Mlo mwepesi wa haraka

Amin amin nawaambia, mwanaume anayeweza kumenya ndizi na kuzipasua kabisa kama huyu, kuoa ni historiaπŸ˜„πŸ˜„
πŸ˜‚ huwa napika sana ila hiyo steji aliyofikia huyo jamaa hapana, kuna siku nimeletewa ndizi nikaona zisiaribike nizimenye, nikaenda kununua vile vifuko vya mia vinne nikavivaa, nilichonga mbili tu nikasema hii kazi hapana bora ziive nitazila mbivu.
 
πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ zikaiva
 
Mkuu mimi mwenyewe napika sana tu ila katika vitu vimenishinda ni ndizi. Naweza kusema hicho ndio chakula ambacho hata kupika sijawahi kujaribu kwasababu ya hiyo kazi ya kumenya. Sasa nikicheki jinsi mwamba alivyoimenya ndizi, kaikwangua imekua nyeupe na kaipasua kitaalamu πŸ˜€πŸ˜€ huyu jamaa akioa niiteni mbwa niko apa nimekaa.
 
Hana hata mpango huo wa kuoa, waoaji hawamenyagi ndizi πŸ˜‚
 
Mbona mambo madogo hayo πŸ˜‚
 
Ungeweka Nazi natural mkuu, mbona unaishi mazingira mazuri natural Ila unatumia vifaa fake , mfano ilifaa utumie chungu kabisa sio sufuria,mwilko wa mbao jambo zuri, Ila usizidishe sana nyama hata kwa wiki mara moja inatosha red meat
 
Mchaka wokui?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…