Mmarekani wa Tandale akiwa kwao Marekani na wenzake

Mmarekani wa Tandale akiwa kwao Marekani na wenzake

Jamaa yuko vizuri...kapiga hatua kubwa, tupunguze wivu tuendelee kupambana, huo ni mti wenye matunda
 
Sio Lugha yake hata akina snoop wanaelewa kwanini jamaa mdomo mzito
 
Siku ya kwanza kuongea na hao wa mbele ilikuwa na ja rule, badae ikawa na fifty Cent nikajifunza kitu heri kuongea na mzungu tu mweupe sisi watoto wa Kigogo Wenye elimu elimu za kuunga unga inahitaji sana masikio na kuisoma midomo ya black america ili uwe confortable akizungumza
 
Ila kingereza ua chepes sana ukiwa unaongea pekeako ngoja usemeshwe sasa ndio unaishia na yeees yesss
 
Ila kingereza ua chepes sana ukiwa unaongea pekeako ngoja usemeshwe sasa ndio unaishia na yeees yesss
Siku za mwanzo mwanzo wakati nimefika South Africa nilikuwa sisikii chochote kwenye tv ila watu nikiwa naongea nao ana kwa ana nawaelewa mpaka nikawa najishangaa how come kingereza cha kwenye tv sikielewi? ila baada ya muda atena ikanasa nikawa nasikia hata nikiwa chumbani na tv iko sebleni. Kiingereza huwezi kuwa fluent kama hujaishi na waongea kiingereza kama mother tongue kwao au first language kwao. So Diamond anajua maneno machache sana ya kingereza, ukimuweka kwenye mdahalo lazima maneno yote yamuishie.
 
Four language skills you need to master, namely: 1. Lestening skills, writing skills, reading skills, and speaking skills.

Sasa, Diamond na Mtanzania yoyote anaweza kuongea fluent English akiwa peke yake (One way), lakini akapata ugumu katika mazungumzo na mzungumzaji mzawa wa Kiingereza (Two ways), kwa sababu ya poor listening skills. Hii ni kutokana na kutozungumza na wazungumzaji wazawa wa Kiingereza mara kwa mara.

Hapa Tanzania, tunazungumza Kiswahili kwa asilimia kubwa ya maisha yetu ya kila siku, hivyo tunakosa English Listening Skills.

sasa Diamond kakutana na muhuni Snoop anongea Kiingereza cha wanamuziki, kamwe Diamond hawezi kufua dafu.

Nilifanya utafiti kidogo, marais wa Marekani huwa wanajitahidi kuzungumza Kiingereza rahisi sana. Itakuwa wanajua kila siku wanaingia Wamarekani, ambao hawajaimudu vyema Lugha ya Kiingereza.
 
Ila kingereza ua chepes sana ukiwa unaongea pekeako ngoja usemeshwe sasa ndio unaishia na yeees yesss
Vile ukimsikia barack obama anaongea bas na ww kimoyo moyo unaongea kiingerza cha Barack Obama 😄ongea sasa usikike ndo utajua hujui😂😂😂
 
Back
Top Bottom