nchi za Africa kuanzia Ivory coast, ghana, Kenya, Rwanda, etc wametoa Bail out kwa makampuni na wananchi. Janga la corona linaumiza afya na uchumi wa wananchi. Nchi zinginezo Africa zinatoa unafuu wa kodi mbalimbali, na kugawa chakula kwa wananchi masikini. Tanzania ni kisiwa, ni tofauti. Serikali inaomba wananchi bailout..!!! Mahokaa Yaani Serikali ya Tanzania inaomba wananchi msaada.
Lingine la kushangaza: Mawaziri wa Tanzania, maofisa wa ngazi za juu, sio wazalendo hata kidogo. Mpaka sasa sijasikia kuwa wamejitolea nusu mshahara ili kusaidia katika janga la Corona. Uzalendo wao uko wapi? Ona Kenya, Uganda, Rwanda na kwingine. Spika Ndugai hajatoa mwongozo, wabunge wakatwe shs ngapi...
Haya, basi, enendeni kule Twitter mkapambane na Waziri wa Majoka na Chatu...na kujibu hoja za CAG ...
Kama una povu, ruksa.