Mnafiki Wa Kujitegemea
JF-Expert Member
- Dec 30, 2022
- 4,878
- 8,063
Kama anaweza kuwafutia baadhi ya watu kesi halafu za ugaidi hatufai.Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kuingia madarakani mwaka 2021 na kuombwa sana na Wanachadema na makundi mbalimbali kwenye jamii kuhusu kufutiwa kesi ya Ugaidi iliyokuwa inamkabili Mh Freeman Mbowe na wenzake,kwa hekima kubwa na kulinda 4R's zake alifanya hivyo!
Kupitia kwa Mzee Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa awamu ya Nne aliwahi kusikika kwamba Mbunge wa zamani wa Arusha Godbless Lema alimpigia simu akimuomba amwombee kwa Rais Samia ili aweze kurudi nyumbani bila kukamatwa wala kushitakiwa!Mh Rais Samia akakubali "Majamaa" wakarudi!
Kanisa la Katoliki Tanzania(TEC) nao juzi kupitia Rais wa TEC Mhashamu Pisa, wakatumia "udhaifu" ule ule wa "upole"wa Mama Samia Suluhu Hassan"kumuamuru" kuwaachia mara moja na tena bila masharti Ndugu Tundu Lissu kwa vile alikuwa akidai "haki"
Kwa style ile ya Chadema tena ya kuomba na kutoa amri kwa Serikali hii,Makamu Mwenyekiti wao John Heche ameitaka Serikali imwachie Tundu Antipas Lissu kwani hana KOSA la Uhaini!
HAYA NDIO MAKOSA AMBAYO MH RAIS MAMA YANGU SAMIA ATAKUWA ANAFANYA MARA KWA MARA KATIKA KULINDA/KUBOMOA UHURU WA MAHAKAMA!
I.Safari hii ni muhimu ili Serikali ithibitishe uhalali wa mashitaka yake hata ya huko nyuma dhidi ya Wapinzani ni muhimu sana Mahakama ya Tanzania ipewe "heshima" mpaka "kipindi" kiishe!
Uhalali wa mashitaka ya Nyuma na mashitaka ya Sasa kwa Wapinzani yanategemea sana mchakato wa kisheria Uchukie nafasi yake na watu either wawe "convicted" au "kushinda kesi zao then Rais kwa huruma yake anaweza kuamua vinginevyo!
Hii style ya "kufuta kesi" inaipaka matope Serikali lakini pia "inacompromice" sana Uhuru wa Mahakama zetu katika kutoa Haki kwa watu!Mh Rais asikubali tena "tabia hizi"!
II.Kama kweli Ndugu Tundu Antipas Lissu kwa matamshi yake yale alikuwa hana KOSA la Uhaini ni vizuri tuipe Mahakama nafasi ya kutafsiri Sheria ya Uhaini dhidi ya Matendo na matamshi ya Tundu Antipas Lissu ili kwanza tuwe na uelewa wa pamoja kuhusu mambo haya!
III.Tafsiri ya Sheria ya makosa ya Uhaini kwa Wanasiasa wetu wa Upinzani inapewa TAFSIRI Finyu mno kwamba Tundu Lissu hana Jeshi wala kikundi cha msituni kwahiyo hawezi kuwa Mhaini!
Uhaini sometime unakuwa "defined" kama vile uwepo wa attempt(s)za kutaka (I) "kumobilize" watu kutaka kupindua mifumo halali ya Serikali yao (II)kutishia Serikali halali na (III)Kujipanga kwa kurudia maneno/ujumbe ule ule wa kutaka kupindua mifumo halali ya Nchi(Uwepo wa nia).
Ni kujidanganya kuwa Mhaini lazima awe na Jeshi au Mwanajeshi au kuwa na kundi la waasi ili aweze kupindua Nchi!Rejea Mapinduzi katika Nchi mbalimbali ambayo yalifanyika kwa "kumobilize" watu tu/maandamano mitaani kuingia Ikulu!(Sri-Lanka).
Ili "sura" ya Mh Rais Samia this time isichafuke ni vizuri mchakato wa kupata haki ufuatwe kama unavyofuatwa na wengine waliopo /mahabusu Magereza!
Kesi hii ya Ndugu Lissu inaweza "either (I)kuichafua Serikali kwa kuifuta as usual au (II)kuisafisha Serikali na Mahakama kwa kuendelea nayo kwa kuruhusu mchakato wa Sheria kuchukua nafasi yake!
Kitu muhimu ni kuzingatia tu ile slogan kwamba "Justice Delayed, Justice Denied".Haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyoporwa!
Hii kesi ni muhimu sana katika kuheshimisha Mahakama ya Tanzania na kuheshimu dola/Sheria lakini pia kumpa haki(- au +)ambayo Ndugu yangu Tundu anastahili mbele ya Sheria za Nchi! hii bila kumpendelea wala kumuonea!
Kwa nini hajawafutia watuhumiwa wa wengine ila hao tu?
Vp,hakuingilia uhuru wa mahakama hapo?
Kama ni kweli basi hatufai hata kidogo maana kuna watu wanateseka kwa kunyimwa haki zao wakati waliopaswa kufungwa wana neemeka.
Hivyo siyo mtu mzuri,au nasema uongo ndugu zangu?