"MLOKOLE" ananitia majaribuni!

"MLOKOLE" ananitia majaribuni!

Mkuu,

Mungu yupo makanisa yote, hata huko alipo yupo. Sasa ulazima wa kwenda anakosali dada ni upi? Au kuna lingine zaidi ya kusali? Akijitokeza dada mwingine wa dhehebu tofauti nako aende?? Akijitokeza mwingine na mwingine aende kote huko?? Ya nini kuhangaika huku na kule? Atulie ktk kanisa lake, na wokovu ni matendo, sio kusema tu NIMEOKOKA. Mtu anaokoka kutokana na matendo yake, na sio dhehebu lake. Hivyo hata wakatoliki wanaokoka thru matendo yao.
Kwa kumalizia nasisitiza jamaa abaki anakosali, kusoma bible, wokovu, n.k vyote atafanya akiwa RC.
Mkuu,
Niliposema aende pia kanisani kwa dada basi ni kutokana na kujuwa kuwa Mungu yupo makanisa yote. Pia ni katika kupanua wigo na kujenga mapenzi katika jina la bwana. Huko hukuiti "kuhangaika". bali ni kuitika wito.
kama ataweza kwenda makanisa 100 basi aende tu hata kama hatakaribishwa na akina dada. ndio katika kujenga umoja na mapenzi huko.
 
Mungu ni mmoja, imani ndio inatakiwa hiyo kutaka kukubadilisha ni pumba unaweza kuwa kanisani kwako ukaokoka pia, je mmefikia wapi sasa ni January? au ulimwambia utamuoa, du kama anaanza kabla ya ndoa hivi mkioana itakuwaje? au lazima kwao kaambiwa aolewe na mtu wa dhehebu lake
 
Kasha, hebu tufahamishe vizuri au kama bado hujamsoma huyo dada basi jaribu kufanya hivyo tujue kama ana ajenda gani zaidi ya kusali, then ndo naweza kutoa ushauri mzuri zaid.

Lakin kwa angalizo tu, endelea kukamua RC
 
Mungu ni mmoja, imani ndio inatakiwa hiyo kutaka kukubadilisha ni pumba unaweza kuwa kanisani kwako ukaokoka pia, je mmefikia wapi sasa ni January? au ulimwambia utamuoa, du kama anaanza kabla ya ndoa hivi mkioana itakuwaje? au lazima kwao kaambiwa aolewe na mtu wa dhehebu lake

Dada huyo anajua kuwa nimeoa na nina watoto. Mbaya zaidi, kama ni kutaka kuleta wokovu katika familia, hajishughulishi na mke wangu. Meseji zote ni kwangu tu. Yeye alianza kwa kuniambia kuwa nikitaka baraka zaidi niokoke.
 
Chunga sana maamuzi utakayofikia siku hizi mitego kila mahali. Kondomu moja kwa kila tendo ndiyo itakuokoa. Acha ngono zembe.okoka umrejee yesu.
Kazi kwako.
Nilidhani angeikimbia zinaa na kujificha kwenye ngome YESU ambaye ndiye wokovu , kuliko kujichimbia kwenye wokovu wa kondomu !!!
 
Chunga sana maamuzi utakayofikia siku hizi mitego kila mahali. 1.Kondomu moja kwa kila tendo ndiyo i(takuokoa???). Acha ngono zembe. 2.okoka umrejee Yesu.
Kazi kwako.

Nichukue lipi kati ya mawili? Ila nina uhakika kondomu haileti wokovu.
 
Nichukue lipi kati ya mawili? Ila nina uhakika kondomu haileti wokovu.

ukienda kwenye mzinga unategemea kuwa utapata asali pia nyuki wanakuuma tu. Na pia si mizinga yote ina asali na nyuki, mingine haina asali ila ina nyuki tu. ila palipo asali lazima pana nyuki. Tia akili mu kichwa.
 
Back
Top Bottom