MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
Wengi wenu hapa JamiiForums bahati mbaya miaka hiyo ya mwishoni ya 90 bado mlikuwa katika Zipu za Baba zenu ila kwa Wakongwe tulikuwepo na mpaka hii leo sijaona bado Harusi ya Kuizidi hiyo.
Ilikuwa ni Harusi ya Mtoto wa Mzee Rupia ( Tajiri wa Kihistoria Tanzania ) na Binti yake Mzee Mramba ( aliyekuwa Waziri wa Fedha ) ambapo Harusi yao ilifanyika ndani ya Meli, Watu tulikunywa na kula Wiki Mbili na kila Kitu kilikuja na Meli kutoka huko ilikotoka na baada ya Harusi ikaondoka.
Cha Kusikitisha zaidi pamoja na Mbwembwe zote hizi ( hizo ) Harusi hii ilidumu kwa Wiki Mbili tu sababu kubwa ni Mke ( Bibi Harusi ) kukataa Kutekeleza Majukumu yake kwa Mumewe ( siyo Kufanya Ngono ) na kutaka kila Kitu kifanywe na Beki Tatu / Dada wa Kazi na hatimaye wakashindwana.
Ulikuwa ukienda Posta kwa Shughuli zako ukisikia tu hamu ya Gambe ( Bia ) basi unaelekea ilipo Meli na Kuchukua zinazokutosha kisha unaendelea na Ratiba zako za Kimaisha. Na Watu wengi walijifunzia Kulewa katika hizi Bia za Bure za iliyokuwa Harusi ya Mtoto wa Mzee Rupia na Binti wa Mzee Mramba.
Nasikia Mlimani City Bia za Uchoyo!!!!!