Mlipuko mkubwa watokea mji mkuu wa Lebanon, Beirut. Watu zaidi ya 78 wafariki na zaidi ya 4,000 kujeruhiwa

Mi naomba Israel awe hajahusika,maana hao hezibullah kwa hiyo michezo ni hatari sana,halafu walipuaji wa vikundi vidogo hawawezi kuwa na bomu la tani kubwa kiasi hicho,hapa labda ni nchi fulani imefadhili...
 
Hahahaha mwenye Mbwa Iran mpaka leo hii haijajibu kitu sembue huyo
IRAN ajibu nini kuna siku umesikia ISRAEL kaigusa IRAN [emoji23][emoji23][emoji23] akijitia ujinga wakuigusa mchana usiku mtaitafta nahamtakaa muione ilipo

Israel adil na hamas nakwambia nanakuhakikishia akijulikana kahusika hatakwapunje yamtama atateseka mnoooo.....
 

Unalipua ukiwa kitandani au wp[emoji3]
 
Unaweza kutuwekea ushahidi?
Wale watu manne walioingia mipakani Israel iliwafyeka hawajaachwa
 
Iran lazima akomalie hiyo show maana hizbolah ni derivative yao, na mfaransa ni muuza bidhaa za nyuklia wa siri mashariki ya kati.
 
Israel was ruled out. Tangu mwanzo Israel huwa haina bifu na Lebanon bali ina bifu na Hezbollah. Hezb yenyewe iliomba kuwepo umoja katika tukio hili, hawajajiapiza kama wanavyofanyaga mara zote. Maana yake mpaka wao wanaamini ni ajari, ingawa najua wanachunguza kivyao.

Mkuu wa Usalama na Waziri Mkuu wamesema kulikuwa na ammonium nitrate tani 2750 zimehifadhiwa kwenye ghala kwa kipindi cha miaka 4-6. Hizi hutumika kutengeneza mabomu na mbolea, nyingi serikali ilikuwa inazikamata kama magendo. Kuna uzembe wa mamlaka za bandari. Mafataki pia yalikuwepo, moto ulianza kwa namna nyingine ndipo ammonium nitrate ikalipuka. Chanzo cha huo moto wa mwanzo ambao ulikuwa unatoa flash nyeupe za mwanzoni ndo bado kujulikana. Kuna mchanganyiko wa explosive substances maana ni kama warehouse ya milipuko ya aina yote. Ndo maana kuna moshi mweupe, yellow, na rangi gani sijui.

Naamini nchi nyingi zitatoa msaada maana Lebanon ni ndogo. Israel yenyewe imesema ina mazungumzo kupitia third party kutoa msaada. Qatar inatuma vitanda vya dharula kwa majeruhi, Saudi Arabia inakuja, Turkey, Iraq na wengine.
Trump kama kawaida yake anatoa taarifa bila uhakika, alidai inaonekana ni shambulizi. Kauli yake itapuuzwa.
 
mi naomba israel awe hajahusika,maana hao hezibullah kwa hiyo michezo ni hatari sana,halafu walipuaji wa vikundi vidogo hawawezi kuwa na bomu la tani kubwa kiasi hicho,hapa labda ni nchi fulani imefadhili...
Iran anaemfadhili Hezibullah kila siku analipuliwa sehemu zake nyeti na hajalipia mpaka sasa.
 
Wale watu manne walioingia mipakani Israel iliwafyeka hawajaachwa
Taarifa za Israel zinasema zimewaacha, intelligence ya Iran inasema wameachwa, wewe unasema hawajaachwa.

Israel nowadays haiui members wa Hezbollah, kwakuwa wanalipiza. Kwa kipindi hiki Netanyahu ana maandamano, serikali bado haijatengamaa, alikuwa na annexation plan, kuna US election na uchumi mbovu. Ikitokea mapigano yoyote raia watalaumu sana. Hezbollah wanajua hili, Iran wanajua na Israel inajua kuwa wanajua. Ndiyo maana Iran na Syria siku hizi zinawachukua wapiganaji wa Hezbollah kisha zinaifanya Israel ijue, Israel wenyewe wanaita hii mbinu "new antiaircraft weapon".

Hao jamaa wanne waliingia kisa shambulizi moja lililoua member wao, walipoonekana vikosi vikaomba ruhusa ya engagement ambayo ilifika mpaka kwa Waziri Mkuu, hii haitokei siku za nyuma kanali tu alikuwa anaruhusu kushambulia mtu yeyote mwenye silaha akivuka mpaka. Polisi wanaua Wapalestina wanaoandamana lakini jeshi linajitahidi kukwepa kuua Hezbollah mpaka PM mwenyewe hataki mzozo.

Hata Hezb yenyewe inajua kuna uchumi mbovu wakianza mapigano wataamsha hasira za raia.
 
Ukiutazama mlipuko huo video yake ina viashiria kuwa ni ya kutengenezwa:
Mosi: moshi unaoanza kufuka unaashiria kuwa ni mlipuko wa bomu la atomic, sidhani kama ni rahisi kwasasa (ethically) kwa jeshi kutumia bomu la ainahii.

Pili: mlipuko wa chini unaonesha kama ni bomu la kawaida tena la kutegwa na si la kutupwa. Combination hizi mbili zinashiria kuwa video ni ya kutengenezwa. Period.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…