Mlo wa wiki (Health Diet)

Mlo wa wiki (Health Diet)

Yummie

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2015
Posts
1,363
Reaction score
1,081
Habari zenu wanaJF
Hii ni ratiba ya mlo kwa wiki nzima kwa ambao wanapenda kuwa na afya bora pamoja na kujiepusha na baadhi ya maradhi na magonjwa kwa kupitia mpangilio mzuri wa vyakula.

Jumatatu:
Asubuhi- mayai ya kukaanga pamoja na baadhi ya mbogamboga zilizopikwa kwa siagi(butter) au mafuta ya nazi.

Mchana; Changanya mtindi/strawberries au blue berries pamoja na almonds saga kwenye blender kisha kunywa (smoothie).

Usiku; Cheese burger iliwe na mbogamboga na salsa sauce.

Jumanne:
Asubuhi;bacons and eggs

Mchana;brown bread na mboga za majani.

Usiku; Samaki,butter na mbogamboga.

Jumatano:
Asubuhi; mayai ya kuchemsha na mbogamboga

Mchana;Salad ya samaki aina ya kamba waliopikwa kwa olive oil.

Usiku; kuku choma na mbogamboga

Alhamis:
Asubuhi;omelet na mbogamboga

Mchana;Chicken salad iliyoandaliwa na olive oil.

Usiku;Nyama especially steak na mbogamboga.

Ijumaa:
Asubuhi;bacons and eggs

Mchana;Smoothie(saga strawberries tui la nazi almonds na protein powder.)

Usiku;Nyama na mbogamboga

Jumamosi:
Asubuhi;omelet na mbogamboga

Mchana;smoothie

Usiku;meatballs na mbogamboga.

Jumapili:

Asubuhi; bacons and eggs

Mchana;smoothie

Usiku;Chicken wings zilizookwa na mboga za spinach.
 
Hebu ngoja kwanza......
Hii inanihusu na mimi wa huku Yaeda au ni nyie wa mjini tu...........

Hahahahaha Yoyote yule,ukiona una access na hivyo na unamudu,there you are
 
hiyo siyo diet, ni murundikano wa fatty food. mwezi mmoja tu mwili pipa
 
Kwani huko kwenu bacons zinapatikana preta hahahahaha

Sisi huku kwetu chakula kikuu ni nyama ya nyani........ugali.....matunda na mangure......kidogo na buzaa.......ukituona tulivyo na afya.......wanaume wote wana six pack.......
 
Hebu ngoja kwanza......
Hii inanihusu na mimi wa huku Yaeda au ni nyie wa mjini tu...........

Ugali, wali, mihogo, kisamvu, mchicha na ndugu zake usile. Ni sumu!!

Baada ya kusema hayo nakukumbusha usihangaike na matunda utapata kansa.

Bia ni anasa za dunia.... kunywa Grants kwa wingi kwa afya ya maini yako.

Tukutane njia panda ya Himo kujadili hii ilani ya afya ya 2015.

Chagua Lowassa kwa afya yako.
 
Ugali, wali, mihogo, kisamvu, mchicha na ndugu zake usile. Ni sumu!!

Baada ya kusema hayo nakukumbusha usihangaike na matunda utapata kansa.

Bia ni anasa za dunia.... kunywa Grants kwa wingi kwa afya ya maini yako.

Tukutane njia panda ya Himo kujadili hii ilani ya afya ya 2015.

Chagua Lowassa kwa afya yako.

Mihogo otee......sili muhogo.........
Hebu fanya haraka tukutane mara moja..........
 
Mihogo otee......sili muhogo.........
Hebu fanya haraka tukutane mara moja..........

Mihogo kaondoka nayo Dokta. Hata ungeitaka ungeipatia wapi??

Mi natia timu next month.... ole wako nikukose.
 
Back
Top Bottom