G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Nimelazimika kuandika bandiko hili baada ya statements kadhaa zinazotoka kwenye mataifa mengine zikionyesha kuwa watanzania wamekuwa wakipita kuvuka mipaka na baadhi yao kwenda kuwa sasa ni chanzo cha matatizo ndani ya mataifa hayo.
Ni jana tu mtendaji mkuu wa wizara ya afya ya Kenya alitoka na kuripoti visa vipya 5 vya ugonjwa wa COVID 19 huku watatu kati yao wakisafiri kutokea Tanzania. Hatujui watu hao pengine walisafiri kutokea wapi? Kwa kutumia usafiri gani? Walipitia mpaka upi? Wenye dhamana wapo kimya?
Ni aibu kubwa kuwa sisi hapa nchini tunapima watu na kufuatilia waathirika kwa kujivuta sana huku ikiwa ni kama tunalazimishwa kufanya hivyo. Aidha kama nchi tumeonyesha uzembe wa kukusudia kupambana na janga hili. Kuanzia kauli ya Rais mwenyewe, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na watu wengine zinaiacha Tanzania kama nchi ya mzaha mzaha kwenye hili.
Ni lazima kama nchi na baadhi yetu tunaoelewa mambo tukiri kuwa serikali ya awamu ya tano imekuwa haijali pale linapotokea janga sehemu fulani ndani ha nchi. Hili nalo ni pigo kubwa na la fedheha kwa watanzania hasa tukitazama namna ambavyo serikali zilizopita zimekuwa zikikabiliana na majanga. Hivyo ni lazima mtu mmoja mmoja kwenye jamii kiliangalia hili kwa umakini mkubwa huku tukijikumbusha kuwa linapotokea janga (huko nyuma) watu tunaachwa tujipambanie kivyetu. Akili kumkichwa, ukizembea umeachwa!
Nalazimika kuandika haya baada pia ya kufuatilia yanayotokea Guangzhou China baada ya kukutana na kisa hiki cha mwana Jf aishiye huko.
Haya yanaanza baada ya China kugundua kuwa imported cases za COVID 19 kwa sasa zinatokea Afrika. Watu wataanza kuangalia nani anayezembea na kupeleka maambukizi kwa wenzao. Wakianza hivyo baada ya hasira za kutokana na kushindwa kufanya mambo ya msingi kwa kufungiwa, aidha kupoteza ndugu na marafiki basi tutajikuta tukikabiliwa na changamoto ya kubaguliwa. Lazima kama nchi tuonyeshe mshikamano na wenzetu na kuonyesha kujali juu ya janga hili.