Mlipuko Beirut: Serikali ya Lebanon yajiuzulu huku ghadhabu ya umma ikiongezeka
Serikali ya Lebanon imejiuzulu huku ghadhabu ya umma ikiendelea kupanda nchini humo juu ya mlipuko uliotokea Jumanne ulioharibu sehemu ya mji wa Beirut na kuwaua watu 200.
Tangazo la kujiuzuli lilitolewa katika televisheni ya taifa na Waziri Mkuu Hassan Diab Jumatatu usiku.
Watu wengi wameiutuhumu uongozi wa nchi kuhusika na mlipuko huo kwa madai ya uzembe na ufisadi.
Waandamanaji wameingia mitaani na kukabiliana na polisi kwa siku ta tatu mfululizo.
Mlipuko mkubwa ulisababishwa na kulipuka kwa tani 2,750 za mbolea ya ammonium nitrate iliyowekwa bila kuzingatia usalama kwenye ghala kwa miaka kadhaa bila
Rais Michel Aoun ameiomba serikali iendelee kushikilia mamlaka kwa muda hadi pale serikali mpya itakapoundwa.
Waziri mkuu alisema nini?
Bwana Diab, ambaye aliyeteuliwa kama waziri mkuu Januari baada ya miezi kadhaa ya mkwamo wa kisiasa, alisema kuwa serikali "serikali imefikia mafanikio makubwa ya kandaa mpango wa kunusuru nchi ".
Lakini ufisadi nchini Lebanon "ni kubwa kuliko taifa" lenyewe, na "kuna ukuta mkubwa unaotutenga na mabadiliko, ukuta wa watu ambao wanatumia mbinu chafu za kupinga na kuhifadhi maslahi yao", alisema .
"Walifahamu kuwa sisi ni tisho kwao, na kwamba mafanikio ya serikali hii yanamaanisha mabadiliko halisi miongoni mwa tabaka hili la watu waliotawala kwa muda mrefu ambao ufisadi wao umeiathiri nchi ,"aliongeza
"Leo tunafuata utashi wa watu katika madai yao kuwawajibisha wale waliohusika na mkasa ambao ulijificha kwa miaka saba, nia yao ya mabadiliko halisi," Alisema Bwana Diab.
Waandamanaji wakirusha fataki mjini Beirut siku ya Jumatatu
Nini kitakachofuata?
Katika hotuba waziri mkuu alijionyesha binafsi kama kiongozi mwanamageuzi aliyekwamishwa na janga la ufisadi lililokita mizizi tangu mika kadhaa ya nyuma , anasema mwandishi wa BBC wa Mashariki ya kati Tom Bateman.
Bunge sasa litatakiwa kuamua juu ya Waziri Mkuu mpya -mchakato utakaohusisha siasa zilezile za kimaeneo ambazo ndio mzizi wa maandamano, anaongeza mwandishi wetu.
Hautakua mchakato rahisi na wa haraka kutokana na mfumo wenye utata wa siasa za nchi.Mamlaka nchini Lebanon yanagawanywa baina ya viongozi wanaowakilisha makundi ya dini mbalimbali.
Zaidi ya hayo, kufuatia mwisho wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kati ya 1975-1990 idadi kadhaa ya wababe wa kivita waliingia katika siasa nab ado wanadhibiti sehemu kubwa ya siasa, uchumi na sekta za kijamii.
Waandamanaji wengi wanalaumu mfumo mzima wa uongozi wan chi kwa ufisad.
Jumatatu polisi walikabiliana na wakazi wenye hasira huku maandamano yakiendelea katika mji mkuu baada ya kujiuzulu kwa serikali.
Picha zilionyesha waandamanaji wakikusanyika karibu na vizuizi vilivyowekwa kwenye barabara ya kuelekea kwenye jengo la bunge huku vikosi vya usalama vikiwafyatulia gesi za kutoa machozi.
Beirut imeathiriwa vipi na mlipuko?
Idadi ya vifo vilivyotkana na mlipuko wa wiki iliyopita imepanda hadi watu 220 huku watu 110 wakiwa bado hawajapatikana, gavana wa Mji wa Beirut Marwan Abboud alinukuliwa akisema na mtandao wa habari wa al-Marsad nchini humo.
Polisi wa kukabiliana na ghasia walilazimika kutumi vitoz amachozi kuwatawanya waandamanaji mjini Beirut
Wafanyakazi wengi wa kigeni na maderva wa malori walikua ni miongoni mwa watu ambao hawajulikani walipo, aliiambia Televisheni ya Al Jadeed.
Nini kilichotokea kabla ya kujiuzulu kwa serikali?
Hali ya kutoridhika nchini Lebabon limekua ni jambo linalotokota kwa miaka mingi. Hivi karibuni 2019, mpango wa kulipisha ushuru simu za Whatsapp lilisababisha maandamao makubwa dhidi ya hali mbaya ya uchumi ina ufisadi, ambayo hatimae yalisababisha kujiuzulu kwa serikali.
Virusi vya corona vilikua vimezuwia maandamano, lakini hali ya kiuchumi imeendelea kuwa mbaya zaidi na mlipuko wa Jumanne iliyopita ulionekana na wengi kama ni matokeo mabaya ya ufisadi ya miaka mingi na uongozi mbaya.