Mlundikano wa michango makanisani itafanya watu warudi kuabudu mizimu ya kwao

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
5,168
Reaction score
8,982
Wakuu huu ni ubashiri tu, muutunze huu uzi.

Hatuna miaka mingi kabla hatujafika hapo.

Michango imekuwa mingi mno.

Inabadilishwa majina tu.

Mingi haipo hata kwenye maandiko.

Tunakoelekea itakuwa gharama sana kuwa msharika.

Itakuwa ni heri uende vichakani ukaililie mizimu ya kwenu.
 
Toa sadaka zote toa na fungu la kumi basi.
Siku hizi matangazo ya michango kanisani mengi kuliko ibada.
 
Ujinga wenu tu waumini wa kisasa. Mnarundikiwa mamichango haya na mnatoa ili kuwa washarika wazuri eti siku mkifa mje mzikwe vizuri kiimani. Kwani hata ukizikwa na halmashauri ya jiji au ukatupwa porini ukaliwa na wanyama huko kuendeleza food chain wewe marehemu inakusaidia au kukuathiri kivipi? Kama uko sawa na Mungu wako mbinguni si utaenda tu? Kuna mtu atakosa kwenda mbinguni kisa eti hakutoa mchango wa jengo la kanisa au hakuzikwa kikristo? Shwaini kabisa! 🚮
 
😅😅😅😅😅

Upo sahihi mkuu
 
Hausaidiw na kitu chochote ni hofu zetu tu.
Ila michango me kama ninayo natoa kama sina sina Cha kutoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…