Wenye ugonjwa wa "uKondoo wa Nyerere" bado tupo wengi, hata tukikanyagwa tunashangilia, likimpata jirani yangu nasema hilo ni lake. Ukisema mfalme kakaa uchi tunakuambia wewe ni mtukanaji na mchochezi. Ukiandamana tunasema unafanya vurugu. Ukiikosoa serikali tunakuita msaliti. Upinzani ukipigwa dafrau tunasema hao watukutu ni stahiki yao. Neno haki hatulitamki tujualo ni neno amani lazima ilindwe kwa nguvu zote. Wengi wetu humu JF tunaugua ugonjwa huo-tukisha piga kelele tunalala, ingawa kupiga kelele ni dalili ya kwanza kuanza kupona ugonjwa huo.
Tukipata viongozi mkakati na kwenda nao sambamba huu ugonjwa waweza pona hata kama sio mara moja. Hata hivyo hakuna ajuae kesho yake.