanajibu, hii sio Gaza ambako hawana technology ya kujitutumua. Mwaka 2006 kulitokea upinzani mkali dhidi ya Hezb, mwaka 2013 wakati Israel anashambulia Gaza strip walikuwa wanajibu na viroketi vichache. Hezb ina mkono wa Iran, ina engineers, technicians, commando unit, na roketi za masafa ya kati. Ni jeshi lisilo na mamlaka kamili na lisilo rasmi lakini lenye nguvu kuliko jeshi la nchi. Ni kama Iran (walimu wao) ilivyo na IRGC na jeshi la nchi.
 
Wakuu tufunge huu mjadala sasa.wengne ni wajumbe wa heshima MMU na kule chini ya mbali
 
انا لله وانا اليه راجعون Allah awape qauli thabit!

Poleni sana ndugu zetu, Allah awape subra wote mliofiwa, majeruhi Allah awape shufaa ya haraka waweze kupona.
 
Huko mashariki ya Kati Nchini Lebanon ,Maeneo ya Beirut Kumetokea Mlipuko mkubwa na kusababisha Vifo zaidi ya 70 na wengine zaidi ya 3200 kujeruhiwa Vibaya, kwa mujibu wa Maelezo ya Waziri Wa Afya.

View attachment 1527396
Kwa mujibu wa Jenerali Wa Ulinzi wa Lebanon Bwan Abas Ibrahim amesema kuwa Mlipuko huo umetokea maeneo ya Bandari ya Beirut na sababu kubwa ni uwepo wa Tani 2700 za Ammonium Nitrate zilizokuwa zinatakiwa Kusafirishwa Barani Afrika

Kwa upande wa Serikali ya Uturuki raisi wa Nchi hiyo bwana Tayyip Erdogan amehaidi kutoa Msaada wa Kibinadamu pale utakapohitajika

Wenye upadate zaidi watupatie

Source: Aljazeera
View attachment 1527395
 
Duuh, si mchezo. Hivi lile gorofa pembeni pale lillikuwa na watu bila shaka.

Ila huu mlipuko ulikuja baadae, inaonekana kama kulitokea hitilafu fulani hapo kabla, maana kama kulikuwa kuna moto mdogo umeanza hivi.
Mossad noma sana Kama nuke bomb yani
 
Hapo ndipo utapoona umuhimu wa kuratibu uagizwaji, utunzajwi na usafirishaji wa kemikali hatari na milipuko zinazoweza kutishia usalama wa maisha, mazingira na mali .

Kwa Tanzania mamlaka kama OSHA Occupational Safety and Health Authority Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania KAZI ZETU | TAEC , Idara ya Customs / TRA, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na TPDF zinatakiwa kufanya kazi za ukaguzi na kwa ukaribu na wananchi ili kuona miongozo ya usalama inazingatiwa na wote pia kuratibu bidhaa zenye uwezekano wa kulipuka, kuumiza kama sumu au kemikali n.k

Mlipuko huu wa Beirut Lebanon ni somo kwetu wote kutochukulia kwa wepesi usalama wetu iwe kemikali za mercury, sulphuric acid, mbolea za kemikali, baruti , ma cylinder ya gas za majumbani na viwandani, oxygen cylinder , gesi za kuchomelea vyuma n.k

Siku zote tunapotumia bidhaa za hatari tushirikishe taasisi na mamlaka zinazohusika ili zitushauri namna bora ya kutumia, wingi wa kuhifadhi, maeneo salama ya kuhifadhi na usafirishaji wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…